Nchimbi na Mwema Wang'oke... hata Vuai?

Nchimbi na Mwema Wang'oke... hata Vuai?

Ukitaka kujua jeshi la polisi lina weledi kiasi gani angalai linavyofanya kazi wakati wa vurugu, dharura, au pale ambapo mmojawao anaumizwa. Mambo ambayo yanadaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi na wale wa JWTZ dhidi ya wananchi ni mambo yanayoita watu kuwajibishwa.

Kwamba kuna nyumba zimechomwa na polisi wametoa adhabu ya jumla (collective punishment) wakiingia kwenye majumba ya watu na kusababisha hali ya hofu kwa wananchi badala ya kuonesha weledi na amani toka mwanzo - kwani jambo hili lilijulikana kabla!

Tumeshasema mara nyingi huko nyuma wengine wanaobebwa hawabebeki... Wasije kudhania kuwa kulazimisha amani kwa nguvu namna hii kunawafanya watu wageuka na kuwapenda zaidi... wanachofanya wao wenyewe wanazidi kupandikiza chuki, sumu ya chuki inanyonywa na watoto katika matiti ya mama zao...

Binafsi sielewi kabisa kwanini Nchimbi ni Waziri! I have never understood kwanini ameendelea kuwa Waziri licha ya kuboronga wizara zote alizopitia.. kitu pekee alichowahi kuwa mzuri kwacho (kama naweza kusifikia) ni kuwa Katibu ya Umoja wa Vijana wa CCM... nje ya hapo sijui! KUhusu Mwema ndio wala sitaki ksuema maana nishasema vya kutosha... ingekuwa nchi nyingine angetimuliwa miaka minne nyuma... !

Vuai bado sijajua maana ningependa kusikia kauli yake ya kuhusika kwa JWTZ katika kadhia iliyotokea Mtwara.

Kinachonichosha zaidi ni Nchimbi kuzungumziwa kama mmoja wa watu wanaopigiwa chapuo kugombea uraisi 2015..Ni hatari sana,gari lenyewe bovu halafu tumpe utingo kuliendesha!!
 
ADUI wa jeshi ni wa ndani ya nchi au nje ya nchi?

Philosophia ya jeshi ni kwamba linapambana na adui awe wa nje ama wa ndani. Mkiona kombati zipo mtaani ni bora mkaketi mbali manake kinachoweza kufuatia ni curfew.
 
Mzee Mwanakijiji,

Kupitia mada zako, umekuwa ukitoa ushauri mwingi, mzuri na unaoeleweka kwa urahisi sana kama mlengwa ni mtu mwenye nia njema kwa yale ayafanyayo. Said Mwema, Nchimbi na wengineo ndani ya utwala wa Kikwete wanatoa taswira ya aina ya Serikali tuliyonayo na Rais wa nchi kwa ujumla. Kumshauri ama kumwambia Kikwete awawajibishe hao watu ni sawa na kumwambia ajiwajibishe mwenyewe.

Tusitarajie hata siku moja Kikwete kuwawajibisha hao mawaziri na watendaji ndani ya utwala wake ambao wengi hatujui alitumia vigezo gani katika kufikia uamuzi wa kuwateua na kuwapa hizo nafasi. Kigezo kikubwa pengine ni kufahamiana, urafiki ama pengine kuna nguvu ama ushawishi wa pembeni kuwa nafasi fulani mweke fulani.

Si vyema kuacha kushauri pale inapobidi lakini kwa Kikwete tusitarajie lolote la tofauti hata angeshushwa mshauri kutoka sayari nyingine
 
Ukiona mtu anavichukia vyombo vya ulinzi na usalama wa taifa lake basi anza kumtilia shaka lazima atakuwa ni adui wa vyombo hivyo, maana vyombo vya ulinzi na salama moja ya adui wake ni wahalifu. sasa wewe unavichukia vyombo vya ulinzi na usalama una ajenda gani na usalama wetu. DKT. NCHIMBI, IGP MWEMA, pamoja na Nahodha pigeni kazi ni kutokana na kazi yenu ndio maana hao watu wanapata hata nafasi ya kukaa majukwaani, vijiweni, na katika mitandao ya kijamii kuanza kuwakashifu na kutoa maneno ambayo hayafai, msirudishwe nyuma kazeni buti nyie ni makamanda kushindwa ni mwiko.
 
Kwa hii kadhia ya Mtwara nadhani Polisi wamejitahidi sana kuwa wavumilivu hadi ikaonekana kama wameshindwa kitu ambacho si kweli.
na wala sio kwamba walivumilia bali walitaka wavuke benchmark yao, na ndicho walichokifanya.
Kwa kweli Nchimbi ni majanga!
hivi Nchimbi yye personaly alitakiwa afanyeje?? na je yawezekana kabisa katika utawala wa sheria ukamwajibisha mtawala mmoja ilihali huyu mmoja hatoi maamuzi peke yake??

sasa nashindwa kutofautisha na wale waliosema Mungai ama Kapuya wameua elimu ila wakasahau kwamba hawa hawakuwa wanaamka na kusema la hasha baraza zima la mawaziri walikuwa wanakaa na kukubaliana na hoja zao na wanashiriki direct ama indirect kwenye implementation yake.

to me bado sielewi kabisa nini kipo nyuma ya haya yanayotokea twaweza sema ni gesi kumbe gesi ni kiini macho tu, kwani huyo shaha alomwagiwa tindikali huko zanzibar nae alipinga kuhusu gesi??
 
