Kitombile
JF-Expert Member
- Mar 21, 2021
- 6,656
- 7,269
Hakuna kama yeye, namkubali sana Rais wangu Samia hakika Mungu ampe maisha marefu hazidi kufanya mambo makubwa zaidi🙏🙏NDANI YA SIKU 100, RAIS SAMIA AMEFANYA MAMBO MAKUBWA
Wanaandika Ndugu Twahir Abasi Kiobya na Denis Shanyangi
Kama kuna jambo lolote linalonipa amani na Faraja kwenye nafsi yangu katika siku 100 zilizopita, basi ni kuona kuwa tuna rais wa aina ya Mama Samia Suluhu Hassan.
1. Ndani ya siku 100 tu za utawala wake, Keshaondoa zimwi la 6% retention fee kwenye mikopo ya elimu ya juu, Hii retention fee ilikuwa ni pasua kichwa sijawahi kuona, mtu ulikywa unalipa lakini deni haliishi, na kinshahara chako kinakwanguliwa tu month after mobth
2.Wale standard 7 waliotimuliwa na Magufuli kipindi cha Uhakiki mama kasema walipwe stahiki zao, Hii ni faraja kubwa kwa ndugu zetu wa darasa la Saba ambao walivuja jasho kwa haki kabisa kwa ajili ya Taifa hili.
3. Serikali ya mama iko serious kwenye kupandisha madaraja ya watumishi wa serikali yaliyosimama kwa miaka 5 ya Magufuli.
4. Samia anarudisha uhuru wa habari kwa mfano online TVs sasa zimefunguliwa
5. Wafanyakazi wa serikali wamepunguziwa PAYE hadi 8%
7. Ameshatoa bilion 172 kwa ajili ya kuboresha barabara za vijijini angalau barabara hizo ziweze kupitika. Ifahamike kuna watu wanashindwa kuwahisha wajawazito hospitali kujifungua kwa sababu ya barabara mbovu, Hatua hii ya mama itasaidia sana.
8. Serikali yake imeweka utaratibu wa watoto wanaopata ujauzito waendelee na masomo, hili ni jambo zuri katika vita dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi. Maana huwezi kumsaidia mtoto kwa kumfukuza shule maana ukifanya hivyo unamtia yeye na mwanae umasikini wa kutisha, na litakuja kuwa ni mzigo kwa Taifa mbeleni
9. Mama karudisha common sense kwenye suala la Korona, sasa hivi hatusemi tena "Changamoto ya kupumua", bali tunasema Korona—Huwezi kupambana na ugonjwa usiotaka kuuita hata jina lake ukaushinda, lakini sasa hivi tunapambana nao kitaalamu na siyo kienyeji
10. Rais Samia karudisha nidhamu ya wateule, wasijimwambafy na kuzichukulia poa mamlaka, Sasa hivi yule kijana jeuri ananyea ndoo
11. Rais Samia kakataa kupora pesa za watu ili eti kuongeza makusanyo, yeye anataka kodi za haki
12. Rais Samia keshafungulia account za watu zilizofungwa kimagumashi
13. Rais Samia anataka mabenki yatoe interests rate ndogo, anataka 10% ili wananchi waweze kuafford kukopa na kuendesha biashara zao, Riba ya mabenki enzi za nyuma ilikuwa pasua kichwa, ilikuwa inaenda hadi 25%
14. Rais Samia kaamua mradi wa Gesi Lindi uendelee, faida za mradi huu ni kubwa, tutapata gesi kwa ajili ya viwanda vyetu, tutauza nje, na tutazalisha umeme mwingi zaidi.
15. Kesi za Kubambikiza rais Samia kazifuta, watu 172 waliobambikiziwa kesi na TAKUKURU rais Samia keshazifuta, Huu ni utu na ubinadamu ulioje!
16. Mama kafuta adhabu ya kulipa 10% kwa wale wanaochelewa kuanza kulipa mkopo wao bodi ya mkopo
17. Mama Samia keshashusha bei za bando ambazo utawala uliopita uliacha umepandisha na kupelekea kuleta taharuki kubwa nchini, Imagine eti ulikuwa ukiweka sh 2000 hupati GB hata moja, lakini sasa hivi angalau kwa sh 2000 unapata GB 1 na kuendelea
18. Rais Samia keshafanikisha uuzwaji wa mahindi yetu Kenya Wakulima sasa hivi mioyo yao kwatu, imetukia tuli
19. Rais Samia keshafanikisha utiwaji saini dili la kuiuzia Kenya gesi, hili ni dili safi safi sana, tuna gesi nyingi tu, tukitumia wenyewe na ziada tukiuza na kupata mpunga mrefu itasaidia kwenye uchumi wetu
20. Rais Samia ameendeleza miradi ya kimkakati ya mtangulizi wake, amepeleka hela kwenye miradi yote ya maana ya mtangulizi wake
21. Ndani ya siku zake 100, Rais Samia ameshatangaza ajira zaidi ya 9000 za walimu na wahudumu wa Afya na vijana wetu maelfu kwa maelfu wameomba. Hili ni jambo zuri sana, na huu ni mwanzo tu Mama anaendelea kumwaga ajira kwa vijana wetu.
22. Ndani ya siku 100, Rais Samia kapunguza faini za pikipiki kutoka 30000 hadi 10000, hii habari njema ilioje kwa wenzetu wa bodaboda!
23. Ndani ya Siku 100 za uongozi wake, Rais Samia kapunguza gharama za kuunganisha umeme mijini kutoka shilingi 300000 hadi shilingi 27000, hili ni jambo zuri sana, wananchi wanapunguziwa mzigo wa maisha.
24. Ndani ya siku 100, Mheshimiwa rais Samia, amerejesha imani ya Wawekezaji, Dangote anasema Tanzania chini ya Rais Samia ni mahali pazuri pa kuwekeza, Manji amerudi maana yake confidence ya Wawekezaji na wenye mitaji imeanza kurudi, hii itasaidia wawekezaji kutengeneza ajira zaidi na kulipa kodi serikalini
Kwa hiyo by all Standards, Rais Samia ameupiga mwingi sana ndani ya siku zake hizi 100 za utawala wake.
Na namtabiria makubwa kwa sababu ana Hekima, Utu, Subira, Yuko open minded, Ni mchapakazi sana, ana exposure, ana uzoefu mkubwa.
We are Lucky kuwa mama is our president