Nchimbi atambika kwenye kaburi la Gama

Nchimbi atambika kwenye kaburi la Gama

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Baada ya kutemwa uwaziri wa mambo ua ndani mhe. Emmaniel Nchimbi juzi jumamosi alienda kutambikia kwenye kaburi la aliyekuwa kuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Gama.

Taarifa za watu waliokuwa kwenye msafara wa Nchimbi zinasema alifika makabulini hapo kuomba msamaha kwa marehemi Gama kwani anaona yanayotokea pengine ni kwa sababu ua ungomvi wake na Gama..walisema ni kama amechanganyikiwa kwani kutoka kwenye mbio za urais sasa hajiamini hata kuupata udiwani kwani hana ushawishi kabisa kwenye jimbo na alikuwa akiliendesha jimbo kwa mtutu wananchi wakigoma analeta polisi wa kutosha leo ni mbunge wa kawaida hana jeuri ya kuagiza polisi atakavyo.

Maoni yangu:
Nchimbi ukimalizana na Gama njoo Arusha uwaombe msamaha watu uliowauwa kanisa la olasti kwa bomu na wale wa soweto..
 
Teh teh, nchimbi alipata ubunge songea mjini kwa kumpindua Gama kwa kuwahonga wafuasi wa Gama kwa mapesa mengi, nchimbi watu wa songea mjini hata hawamfahamu!
 
Wakati wa kura za maoni huyu jamaa si alichukua wajumbe waliokuwa wanajulikana kumuunga mkono Gama, akajifanya kwenda kupiga kampeni kwao, akawafungia ndani kwa kufuli hadi upigaji kura ukaisha...

Watu wanadhani wataishi milele...
 
Teh teh, nchimbi alipata ubunge songea mjini kwa kumpindua Gama kwa kuwahonga wafuasi wa Gama kwa mapesa mengi, nchimbi watu wa songea mjini hata hawamfahamu!

Sio kuwahonga tu, baada ya kuwahonga aliwafungia ndani hadi kura ya maoni ikamalizika kupigwa...
 
Teh teh, nchimbi alipata ubunge songea mjini kwa kumpindua Gama kwa kuwahonga wafuasi wa Gama kwa mapesa mengi, nchimbi watu wa songea mjini hata hawamfahamu!

nchimbi.jpg
Nchimbi alikuwa pete na kidole na Mkulu kwa hoja kwamba Gama alipokuwa katibu mkuu wa CCM alimtifulia Kikwete kuingia Magogoni kwani Gama aliegemea upande wa Cleupa Msuya. Pamoja na kwamba wote Msuya na Kikwete waliangukia pua kwa Nzee Nkapa, hasira za Kikwete hazikuishia hapo licha ya alichosema tutayamaliza kichama.

Emmanuel Nchimbi wakati huo akiwa mmoja wa viongozi waandamizi wa umoja wa vijana CCM alipata mwanya ili kuchanganya vizuri karata huku akiridhiwa na aliyekuwa mhasimu wa Gama kipindi cha kugombea urais. Bahati mbaya ameshindwa kutumia vizuri nafasi yake, ujuavyo nafasi za ujanjaujanja ambazo zimepatikana kwa gharama kubwa hulindwa kwa gharama kubwa pia. Hatimaye mambo yakiharibika mtu mzimamzima huumbuka hadharani. Maana ile ya kukimbia na sanduku la kura za Meya wa Songea alifanikiwa kulizima, hilo limemtokea puani.
 
@ Tuko kwahiyo alikuwa hawaamini kweli Nchimbi hiyo scenario vijana wanaita mbwanda kala mbwanda.
 
Baada ya kutemwa uwaziri wa mambo ua ndani mhe. Emmaniel Nchimbi juzi jumamosi alienda kutambikia kwenye kabuli la aliyeliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Gama
Taarifa za watu waliokuwa kwenye msafara wa Nchimbi zinasema alifika makabulini hapo kuomba msamaha kwa marehemi Gama kwani anaona yanayotokea pengine ni kwadababu ua ungomvi wake na Gama..walisema ni kama amechanganyikiwa kwani kutoka kwenye mbio za urais sasa hajiamini hata kuupata udiwani kwani hana ushawi kabisa kwenye jimbo na alikuwa akiliendesha jimbo kwa mtutu wananchi wakigoma analeta polisi wa kutosha leo ni mbunge wa kawaida hana jeuri ya kuagiza polisi atakavyo.

Maoni yangu:
Nchimbi ukimalizana na Gama njoo Arusha uwaombe msamaha watu uliowauwa kanisa la olasti kwa bomu na wale wa soweto..

Crashwise - Edit hii habari tafadhali, makosa mengi mno.
 
Wakati wa kura za maoni huyu jamaa si alichukua wajumbe waliokuwa wanajulikana kumuunga mkono Gama, akajifanya kwenda kupiga kampeni kwao, akawafungia ndani kwa kufuli hadi upigaji kura ukaisha...

Watu wanadhani wataishi milele...

gama.jpg pe_108.jpg View attachment 137051
Picha kulia Gama na kati James Komba na kushoto Nchimbi

Songea huko kuna vituko, maana hayati Laurence Gama si la Emmanuel Nchimbi tu ndilo lililomsumbua kichwani hadi kifo chake, lipo jingine watu wa Songea wanalijua nalo lina mahusiano na hayati Archbishop James Yefunani Komba.

Kuna kitu ambacho walipishana wakati Askofu Mkuu Yefunani Komba alipomwangalisha Gama kimwenendo ujue Gama alikuwa Mkatoliki hali kadhalika Askofu Komba alikuwa mwazi sana na wa kujiamini. Gama akaja juu kwamba yeye ni mtu mkubwa kiserikali anatakiwa aheshimiwe na hivyo atamshikisha adabu Askofu Mkuu Yefunani Komba. Gama akaamrisha kikosi chake kwenye kijiji cha Lituhi kando ya mto Luhuhu mwambao wa Ziwa Nyasa alikozaliwa Askofu Mkuu Yakobo (James) Komba. Palikuwa na hospitali kubwa iliyokuwa inahudumia mwambao wa Ziwa Nyasa, akaifunga pale hospitali, parokia Lituhi akaifunga, shule na kila kitu kisha kuhamishia kwa nguvu wanakijiji wote kwenda kuwamwaga vijiji vya huko karibu na Rwanda, Litumba, Litumbadyosi, Mgazini nk. ikumbukwe hiyo ni kipindi cha Mwinyi wakati operation ya vijiji ilishasahaulika. Akalazimisha hospitali iliyokuwa inahudumia mwambao wa Ziwa Nyasa iwe kijiji cha Rwanda ambao ni pua na mdomo na Hospitali Misheni ya Peramiho na Songea.

Ukawapo uhasama mkubwa na hili lilitokea kipindi cha uongozi wa Ali Hassan Mwinyi, lakini Rais pamoja na kupelekewa malalamiko hayo hakuchukulia hatua na kuacha mambo yalivyo, hivyo uadui kati ya wawili hao ukaongezeka.

Gama na Askofu Komba hawakuombana maji wala kutembeleana kama ilivyokuwa kawaida ingawa Gama alikuwa kipenzi cha viongozi wengine wa dini jimboni Songea.

CCM ilipoadhimishwa kitaifa Songea siku kama 3-4 kabla ya kilele chake Askofu Komba alialikwa kuwa mgeni wa heshima wa siku hiyo Uwanja wa Majimaji ambapo kulikuwa na halaiki nzuri isiyo ya kawaida. Askofu Komba alikubali mwaliko kwa heshima ya Rais Mwinyi aliyekuwepo katika tukio hilo. Hapo ilikuwa nafasi ya kuwakutanisha mahasimu hao wawili na hakuwa na jinsi ilibidi Askofu Komba alipofika jukwani kama geni wa heshima alipaswa kusalimiana na viongozi wote waliokuwapo jukwani kuanzia Rais Mwinyi, Gama na wengineo, na ilikuwa nafasi pekee hao wawili Gama na Askofu Komba kusalimiana kwa mikono kushikana, na kumbe mmoja kati yao alikuwa na afya ya kuungaunga, mapigo ya moyo yakabadilika ghafla.

Askofu aliaga mapema na kuondoka kwenye tukio alasiri hiyo, na alipofika maskani yake kwenye kanisa Kuu la St Mathias Mulumba, mjini songea karibu kabisa na Songea bus Terminal hali ilimzidia. Baada ya saa chache tu majira ya saa mbili jioni siku hiyo hiyo Naibu Askofu Mlelwa alitangaza rasmi kuwa Askofu Mkuu Yakobo (James) Yefunani Komba amemwendea baba wa milele.

Gama tangu wakati huo hakuwa na raha, amekuwa mtu asiye tulia licha nafasi kadhaa alizopata, kwani kabla yakifo chake Askofu Mkuu Yakobo Komba ambaye alijulikana na wengi kuwa na kauli nzito anazotole na zikatekelezeka alisema kamwe Gama hatafanikiwa katika maisha yake ya kisiasa kwa sababu ya usaliti, kisasi na unyama aliwatendea wananchi wa Lituhi mwambao wa ziwa Nyasa wasio na hatia.

Gama hata alipohama Songea, nakumbuka Tabora akawa hata hafiki kusali Kanisa Kuu la Mt Teresya ambapo kiongozi wa wakati huo alikuwa hayati Askofu Mkuu Mario Abdalah Mgulunde, alikuwa anapitiliza kwenda kusali kanisa la Makokola njia iendayo urambo, nilikuwa na kawada mara fulani kusali huko tukawa tunakutana kwa vile tulifahamiana.

Ujio wa Pope hakuwa na jinsi kwa vile Gama kiserikali ndiye aliyekuwa mkaribishaji wa wageni wote kiserikali na kikanisa, nilimwona siku hiyo akijitahidi kusimama muda mrefu pale makao makuu ya Askofu Mkuu Tabora ilipokuwa St Mary's shule aliyofundisha Nyerere enzi hizo, siku za kawaida hakuwa na kawaida ya kusogelea makazi ya maaskofu kutokana na kilichojilia alichomfanyia mwenzao Hayati Komba. Niliwahi kusafiri na Hayati Askofu Mkuu Mgulunde once safari ndefu kidogo aliyekuwa Askofu Mkuu wakati huo pale Tabora tulijadili sana jambo hilo na kuona namna maaskofu walivyokuwa na mtazamo juu ya Gama.

Suala la Gama asitupiwe Nchimbi pekee lawama ni mchanganyiko wa Mengi

  • Nchimbi
  • Askofu Mkuu Yakobo Komba
  • Rais Kikwete ambaye alipishana naye nafasi ya kugombea urais
Hayo kwa vyo vyote yaliweza kumletea fikra nyingi Gama na pengine ndiyo yaliyokatisha haraka maisha yake ingawa alionekana kabla kama mtu mwenye siha nzuri.

CC;
Pasco
 
Sio kuwahonga tu, baada ya kuwahonga aliwafungia ndani hadi kura ya maoni ikamalizika kupigwa...

nakumbuka sana miaka hiyo nilikuwa Songea, sio siri yote aliyokuwa anafanya Mkulu anajua na alikuwa anampa hela afanye yote hayo.
 
Nchimbi, alipewa madaraka akajiona mungu mtu, damu za watanzani zilizomwagika bila hatia zinamlilia, malipo yameishaanza, na bado, Mungu hawezi kuwaacha watu wauaji kama hawa, atakiona cha moto.
 
afanye tambiko kwa kuomba msamaha watanzania wote
 
Baada ya kutemwa uwaziri wa mambo ua ndani mhe. Emmaniel Nchimbi juzi jumamosi alienda kutambikia kwenye kabuli la aliyeliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Gama
Taarifa za watu waliokuwa kwenye msafara wa Nchimbi zinasema alifika makabulini hapo kuomba msamaha kwa marehemi Gama kwani anaona yanayotokea pengine ni kwadababu ua ungomvi wake na Gama..walisema ni kama amechanganyikiwa kwani kutoka kwenye mbio za urais sasa hajiamini hata kuupata udiwani kwani hana ushawi kabisa kwenye jimbo na alikuwa akiliendesha jimbo kwa mtutu wananchi wakigoma analeta polisi wa kutosha leo ni mbunge wa kawaida hana jeuri ya kuagiza polisi atakavyo.

Maoni yangu:
Nchimbi ukimalizana na Gama njoo Arusha uwaombe msamaha watu uliowauwa kanisa la olasti kwa bomu na wale wa soweto..

Taarifa hii mimi sijaielewa kabisa, hasa hayo maneno niliyoyawekea rangi nyekundu.
 
View attachment 137043
Nchimbi alikuwa pete na kidole na Mkulu kwa hoja kwamba Gama alipokuwa katibu mkuu wa CCM alimtifulia Kikwete kuingia Magogoni kwani Gama aliegemea upande wa Cleupa Msuya. Pamoja na kwamba wote Msuya na Kikwete waliangukia pua kwa Nzee Nkapa, hasira za Kikwete hazikuishia hapo licha ya alichosema tutayamaliza kichama.

Emmanuel Nchimbi wakati huo akiwa mmoja wa viongozi waandamizi wa umoja wa vijana CCM alipata mwanya ili kuchanganya vizuri karata huku akiridhiwa na aliyekuwa mhasimu wa Gama kipindi cha kugombea urais. Bahati mbaya ameshindwa kutumia vizuri nafasi yake, ujuavyo nafasi za ujanjaujanja ambazo zimepatikana kwa gharama kubwa hulindwa kwa gharama kubwa pia. Hatimaye mambo yakiharibika mtu mzimamzima huumbuka hadharani. Maana ile ya kukimbia na sanduku la kura za Meya wa Songea alifanikiwa kulizima, hilo limemtokea puani.
ni kweli mkuu, na inasadikika kama Chadema wataweka mgombea ubunge makini wa CHADEMA mwaka 2015 jimbo linaweza kwenda upinzani...
 
Back
Top Bottom