Kwa hii kadhia ya Mtwara nadhani Polisi wamejitahidi sana kuwa wavumilivu hadi ikaonekana kama wameshindwa kitu ambacho si kweli.

Kwa kweli Nchimbi ni majanga!

Mzee Mwanakijiji,

Kupitia mada zako, umekuwa ukitoa ushauri mwingi, mzuri na unaoeleweka kwa urahisi sana kama mlengwa ni mtu mwenye nia njema kwa yale ayafanyayo. Said Mwema, Nchimbi na wengineo ndani ya utwala wa Kikwete wanatoa taswira ya aina ya Serikali tuliyonayo na Rais wa nchi kwa ujumla. Kumshauri ama kumwambia Kikwete awawajibishe hao watu ni sawa na kumwambia ajiwajibishe mwenyewe.

Tusitarajie hata siku moja Kikwete kuwawajibisha hao mawaziri na watendaji ndani ya utwala wake ambao wengi hatujui alitumia vigezo gani katika kufikia uamuzi wa kuwateua na kuwapa hizo nafasi. Kigezo kikubwa pengine ni kufahamiana, urafiki ama pengine kuna nguvu ama ushawishi wa pembeni kuwa nafasi fulani mweke fulani.

Si vyema kuacha kushauri pale inapobidi lakini kwa Kikwete tusitarajie lolote la tofauti hata angeshushwa mshauri kutoka sayari nyingine

hivi mkuu taffu69 ulitaka labda mawaziri wakushika hizi wizara wawe na sifa zipi za ziada??

je wewe unaamini kabisa kwamba waziri wa mambo ya ndani ama waziri wa ulinzi anaweza kusema ama kutenda lolote bila baraza lote la mawaziri kukubali yatendeke?? na je mkuu wa jeshi la polisi mpaka atumie polis wataka kusema kwamba hakuwasiliana na bosi wake kwanza??

vitu vingine tuangalie uhalisia zaid.

labda nikuulize ni nyumban kwako wanao wanapigana jikoni mbele ya kaka zao na dada zao, kelele zinasikika, dada na kkaka wanawaamua wanashindwa je wataka kuniambia mama akiwagombelezea na kisha kuwaadhibu atakuwa amekosea?? na atakuwa kinyume na matakwa yako??
 
Last edited by a moderator:
Kuna huyu jamaa anaitwa kunduro bompwa anaharibu mada maana hajui hataachokiandika.hivi ukibishana na huyu jamaa naona unapoteza muda.mzee mwanakijiji msamehe tu kuna watu wapo duniani lakini hawajui kwa nini wapo
 
Sijaona kipya kwenye post yako mkuu,wewe unataka polisi wakae na kucheka na watu ambao ni waharifu hayo mawazo yako siyo varid pengine na wewe ni miongoni mwa hawa wachochezi kwa nini hujasema chochote juu wanasiasa waliochochea na wale wanaofanya hizo vurugu,acha mambo ya ajabu.
Utaonaje kipya wakati uwezo wako wa kufikiri ni mdogo? watoto wadogo wanaonyonya ambao wamechomewa makazi yao walifanya uhalifu gani? Polisi wamepata wapi kibali cha kutoa adhabu? kwanini walianza kupora simu na mali za watu ambao wengi walikuwa wapita njia! polisi sasa wanaongoza kwa uhalifu, lakini wewe nawe kwa kuwa unaasili ya uhalifu bila aibu unawapokeza wahalifu wenzio!
 
Sijaona kipya kwenye post yako mkuu,wewe unataka polisi wakae na kucheka na watu ambao ni waharifu hayo mawazo yako siyo varid pengine na wewe ni miongoni mwa hawa wachochezi kwa nini hujasema chochote juu wanasiasa waliochochea na wale wanaofanya hizo vurugu,acha mambo ya ajabu.
Mbona Kikwete ameiba twiga akapeleka uarabuni na wakamchekea? Mbona Pinda alituma watu wa usalama wa majambazi kwenda kumwuua dr. Ulimboka na wakacheka nae!
 
Kinachoendelea Mtwara ni uhalifu kwa wananchi na kibaya kuliko vyote wamebaki yatima bila utetezi wa nguvu sasa.
Na nyie kazi yenu si kubwabwaja tuuu hakuna hata mwenye akili akawasiliana na mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa mtasemaje wamebakia yatima halafu mnachonga tuuuu au ndo mnawalilia hao cdm wenu nilishasema hakuna mwenye shibe aliyewahi kuleta ukombozi mahali popote duniani mnadanganyika bure mtaleta fujo kufurahisha walioshiba lakini zitakuwa ndio kaburi lenu chungeni sana maneno ya Nchimbi serikali sio bibi yako ukacheze nae cha ndimu
 
Mzee Mwanakijiji, nilisha wahi kuandika hapa jamvini ya kuwa haiwezi tokea kiongozi mzuri akafanya kazi na watendaji wabovu, tena kwa mda mrefu.

Hivyo basi Nchimbi, Nahodha na Mwema ni clear reflection ya features za Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Back
Top Bottom