Ndani ya Daladala!......

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,663
7,743
Aisee! Ndani ya daladala kuna kero jamani mtu unaweza kuwa upo kimya unawaza mambo yako kichwani, mara konda au abiria mwenzako akalianzisha utajuta kupanda daladala hilo mbaya zaidi kushuka huwezi maana kama hujachelewa kazini basi nyumbani kwako.

Huu ni uzi maalum wa kushare kero mbalimbali ndani ya daladala na kushirikiana jinsi gani ya kuzitatua. Mnaowahi kukaa siti za dirishani kwenye daladala mnakera sana yaani mnafunga vioo wakati gari limejaa hata pa kuweka pua hakuna tupumuliane kwenye makwapa au?
 
Aisee! Ndani ya daladala kuna kero jamani mtu unaweza kuwa upo kimya unawaza mambo yako kichwani,mara konda au abiria mwenzako akalianzisha ujajuta kupanda daladala hilo mbaya zaidi kushuka huwezi maana kama hujachelewa kazini basi nyumbani kwako.Huu ni uzi maalum wa kushare kero mbalimbali ndani ya daladala na kushirikiana jinsi gani ya kuzitatua....Mnaowahi kukaa siti za dirishani kwenye daladala mnakera sana yaani mnafunga vioo wakati gari limejaa hata pa kuweka pua hakuna tupumuliane kwenye makwapa au?
mkuu huko kwenye dala dala Kuna changamoto kubwa maana hupanda watu wengi sana na kila mtu na tabia yake
 
Au mwenye stress akukanyage umwambie....atakutolea povu SI UPANDE TAXI!!!!!
Hahahaha au wakuambie kama ungekua na haraka ungekwenda tangu jana unakoenda daladala zina vituko sana nakumbuka siku hiyo alipanda mlevi, sasa tulikua tunaelekea home hapo bado tukiwa mbali sana kufika home, vituo kama vinne mbele walokua wanaingia wadada tu na ndani ya daladala alikua yeye dereva na konda ndio wanaume tulipofika kituo cha mbele tena akaingia msada tena yule mlevinakapaza saut dereva hii gar ni ya wanawake tu?? Hakuna aliemjibu tulipofika stand akaingia mkaka kwa zile pombe akaropoka tena hee dereva nishushe hili gar la wanawake mnanipeleka wapi, yan mwanaume peke yangu tu humu ndan dereva akamjib kwa hiyo me pia mwanamke akasema gari zima wawake tunaenda wapi nilicheka sana that day
 
Back
Top Bottom