Ndani ya dilemma

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,233
Tumekua katika mahusiano toka tukiwa wadogo,...
toka enzi hizo niko form4 na binti huyu akiwa form2.

Ingawa tulikuwa wadogo sana,hatukujua kama tutakuja kuwa na
ndoto za kuoana baadae.Lakini jinsi miaka ilivo kwenda tuliweka malengo
ya kuja kuishi pamoja.

Binti ni mstaarabu sana,siwezi jisema niko vipi ila ndani ya miaka mitano
na unusu tulio kuwa pamoja nilimsaliti na kupata mtoto na dada mwingine.
nilipata mtoto na mtu nisiye kuwa na future nae,na binti huyu nilipo
mweleza,japo ili muumiza kwa mda mrefu sana alikubali kutovunja
uhusiano wetu pale ulipo fikia.

Nampenda sana,na hivi juzi nilipo kwenda nyumbani for christimas,..
nilimwambia mzazi wangu (mama )kuwa nimempenda huyo binti na
tuna tarajia kuishi pamoja.

Alimsifu kwamba ni binti mzuri wa tabia na mstaarabu sana.
na akadai kama tabia aliyo nayo ni ya mama yake (uvumilivu) basi atakuwa mke mwema sana.

Aliniumiza mwisho aliposema,kwamba mama mdogo wa huyo binti alizaa na mjomba wangu (hawa kuoana).

Nilipo muuliza binti kuhusu hiyo habari akasema ni kweli,na mtoto ana fanana kweli na mjomba wangu
lakini yeye haoni kama ni kikwazo maana hawa kuoana.

Binafsi naona kama ni tatizo/kizingiti kimeingia kati yetu.
Pamoja na hivo,nadhani kwendelea mbele ni rahisi kuliko kurudi nyuma baada ya kuona kizingiti hiki.

Sina uhakika kama ni sahihi mimi kuja kuishi kama mke na mume na binti ambaye
mama mdogo wake kazaa na mjomba wangu.

Too bad nimeondoka nyumbani bila kupata ushauri zaidi na siwezi kuongelea this matter on phone.
Nipeni mawazo yenu,niendelee mbele au ni sawa na kuoana na ndugu yangu

Regards,.
Clemmy
 
utakuwa bado unakumbuka mauno ya mzazi mwenzio hamna lolote

rafiki wa mama yake na shangazi yangu ambao kipindi cha ujamaa walishiriana kuchimba kisima kaumuoa aliyekuwa balozi wa kijiji cha mchumba angu.

Ihahusu nini?
Unanzingua bure!
 
Mbona uhusiano uko0 mbali sana
Kwani kinakuzuia nini kuoana na huyo dada
Sioni kikwazo hapo mkuu labda kuna jingine ambalo linakufanya usimuoe huyo dada ila kwa hapo hakuna kitu
dada wa watu ushampa matumaini then tena ghafla unaleta habari za mahusiano ya wajomba na mama yake mdogo
Ingekuwa huyo mjomba ana uhusiano na mama yake na huyo binti hapo ingekuwa mbaya
Ila mama mdogo na mjomba too far uhusiano huo bana
 
tukushauri nini sasa... huo undugu unaulazimishia wewe! katu hauwezi kua ndugu na huyo mtarajiwa wako
 
kuna watu wana matatizo kweli... Yaani wazae wengine uhangaike wewe... Naenda rg, jiandae kwa matusi.

Advice: usije kiomba ushauri wakati una mawazo ya kipuuzi kwa utakua unastahili kupuuzwa
 
Unataka tu kutuongezea idadi ya wadada wanaovunjwa mioyo kila siku. Sasa hebu tueleze hapo undugu wenu unaanzia wapi.
 
msimseme sana,
mama yake mdogo kazaa na kaka yake mama yangu,
kaka wa mama yako ni sawa na mama yako mzazi,
sasa amua mwenyewe lakufanya.
 
utakuwa bado unakumbuka mauno ya mzazi mwenzio hamna lolote

rafiki wa mama yake na shangazi yangu ambao kipindi cha ujamaa walishiriana kuchimba kisima kaumuoa aliyekuwa balozi wa kijiji cha mchumba angu.

Ihahusu nini?
Unanzingua bure!

Sorry,sijui umeongea lugha gani.
Natumia kiswahili,kiingereza,kusukuma,kikurya,kuzanaki, kikabwa na
(kidoogo kijita).
ukiongea lugha hizo nitakuelewa sana.
 
Mbona uhusiano uko0 mbali sana
Kwani kinakuzuia nini kuoana na huyo dada
Sioni kikwazo hapo mkuu labda kuna jingine ambalo linakufanya usimuoe huyo dada ila kwa hapo hakuna kitu
dada wa watu ushampa matumaini then tena ghafla unaleta habari za mahusiano ya wajomba na mama yake mdogo
Ingekuwa huyo mjomba ana uhusiano na mama yake na huyo binti hapo ingekuwa mbaya
Ila mama mdogo na mjomba too far uhusiano huo bana

Thanks rocky,i just need to be sure
kwamba sifanyi kosa
 
sasa undugu hapa uko wapi.....
mtoto atakuita wewe binamu......na mkeo atamuita dada....
mbali sana huko........oa bana.....
 
kuna watu wana matatizo kweli... Yaani wazae wengine uhangaike wewe... Naenda rg, jiandae kwa matusi.

Advice: usije kiomba ushauri wakati una mawazo ya kipuuzi kwa utakua unastahili kupuuzwa

Asante sana genius
 
Sorry,sijui umeongea lugha gani.
Natumia kiswahili,kiingereza,kusukuma,kikurya,kuzanaki, kikabwa na
(kidoogo kijita).
ukiongea lugha hizo nitakuelewa sana.

Hii si sababu ya kuvunja uhusiano na 'mchumba' wako. Kama unamfeel muoe kama humfeel tena mwambie usitake leta visingizio vya Taifa Stars.
 
Hufanyi kosa! Labda kama kuna sababu zingine mbali na hiyo. Kama umempenda kweli muoe ya wajomba na mama wadogo waachie wenyewe. Wazazi wa huyo dada wamekukubali?!
 
Hii si sababu ya kuvunja uhusiano na 'mchumba' wako. Kama unamfeel muoe kama humfeel tena mwambie usitake leta visingizio vya Taifa Stars.

ndo maana idadi ya wanafunzi wanaofeli siku hizi
shule za kata inaongezeka sana.
 
You must be kidding right?
What is the problem here! Mjomba kazaa na mdogo wake, so what? Au unakumbuka maunao ya mzazi mwezio na unatafuta loop hole ya kutokea sio? What a waste!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom