Ndege hazitui Tabora wabunge mnafanya nini?

Bijou

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,219
335
Mkoa wa Tabora ni chimbuko la uhuru wa nchi ya Tanganyika kwa wakati huo, lakini imekubuhu na matatizo lukuki, train ya kusuasua, barabara ni za tope hakuna lami inayounganisha mkoa huu (shame).


Kimbilio la dharura lilikuwa ndege, ATCL iliingia mitini, ikabaki precision, nayo imeacha kutua kwa miezi kadhaa kwani uwanja ule wa tope haujakarabatiwa. Jamani wana Tabora, wabunge wanafanya nini kusaidia maendeleo ya mkoa wa tabora?

Inauma sana
 
wanaongoza klabu za mpira na wote wanaishin dar



kweli ndugu yangu wala hukukosea kabisa, rage, kapuya , sitta, mfutakamba uliyoko kwenye wizara yenye dhamana mliho?????? Au ndiyo wote mmejichimbia dalisalama????
 
kwa hali hii,hatuna haki ya kulalamika kama kenya wakijenga hiyo airport karibu na border yetu..si wanatusaidia kuunganisha usafiri bana!
 
Mkoa wa Tabora ni chimbuko la uhuru wa nchi ya Tanganyika kwa wakati huo, lakini imekubuhu na matatizo lukuki, train ya kusuasua, barabara ni za tope hakuna lami inayounganisha mkoa huu (shame).


Kimbilio la dharura lilikuwa ndege, ATCL iliingia mitini, ikabaki precision, nayo imeacha kutua kwa miezi kadhaa kwani uwanja ule wa tope haujakarabatiwa. Jamani wana Tabora, wabunge wanafanya nini kusaidia maendeleo ya mkoa wa tabora?

Inauma sana

Baada ya mechi ya leo na kusitokee migogoro ya kimaslahi pale msimbazi...ndipo ungeuliza swali kama hili. Alhaaj mmiliki wa VOT tunae tu hapa mjini Dar tukigongana nae kwenye migahawa, wengine wanatazama nafasi zao kwenye chama na kashfa ya uanzishwaji wa CCJ...wana Tabora tusahau kwa muda maendeleo kwa miaka ya karibuni.
 
Barabara ya Nzega-Puge-isikizya mpaka TBR mjini ...ndo inajengwa,
Barabara ya Kipalapala, pangale, Sikonge...mmmh!!
Barabara ya TBR mjini-Ibiri-Ibambo-Ulyankulu...mmmh!
Barabara ya TBR-Tumbi-Lolangulu-Usoke-Urambo-Kaliua...mmmh!
Barabara za mjini ndo usiseme...mmmh
Barabara za kwenda Itaga-mpaka kule beach ya mabwawa (igombe)...mmmh usiseme,
Barabara ya (walau) kuelekea kwenye hospitali za mission Ndala & Nkinga...mmmh weeee usiulize,

Hii ndio TBR yetu, mboka, Unyamwezini, Kitovu cha uhuru, Unyanyembe....ndege, reli...tusahau.
 
Na siye Minyamwezi Mipumbavu sana..... Acha ziache kabisa kutua maana tumezidi na CCM.

Kama kuna hela ya Serikali, kwa nini wasizipeleke mikoa ya Wakorofi ili kujionyesha wanafanya kazi?

Tabora hata ukiichapa viboko na kuiambia itembee uchi kwa ajili ya CCM, itafanya hivyo.....

Sasa wasiwasi wa nini? Serikali, tafadhali pelekeni pesa zenu sehemu wanapozihitaji.

Hata hiyo barabara ya Nzega Tabora mwaweza kuiacha na nendeni mkajenge walau Singida kwa Tundu Lissu.

Au zichukueni na mkamalizie uwanja wa ndege wa Mbeya maana huko wapanda ndege watakuwa wengi kuliko sisi.....
 
Inakuwaje hamna miundombinu hali wabunge wenu wanajitapa kuwa ni watu wa viwango? Pengine hivyo viwango vinatumika kujiletea umaarufu binafsi badala ya maendeleo ya watu!!
 
Back
Top Bottom