Ndani yake

Ndani yake

Yes Yes Yo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2014
Posts
232
Reaction score
99
Umewahi Kumwona Kuku Anayejaribu Kumdonoa Panzi Ndani Ya Chupa Ya Soda?
Yule Panzi Anakuwa Na Mashaka Na Hofu Kila Mara Kuku Anapochukua Hatua Ya Kuikaribia Chupa Na Kujaribu Kudonoa; Akili Ya Panzi Inadhani Kwamba ULE NI MWISHO WAKE.... Lakini Kwa Upande Wa Pili; Kuku Anapomuona Panzi Ndani Ya Chupa Anafurahi, Anadhani Tayari Amepata Kitoweo, Anaisogelea Ile Chupa Kwa Kiburi Na Uchu Halafu Anadonoa; Halafu Anashangaa Mdomo Wake Umegonga "KITU KIGUMU" Halafu Anarudi Nyuma ANAJIPANGA TENA NA KUCHUKUA HATUA YA KUJARIBU NA KUJARIBU Mpaka Pale ANAPOKUBALI KWAMBA HAIWEZEKANI KUMPATA "Yule Panzi Ndani Ya Chupa Japo Anamwona Na Anamtamani"

TUNACHOJIFUNZA HAPA:
JAMBO LA KWANZA:

Panzi Ni Mwanadamu Wa Kawaida [Kama Mimi Na Wewe] Ambaye Kutokana Na Dhambi AMEKUWA MNYONGE Kwa KUKU [IBILISI]!
Huyu Panzi [Mwanadamu Mwenye Udhaifu] Akiwa Nje Ya Chupa [YESU KRISTO] Anakuwa DHAIFU, MNYONGE NA WA KUONEWA NA ADUI YAKE KUKU [SHETANI]... Lakini Akichukua UAMUZI WA BUSARA WA KUINGIA KWENYE CHUPA [YESU KRISTO] Kupitia MLANGO MWEMBAMBA WA CHUPA [WOKOVU] Tayari Anakuwa Amepata UHAKIKA WA USALAMA WA MAISHA YAKE Ilimradi ASITOKE NDANI YA CHUPA [ASIUACHE WOKOVU NA KURUDI TENA DHAMBINI] Maana Akirudi Tu Nje ATAKUWA CHAKULA CHA KUKU [IBILISI]!


JAMBO LA PILI:

Chupa INAONESHA [TRANSPARENT] Hivyo Panzi Anamuona Kuku Na Kuku Anamuona Panzi; Wote Wanaonana!
Ndivyo Ilivyo KWA MTU ALIYEOKOKA NA KUINGIA NDANI YA YESU [CHUPA] Ataendelea KUMWONA ADUI YAKE SHETANI NA VITISHO VYAKE KUPITIA Majaribu, Changamoto, Matatizo Na Hila Zote Za Yule Adui! Na Pia ADUI Naye Ataendelea Kumwona Huyu MTU NDANI YA CHUPA Na ATAFANYA KILA HILA NA MBINU "Kumtisha, Kumtia Hofu, Kumwogopesha Na Ikiwezekana Huyu Mtu [PANZI] Aruke Na Kutoka Ndani Ya Chupa Halafu AMAKAMATE KWA URAHISI"

Usalama Wa Panzi Ni KUAMINI UBORA, UIMARA NA NGUVU YA UKUTA WA CHUPA Katika Kudhibiti Kila SHAMBULIO LA ADUI KUKU!
Kama Panzi HATAAMINI Bali Akayumbishwa Na HISIA ZAKE Badala Ya UHAKIKA ALIOPEWA NA NGUVU ZA UKUTA WA CHUPA Atajikuta Anapata HOFU Na Kuanza KURUKARUKA Na Mwishowe ATATOKA NDANI YA CHUPA NA KUWA CHAKULA CHA Adui Yake KUKU!!
Hiki Ndicho Kinachowakuta WALIOOKOKA WENGI Wanatishwa Na MNG'URUMO ZA SIMBA "AZUNGUKAYE AKITAFUTA MTU AMMEZE" Hivyo WANAINGIWA NA MASHAKA NA HOFU Wanasahau AHADI YA UKUTA WA CHUPA [NGUVU YA MUNGU NA NENO LAKE] Na Wanaanza KURUKARUKA KILA ADUI AKIJA KUDONOA Na Mwishowe WANAJIKUTA TAYARI WAMETOKA NJE YA CHUPA NA KUWA CHAKULA CHA ADUI YAO IBILISI!

Lakini KUNA PANZI WALIOELEWA [WALIOKOMAA] Hawa WANAAMINI UKUBWA NA NGUVU YA UKUTA WA CHUPA; Ndiyo WANAMUONA ADUI NA KILA ANALOJARIBU KUWATISHA NALO Lakini WANAJUA KWAMBA, "ILI AWAPATE LAZIMA AIVUNJE CHUPA" Kitu Ambacho Mdomo Wa Kuku HAUWEZI!

Hawa WANAZIAMINI AHADI ZA NENO LA MUNGU BILA KUJALI NINI ADUI ANALETA KINYUME CHAO... Wanajua Ya Kwamba, "BWANA NI NGOME NA MWAMBA WAO" Wanaelewa HAKUNA CHA KUWAANGUSHA WALA KUWADHURU MAADAMU WAMEDUMU KATIKA UTULIVU NA KUTOTOKA NDANI YA CHUPA!

Asomaye Na Afahamu.
"HATA IMEKUWA MTU AKIWA NDANI YA KRISTO YESU, YA KALE YAMEPITA; TAZAMA! YOTE YAMEKUWA MAPYA" (2Kor 5:17).
"NDANI YAKE TUNAISHI, TUNAKWENDA NA KUWA NA UZIMA WETU" (Matendo 17:28).
"NAYE ALITUOKOA TOKA NGUVU ZA GIZA; AKATUHAMISHA NA KUTUINGIZA KATIKA UFALME WA MWANA WA PENDO LAKE" (Wakolosai 1:13).
 
Na wasioamini katika Yesu, hawako salama asilani?
 
Amen mtumishi.... ni neno la faraja sana katika maisha ya yetu kila siku......huyu kuku huyu....dah!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom