Masha na wanaomshabikia jueni kuendesha shirika la ndege sio kuuza njegere

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
Anaandika Mwamba wa Kaskazini

Nimemsikia Lau Masha anayejitambulisha kama mmiliki wa Fastjet akilalama kuhusu shirika lake na baadhi ya wapokea mambo bila kutafakari wakiungana naye tena kwa kwenda mbali wakidai eti fastjet inauawa na Serikali kuipendelea ATCL

Nianze kwa kusema na kusisitiza sote tunaochangia mjadala huu tutulize akili kwanza: na tukibaliane kabisa kuwa biashara ya ndege sio njegere. Kwanini?

*_SIO NJEGERE NI NINI?_*

Biashara ya ndege duniani kote ni "highly regulated enterprises" kwa maana ya usalama kwanza na pili abiria kujisikia wako maridhawa na kisha hayo mengine mnauotaka ndio yatokee baadaye.

Siku nilipomuona Mhe. Masha tena akijitambulisha kuwa mmiliki mpya amekwenda kupambana na wateja waliocheleweshwa siku kadhaa kwa safari za fastjet kuhairishwa hairishwa niliamini kabisa wakili Masha biashara hii haiwezi labda asaidiwe kuweka mifumo.

Kwanza alishindwa kujibu maswali kwa ufasaha kwa sababu yeye sio mtu wa technical, pili akaahidi ahadi zisizoeleweka mara baada ya saa 1 ndege itaruka mara akigeuka akaulizwa swali kama hilo na mteja mwingine anabadili majibu anasema kama 2 hours hivi itaruka.

Kwa kifupi haijawahi kutokea duniani mmiliki akawa competent kujibu na kuwaridhisha wateja masuala ya kiufundi. Hii tu inaonesha Masha haiwezi biashara hii.Waliomwachia shirika wamekosea sana.

Ndio maana nchini India shirika moja la ndege limewahi kuzuiwa kurusha ndege kwa kukosa tu operations manager sembuse matatizo lukuki waliyo nayo fastjet kwa sasa.

*USALAMA NA HUDUMA BORA AU MATAKWA YETU?*

Masha na sasa wanaomtetea hawaonekani kuelewa tatizo...yeye anazidi kulalamika kuwa anazuiwa kuingiza ndege. Nadhani hajaelewa.Nirudie tena katika usafiri wa anga makubwa ambayo hayawezi kuwa na siasa ni haya mawili:

*A* Usalama: ndege za fastjet sijui zina nini kwa sasa kila siku ziko matengenezo...hii ni hatari sana kiusalama.Ndege huwa ina mileages za kufikia kisha kwenda matangenezo na hujulikana kimataifa labda kwa dharura...sasa fastjet sio dharura ni kadhia ya kila siku ziko matengenezo na lawama zimejaa pale airport na TCAA wanaopata madhara makubwa kila siku wamepata kusema labda kuna mtu Serikalini ana hisa fastjet.

Ndege inatoka Dar ikifika Mwanza inatengenezwa siku 3 ndio iruke tena. Nilidhani Watanzani tuliolalamika sana na kuumizwa sana hatimaye tungeipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini kwa hatua za kuwabana kabla ya maafa kumbe watanzania hatuna shukrani ni wale wale.Tunataka ziangaliwe tu ila siku zikileta janga maswali yaanze Waziri ajiuzulu, sijui Serikali ilijua ikanyamaza n.k!

*B* Huduma bora: siamini kama Masha huwa anasafiri na ndege za Fastjet na kama ameshakutana na kadhia ambazo mamia ya watanzania wamekumbana nazo.

Mimi mwenyewe nilishalala Mwanza siku nzima kisa Fastjet na wala hawakuomba radhi wala kunifidia...ndege iliahirishwa kuanzia asubuhi, ikawa mchana, ikawa jioni ikashindikana hadi kesho yake. Na hata hiyo kesho yake sijawahi kukutana na kituko katika maisha yangu kupanda ndege AC zimegoma zinafanyakazi feni tu.Sitasahau.

Rafiki yangu mmoja alilazimika kusafiri usiku kucha kwa gari baada ya fastjet kumyeyusha siku nzima bila kuombwa radhi wala kupewa njia mbadala na alikuwa anawahi mahafali yake muhimu Dar.

Niwaambie tu tunaolitazama suala la kukwama kwa fastjet kwa macho yale yale ya makengeza, ugonjwa mbaya sana unaowasibu baadhi ya watanzania, tujue tu duniani kote baada ya usalama wa ndege husika kinachofuata ni huduma kwa wateja na uhakika wa safari. Kimoja kati ya hivi tu kinatosha kusimamisha leseni hako.

