Ndani ya CCM hakuna Demokrasia ya kukosoa viongozi, utakosolewa ukimaliza muda wako

Abel 2015

Senior Member
Sep 5, 2015
112
55
Katika Awamu Ya Nne Ya Rais Kikwete Hakuna Mwana Chama Yeyote Aliyejitokeza Adharani Kuikosoa Serikali Yake Zaidi Ya Kusifiwa Kua Mchapakazi, Serikali Sikivu, Amejenga Bara Bara Nyingi, Uchumi Umepanda N.K Hakuna Yeyote Aliyewahi Kujitokeza Kuonesha Mapungufu Yake.. Leo Hii Wale Wale Waliokua Wakimsifia Wanatoa Negative Kwake, Kwann Wasingeyatoa Madukuduku Yao Mapema? Kama Sio Unafiki? Magufuli Ajiandae Kukosolewa Na Wanaomsifia Akimaliza Muda Wake.
 
Mkuu hapo umenena kweli. ni kama sasa hivi mtukufu wetu magogoni hatakiwi kukosolewa kabisa. Yaani utadhani malaika. Ila ajue siku atakavyo achia ikulu ataona matusi na kejeli atakazopewa.
 
Hiyo ni ndani ya ccm.... Nje ya ccm je?

Toa kwanza boriti kwenye jicho lako kabla ya kimwambia mwenzio atoe kibanzi
 
Wana mfumo wa 'carrot on a stick' washajua siasa ni njia ya kukimbia shida kwa wanachama wao wengi.

Ili ubaki kundini utakiwi kuwa na mawazo binafsi sawa mwanachama awezi kuwa kinyume na itikadi za chama chochote duniani lakini wao ata mbinu za viongozi wa serikari wanashindwa kuziuliza if you ask me mawaziri get away easily na majibu ya mkato kwa uoga wa wana CCM; mmbunge anaweza uliza swali la msingi akapewa jibu ambalo alikidhi hoja zake bado utamsikia asante waziri.

Kutokana na fikra zao wanadhani kukata posho za wabunge wa upinzani inaweza leta outcome hizo hizo nimependa Msigwa alivyojibu hayuko kwenye siasa kwa sababu za posho.
 
Hiyo hali inasababishwa na wanachama wengi ni wanafiki na waganga njaa. Wanaogopa watakula wapi wakisimamishwa uanachama.
 
Katika Awamu Ya Nne Ya Rais Kikwete Hakuna Mwana Chama Yeyote Aliyejitokeza Adharani Kuikosoa Serikali Yake Zaidi Ya Kusifiwa Kua Mchapakazi, Serikali Sikivu, Amejenga Bara Bara Nyingi, Uchumi Umepanda N.K Hakuna Yeyote Aliyewahi Kujitokeza Kuonesha Mapungufu Yake.. Leo Hii Wale Wale Waliokua Wakimsifia Wanatoa Negative Kwake, Kwann Wasingeyatoa Madukuduku Yao Mapema? Kama Sio Unafiki? Magufuli Ajiandae Kukosolewa Na Wanaomsifia Akimaliza Muda Wake.
Mpelekee taarifa mzungusha mikono, mkuu wa chama akupe chako.
 
Back
Top Bottom