Nchimb na Mwema Wanasubiri nini Ofisini?

Hiki kijamaa sikipendi ni kijeuri afu kinamadhara sana, nchimbi sikupendi sana yani wakisema chagua mtu wa kufa nae atakua nchimbi
 
Ni ngumu sana kwa madaraka ya kupewa kuwajibika! Si waziri na si IGP sadly it is not a proffesional job to seek it eslewhere! wote wamewekwa kwa makusudi maalumu haiwezekani kuwajibika! Wakati ulishafika muda mrefu wa kuacha kulialia na kuchukua maamuzi magumu kwa hao wapuuzi. Tuko nao katika maisha yetu ya kila siku kama hawataki kuwaheshimu raia sasa ni wakati wa raia nao kuwatorture . It is very simple wote warudi kambini otherwise tusilalamike maana uozo tunaulea wenyewe! Akifa mwenye haki mmoja wafe 20 wahujumu haki na demokrasia tutakuwa tumetatua tatizo kwa vinginevyo tutaendelea kulalama wakati jamaa wanatetea majizi kwa nguvu zote na wanashindwa kuelewa kuwa majority yao nao wanamaisha magumu zaidi ya kunguru!
 
Rais Mwinyi alijiuzulu akaja kuwa rais wa nchi hii kwa kuwa alionekana ni mwajibikaji, kama unataka kujenga imani ya watanzania kwako, achia ngazi haraka. Vinginevyo kupata urais labda ulete alshabab waibe kura
Kwa taarifa yako hata ubunge aliupata kwa kuiba kura kule kwao hakubaliki hata cdm waweke jiwe hapati kura
 
Huyu kazi yake ni kukimbizana na mademu (tena vitoto vidogo vya sekondari) Ndio mazwaziri wa JK.
 
Kati ya mawaziri wasiojielewa huyu ni mmoja wapo

Kwa sisi wengine tunaomfahamu toka akiwa mwenyekiti wa UVCCM hatushangai sana kwa madudu yaliyopo sasa wizarani kwake. U dokta wake anajua mwenyewe alikoutoa, Msemakweli alishamaliza kila kitu
 
Nchimbi fuata mfano wa Ali Hassan Mwinyi (wakati huo Waziri wa Mambo ya Ndani) alivyojiuzulu.
 
Aibu yao wenyewe ila wajue hizi DAMU za watanzania zinamwagika bila hatia watazilipa siku moja tena kwa majuto makubwa
 
Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri basi wakati Mh. Emmanuel Nchimbi anagombea nafasi ya kukiwakilisha Chama cha Mapinduzi katika harakati za kugombea kiti cha ubunge kwa mara ya kwanza huko Songea kulikuwa na kashfa ya utekaji nyara na taarifa za matumizi ya silaha aina ya bastola (aidha kutishia au ufyatuaji wa risasi) kwa wafuasi/washabiki wa mpinzani wake (nafikiri alikuwa Dr. Lawrence Gama), inavyoonekana kwa Dr. Nchimbi hii michezo ameizoea, tusingependa kiongozi wa namna hii kwa nchi yetu ya Tanzania, TUNAMTAKA YEYE NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI WAJIUZULU KWA MANUFAA YA UMMA WA TANZANIA.
 
Watanzania tuamke, TUIKATAE CCM, tuwaambie kwamba wanaua ndugu zetu kwa tamaa yao ya madaraka ilhali uwezo wa kuliongoza Taifa letu na kuliletea maendeleo hawana, TUANZE KWA KUISUSIA CCM NA SERIKALI YAKE, TUSIENDE KWENYE MIKUTANO YOYOTE ILE ITAKAYOITISHWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WALA SERIKALI YAKE, TUSIENDE KWENYE MAANDAMANO YOYOTE YATAYOITISHWA NA CCM WALA SERIKALI YAKE, wakishajiona hawatakiwi watashika adabu, watasimama jukwaani wao wenyewe na kuwahutubia watu wawili na kuona aibu na kuondoka, ikifikia hapo ndipo watakapokaa chini na hawana jinsi yoyote iliyobakia isipokuwa ni kuondoka madarakani, lakini wakiwepo WAPUMAVU WACHACHE, narudia tena WAPUMBAVU HATA WACHACHE TU ambao watajitokeza kuwasikiliza hiyo itatosha kabisa kuwafanya CCM wazidi kung'ang'ania madaraka hata kwa gharama ya maisha ya ndugu zetu, HIMA WATANZANIA WASUSIENI HAWA NA MWISHO MUWAADHIBU KWENYE SANDUKU LA KURA KWA KUTOWACHAGUA TENA.
 
Kauli ya nchimbi kwa kusema Mwandishi Daudi Mwangosi ameuwawa kutokana na bomu la machozi ambalo halikulipuliwa kitaalamu, ni kauli angalau inayo kidhi haja. Na hivyo ndivyo inapaswa kwa IGP pia kutamka kwani naamini Nchimbi ametaarifiwa na IGP. Hivyo IGP na RPC Iringa wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kwa kuongea uongo na kuwa wazushi.

Mkuu kweli umeridhika na kauli hiyo ya "kidiplomasia"? Watu waliodhamiria kuua wanalifanya hili kuwa tatizo la bomu "kutolipuliwa kitaalamu"? Ndio maana kuna watu wameamua kuwa sisi watanzania ni mazuzu tunaostahili kupewa porojo zozote katika masuala muhimu na nyeti ya kitaifa. Wote wanatakiwa ama kujiuzulu au kuwajibishwa tangu juzi!
 
Back
Top Bottom