Niwakumbushe msingi wa ndege ni kumfikisha msafiri mahali aendako kwa haraka na kwa ratiba iliyopangwa ili naye awahi shughuli zake nyingine. Mtu mpaka anapanda ndege na kulipa gharama kubwa anasababu ambayo ni muda na uharaka.

Ndio maana hata ATCL ishawahi kupokwa leseni yake na IATA moja ya kero kubwa haikuwa usalama wa ndege wakati ule hata kama zilikiwa sijui mbili za kukodi bali malalamiko yalikuwa mengi ya wateja kufutiwa safari zao mara kwa mara na ubovu mwingine wa huduma.

CAA suspends CemAir's operating licence indefinitely

Air Odisha's UDAN license cancelled for poor performance - The Economic Times-https://m.economictimes.com/industry/transportation/airlines-/-aviation/air-odishas-udan-license-cancelled-for-poor-performance/articleshow/66772902.cms?utm_source=whatsapp_amp&utm_medium=social&utm_campaign=socialsharebuttons - Download ET Markets APP (http://ecoti.in/vC93ob)

Hata Kenya washachukua hatua kama hizi

Kenya cancels licences of two airlines

Hata hapa nchini ATCL pia ishawahi kuzuiwa na TCAA. Ugonjwa wetu ni ule ule kusahau na kuongozwa na matumbo badala ya ubongo.

Hivi sasa nchini Uingereza na kwingineko watu wanadai mabilioni ya fidia kwa kukatizwa safari zao na walau wanalipwa au kwingine mgogoro, hapa fastjet Masha hasemi madeni aliyonayo haelezi maumivu waliyoyapata wasafiri na hasara na haelezi masharti aliyokiuka ya leseni kwa kiwango cha watanzania tuseme tu tunamshukuru Mungu hapajatokea balaa kubwa, halafu anasema tu simple kazuiwa kuleta ndege!

Sasa wale wale ambao janga lingetokea wangeandamana kudai Serikali na taasisi zake zililala, ndio eti wanadai hatua hizi ni za kuipendelea ATC. Sijui tukifungua akili hizi tutakuta tope au uji. Sijui.

Mashirika yote yanayoingia nchini na kupewa leseni ya kutua mbona hayajazuiwa "kuipa upendeleo ATC?"

Kuna mashirika ya ndani mengi tu kama Precision, Coastal Air, Airlink, Auric na wengine mbona wanatimiza masharti na hawajabughudhiwa?

Hivi ile Community Airline iliyoletaga ubabaishaji mkubwa kisha kubanwa na akaja Fastjet nayo ilikuwa ni kuibeba ATC? ATC yenyewe ilipozuiwa ilikuwa kumbeba nani?

Makosa ya fastjet yanaonekana dhahiri lakini makubwa zaidi anayajua Mungu na msimamizi wa sekta TCAA, naamini lau kama TCAA siku moja wakiamua kuanika usanii wa fastjet kiusalama na kihuduma wengi tunaopiga blah blah sijui za kuua soko binafsi, sijui ajira n.k tutatamani kuingia chini ya meza.

Mola endelea kutupa watu makini kila sekta nchini ili huduma zitolewe kwa umakini ili wananchi waliokuwa wanapata shida kubwa na hata wale wanaoonekana kusahau shida hizo wote wapate huduma bora na faraja katika maisha haya ya dunia hii.

Amen.

*Naitwa Mwamba (sema mara tatu) wa Kaskazini.
 
Hivi fastjet wana ndege au walikodi? Wenye ndege zao nasikia wanazitaka zikafanyiwe matengenezo na zikienda hazirudi....
 
Hoja zako ni nzuri sana, ni kweri kulikuwa na kadhia kadhaa kwa hili shirika. Lakina kuliua ili ATCL inawili ni ujinga na upumbavu maana baada ya miaka mitano matatizo hayo uliyoyaorodhesha hapo ndo yatakuwa matatizo ya ATCL kwa sababu moja kuu hakutakuwa na upinzani hvyo business as usual ndo utakuwa mfumo wa uendeshaji wa shirika. Tungeiacha ft ife natural death na si kuinyoga.
iliyafanya hayo madudu kwa kuwa hakukua na mpinzani wa uhakika.
 
Ndo maana kuna mahali nikasema ningependa kusikia na upande wa pili.

Binafsi nimesikia kwamba Fastjet hawana ndege zao wenyewe.

Yaani ndege wanazozirusha wanazikodisha....sasa sijui hasa ukweli ni upi...
 
Nikisikia mahali hawana ndege, wamekodi na wanadaiwa na wenye ndege na mamlaka ya anga au uwanja tz. Wenye ndege wanataka zikafanyiwe matengenezo na zikienda hazirudi, huku zimepigwa pin kwasababu ya madeni.
 
Hoja zako ni nzuri sana, ni kweri kulikuwa na kadhia kadhaa kwa hili shirika. Lakina kuliua ili ATCL inawili ni ujinga na upumbavu maana baada ya miaka mitano matatizo hayo uliyoyaorodhesha hapo ndo yatakuwa matatizo ya ATCL kwa sababu moja kuu hakutakuwa na upinzani hvyo business as usual ndo utakuwa mfumo wa uendeshaji wa shirika. Tungeiacha ft ife natural death na si kuinyoga.
iliyafanya hayo madudu kwa kuwa hakukua na mpinzani wa uhakika.
Nani kaiua fastjet?
 
Anaandika Mwamba wa Kaskazini

Nimemsikia Lau Masha anayejitambulisha kama mmiliki wa Fastjet akilalama kuhusu shirika lake na baadhi ya wapokea mambo bila kutafakari wakiungana naye tena kwa kwenda mbali wakidai eti fastjet inauawa na Serikali kuipendelea ATCL

Nianze kwa kusema na kusisitiza sote tunaochangia mjadala huu tutulize akili kwanza: na tukibaliane kabisa kuwa biashara ya ndege sio njegere. Kwanini?

*_SIO NJEGERE NI NINI?_*

Biashara ya ndege duniani kote ni "highly regulated enterprises" kwa maana ya usalama kwanza na pili abiria kujisikia wako maridhawa na kisha hayo mengine mnauotaka ndio yatokee baadaye.

Siku nilipomuona Mhe. Masha tena akijitambulisha kuwa mmiliki mpya amekwenda kupambana na wateja waliocheleweshwa siku kadhaa kwa safari za fastjet kuhairishwa hairishwa niliamini kabisa wakili Masha biashara hii haiwezi labda asaidiwe kuweka mifumo.

Kwanza alishindwa kujibu maswali kwa ufasaha kwa sababu yeye sio mtu wa technical, pili akaahidi ahadi zisizoeleweka mara baada ya saa 1 ndege itaruka mara akigeuka akaulizwa swali kama hilo na mteja mwingine anabadili majibu anasema kama 2 hours hivi itaruka.

Kwa kifupi haijawahi kutokea duniani mmiliki akawa competent kujibu na kuwaridhisha wateja masuala ya kiufundi. Hii tu inaonesha Masha haiwezi biashara hii.Waliomwachia shirika wamekosea sana.

Ndio maana nchini India shirika moja la ndege limewahi kuzuiwa kurusha ndege kwa kukosa tu operations manager sembuse matatizo lukuki waliyo nayo fastjet kwa sasa.

*USALAMA NA HUDUMA BORA AU MATAKWA YETU?*

Masha na sasa wanaomtetea hawaonekani kuelewa tatizo...yeye anazidi kulalamika kuwa anazuiwa kuingiza ndege. Nadhani hajaelewa.Nirudie tena katika usafiri wa anga makubwa ambayo hayawezi kuwa na siasa ni haya mawili:

*A* Usalama: ndege za fastjet sijui zina nini kwa sasa kila siku ziko matengenezo...hii ni hatari sana kiusalama.Ndege huwa ina mileages za kufikia kisha kwenda matangenezo na hujulikana kimataifa labda kwa dharura...sasa fastjet sio dharura ni kadhia ya kila siku ziko matengenezo na lawama zimejaa pale airport na TCAA wanaopata madhara makubwa kila siku wamepata kusema labda kuna mtu Serikalini ana hisa fastjet.

Ndege inatoka Dar ikifika Mwanza inatengenezwa siku 3 ndio iruke tena. Nilidhani Watanzani tuliolalamika sana na kuumizwa sana hatimaye tungeipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini kwa hatua za kuwabana kabla ya maafa kumbe watanzania hatuna shukrani ni wale wale.Tunataka ziangaliwe tu ila siku zikileta janga maswali yaanze Waziri ajiuzulu, sijui Serikali ilijua ikanyamaza n.k!

*B* Huduma bora: siamini kama Masha huwa anasafiri na ndege za Fastjet na kama ameshakutana na kadhia ambazo mamia ya watanzania wamekumbana nazo.

Mimi mwenyewe nilishalala Mwanza siku nzima kisa Fastjet na wala hawakuomba radhi wala kunifidia...ndege iliahirishwa kuanzia asubuhi, ikawa mchana, ikawa jioni ikashindikana hadi kesho yake. Na hata hiyo kesho yake sijawahi kukutana na kituko katika maisha yangu kupanda ndege AC zimegoma zinafanyakazi feni tu.Sitasahau.

Rafiki yangu mmoja alilazimika kusafiri usiku kucha kwa gari baada ya fastjet kumyeyusha siku nzima bila kuombwa radhi wala kupewa njia mbadala na alikuwa anawahi mahafali yake muhimu Dar.

