Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 914
- 4,264
Kutumbuana kunarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Makonda kaenda pangani kakutana na mkurugenzi aliyewahi kukorofishana naye kisha amemwelekeza waziri atumbue uteuzi wake huku akijua kabisa wakurugenzi wanateuliwa na Mhe. Rais.
Sitashangaa Makonda kuwa na kiburi chukumwelekeza Mhe. Rais atumbue na kuteua bila kuweka wazi sababu za kufanya hivyo. Tukumbuke huu utaratibu unatumia gharama kubwa sana ambazo hazina tija.
Viongozi wenye kufahamu mifumo ya utendaji wa serikali wanapofanya ziara kama anayofanya nchimbi na Makonda huwa wanaandika ripoti ya kazi. Kupitia hiyo ripoti ndipo ueleza hali waliyokutana nayo kisha kupendekeza wapi panapwaya na nini kifanyike.
Kupitia ripoti hiyo wasaidizi wa Mhe. Rais akiwepo Karibu Mkuu Kiongozi upitia ripoti husika na kufanya uchambuzi ikiwemo kuverify yale yaliyoelezwa kisha kushauri MAMLAKA ya uteuzi nini wafanye..
Mfumo huu unasaidia sana separation of power lakini pia unaondoa hiki kinachotokea sasa cha mtu kumchukia mtendaji kisha anaagzliza aondolewe. Tukiendelea na huu utaratibu wakitibu mwenezi kumwelekeza Mhe rais atumbue tena akiwa kwenye jukwaa tunashusha hadhi ya mamlaka yake.
Lakini pia kwa upande mwingine aliyependekeza kwenye jukwaa aondolewe asipoondolewa utaona umedharaulika. Natumaini hii misingi walipaswa kuisimamia akina Kinana kwa sababu wapo muda mrefu kwenye mfumo wa chama na serikali. Muundo wa sasa wa TAMISEMI upo kwa Mhe. Rais hivyo unapofanya kosa ukatoa maelekezo unamwelekeza Mhe.Rais na siyo Waziri.
Vijana tupunguze miemuko na cheap popularity tufanye kazi kisayansi. Tujifunze kutoa nafasi kwa wakubwa zetu waweze kuheshimika kuliko sisi kujiona ndio kila kitu.
Fanyeni ziara zenu, kamilisheni kazi, andikeni ripoti na mtoe mapendekezo kisha mpeni Mhe.Rais muda wa kutafakari na kutoa maamuzi ya haki. Kama mtaendelea kudhani TAMISEMI ni Mchengelwa mtakuwa mmepotoka. Mamlaka ya uteuzi kwa TAMISEMI ni Mhe. Rais.
Mkitaka kutuelewa sisi wazee wenu mtatuelewa ila mkishupaza shingo mtaishia kufanya siasa majukwaani zisizo na matunda. Kila mtu ana mtu wake, hii ni zamu yenu itumieni kwa busara na hekima.