Ryaro wa Ryaro
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 2,659
- 1,430
Swala la Kung'oka hiyo ni ndoto na ukisahau Itakuwa Imekusaidia sana; Badala yake Ungesema IGP na Waziri Waunde Tume ili Kujua Ukweli; Pole sana Maana hata Haujui Serikali ya CCM; Issue ya Mtwara na Uvunjifu wa Haki za Binadamu ni Good job kwa Serikali Sikivu. Yule Mama Mwingereza Mwezi Kipindi cha February/ March alipata kuandika hivi " Serikali ya Tanzania ni sawa na Majambazi yanayotoa Malekezo kwa Majizi ili waende Kuwakamata Vibaka". Maana ya Makala ile ilikuwa ni kwamba Mfumo Mzima wa kiuongozi Umeoza na Kuparalise. Hakuna sehemu ya Kusema ni afadhali, IThe all system is rotten, Ni kweli mama yule alisema Ukweli japo Tuliumia kwani ni hakika kabisa kwamba kwa sasa ya leo ni afadhali kuliko ya Jana... Kwa khali ilivyo sasa, hakuna aliye na uhakika wa Kesho. Vyombo Vya dola Vimekuwa Juu ya Sheria na Mahakama zetu Zimebakia Majengo tu Haki Imeyeyuka kabisa na Dhuruma Imetamalaki. " Wanyonge Tumekwisha".