Niwaambie tu tunaolitazama suala la kukwama kwa fastjet kwa macho yale yale ya makengeza, ugonjwa mbaya sana unaowasibu baadhi ya watanzania, tujue tu duniani kote baada ya usalama wa ndege husika kinachofuata ni huduma kwa wateja na uhakika wa safari. Kimoja kati ya hivi tu kinatosha kusimamisha leseni hako.

Niwakumbushe msingi wa ndege ni kumfikisha msafiri mahali aendako kwa haraka na kwa ratiba iliyopangwa ili naye awahi shughuli zake nyingine. Mtu mpaka anapanda ndege na kulipa gharama kubwa anasababu ambayo ni muda na uharaka.

Ndio maana hata ATCL ishawahi kupokwa leseni yake na IATA moja ya kero kubwa haikuwa usalama wa ndege wakati ule hata kama zilikiwa sijui mbili za kukodi bali malalamiko yalikuwa mengi ya wateja kufutiwa safari zao mara kwa mara na ubovu mwingine wa huduma.

CAA suspends CemAir's operating licence indefinitely

Air Odisha's UDAN license cancelled for poor performance - The Economic Times-https://m.economictimes.com/industry/transportation/airlines-/-aviation/air-odishas-udan-license-cancelled-for-poor-performance/articleshow/66772902.cms?utm_source=whatsapp_amp&utm_medium=social&utm_campaign=socialsharebuttons - Download ET Markets APP (http://ecoti.in/vC93ob)

Hata Kenya washachukua hatua kama hizi

Kenya cancels licences of two airlines

Hata hapa nchini ATCL pia ishawahi kuzuiwa na TCAA. Ugonjwa wetu ni ule ule kusahau na kuongozwa na matumbo badala ya ubongo.

Hivi sasa nchini Uingereza na kwingineko watu wanadai mabilioni ya fidia kwa kukatizwa safari zao na walau wanalipwa au kwingine mgogoro, hapa fastjet Masha hasemi madeni aliyonayo haelezi maumivu waliyoyapata wasafiri na hasara na haelezi masharti aliyokiuka ya leseni kwa kiwango cha watanzania tuseme tu tunamshukuru Mungu hapajatokea balaa kubwa, halafu anasema tu simple kazuiwa kuleta ndege!

Sasa wale wale ambao janga lingetokea wangeandamana kudai Serikali na taasisi zake zililala, ndio eti wanadai hatua hizi ni za kuipendelea ATC. Sijui tukifungua akili hizi tutakuta tope au uji. Sijui.

Mashirika yote yanayoingia nchini na kupewa leseni ya kutua mbona hayajazuiwa "kuipa upendeleo ATC?"

Kuna mashirika ya ndani mengi tu kama Precision, Coastal Air, Airlink, Auric na wengine mbona wanatimiza masharti na hawajabughudhiwa?

Hivi ile Community Airline iliyoletaga ubabaishaji mkubwa kisha kubanwa na akaja Fastjet nayo ilikuwa ni kuibeba ATC? ATC yenyewe ilipozuiwa ilikuwa kumbeba nani?

Makosa ya fastjet yanaonekana dhahiri lakini makubwa zaidi anayajua Mungu na msimamizi wa sekta TCAA, naamini lau kama TCAA siku moja wakiamua kuanika usanii wa fastjet kiusalama na kihuduma wengi tunaopiga blah blah sijui za kuua soko binafsi, sijui ajira n.k tutatamani kuingia chini ya meza.

Mola endelea kutupa watu makini kila sekta nchini ili huduma zitolewe kwa umakini ili wananchi waliokuwa wanapata shida kubwa na hata wale wanaoonekana kusahau shida hizo wote wapate huduma bora na faraja katika maisha haya ya dunia hii.

Amen.

*Naitwa Mwamba (sema mara tatu) wa Kaskazini.

Baada ya yote ni vyema kuwakumbusha wageni ,(ATCL)inayozaliwa upya , ule usemi wa wahenga
" ukiona mwenzio ananyolewa......"
 
Ukiona ndege inapaa ujue imakaguliwa na kuwa salama kwa safari endapo mkaguzi hakifanya uzembe. Kama alikuwa anaendelea kupata wateja, aliyeliua hili shirika ni nani?
 
Mmiliki gani huyo anajeuri ya kununua ndege? Ashalipa madeni?
Kama kanunua hisa za FT 68% inamaana kayanunua na madeni yake ni wajibu wake kuyalipa na anajua ni jinsi gani ya kuyalipa....

Kuhusu uwezo wake wa kununua ndege siujui lakin si wa kubezwa. Anaweza asinunue kama magu alivyotumia kodi zetu kununua na akakodi kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake..

Nikunong'onezi Masha si level yako
 
Back
Top Bottom