Nchimb na Mwema Wanasubiri nini Ofisini?

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Emmanuel Nchimbi mpaka sasa hujaona sababu ya kujiuzulu? Je unafurahia mauaji haya?

Mbaya zaidi unakuja na matamko yenye utata kuhusu haya mauaji. Hivi ni lini viongozi wa nchi hii mtaacha kuwa wanafiki na msiopenda kuwajibika. Na mbona matukio ya wananchi kuuawa na polisi yameongeza sana baada ya wewe kupewa hii wizara? Kwa nini tusiamini kwamba ulipewa hii wizara kwa kazi ya kuua watanzania? kwa nini tusiamini kwamba wewe ndio unatoa maagizo ya mauaji haya.

Nasikikia una mpango wa kugombea urais 2015, hivi ukipewa madaraka si ndio utachinja watu hadharani. Hii haikubaliki, Nchimbi lazima uondoke!!!!

Kwa chukihii munayo ipandikiza kwa wananchi Musipo wajibika mutaitengeneza Tanzania mbaya yenye visasi.

Igunga mtu alichinjwa mpaka kufa hatujaona lolote linalo endelea.
Viongozi wa siasa wamevamiwa na majambazi na kupigwa sana tena mbele ya polisi katika Campaign hatuoni lolote
Morogoro mtu kapigwa risasa Majibu ni blabla
Na Mwandishi wa Habari ameuwawa kwa bomu na Polisi wanafahamika (Munatupa report kuwa ni kitu kilichotupwa na wananchi)

Tuachane na hayo je wajane na watoto wanao achwa yatima kwa uzembe na chuki za maaskari munao watuma kwenda kuhatarisha maisha ya wananchi, munawajengea mioyo gani? je Tukizalisha kizazi chenye chuki na kisasi kwa polisi tutaishi kwa amani?

Kwakifupi Amani ya nchi hii inaharibiwa na Selikali (WAZIRI NA IGP SAID MWEMA MUWAJIBIKE)
 
Rais Mwinyi alijiuzulu akaja kuwa rais wa nchi hii kwa kuwa alionekana ni mwajibikaji, kama unataka kujenga imani ya watanzania kwako, achia ngazi haraka. Vinginevyo kupata urais labda ulete alshabab waibe kura
 
Haujasikia maelezo yake wanavyopishana na Kamanda wake Kamuhanda?? Yaani sanaa tupu... aibu yao aibu yetu??
 
Emmanuel Nchimbi mpaka sasa hujaona sababu ya kujiuzulu? Je unafurahia mauaji haya?

Mbaya zaidi unakuja na matamko yenye utata kuhusu haya mauaji. Hivi ni lini viongozi wa nchi hii mtaacha kuwa wanafiki na msiopenda kuwajibika. Na mbona matukio ya wananchi kuuawa na polisi yameongeza sana baada ya wewe kupewa hii wizara? Kwa nini tusiamini kwamba ulipewa hii wizara kwa kazi ya kuua watanzania? kwa nini tusiamini kwamba wewe ndio unatoa maagizo ya mauaji haya.

Nasikikia una mpango wa kugombea urais 2015, hivi ukipewa madaraka si ndio utachinja watu hadharani. Hii haikubaliki, Nchimbi lazima uondoke!!!!
Hapo kwenye red,atakuwa anaota
 
Huyu KICHWA KUBWA juzi tukio la moro kauli yake nlifananisha na zile za Teja KITALE..ajiuzulu haraka.
 
Kauli ya nchimbi kwa kusema Mwandishi Daudi Mwangosi ameuwawa kutokana na bomu la machozi ambalo halikulipuliwa kitaalamu, ni kauli angalau inayo kidhi haja. Na hivyo ndivyo inapaswa kwa IGP pia kutamka kwani naamini Nchimbi ametaarifiwa na IGP. Hivyo IGP na RPC Iringa wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kwa kuongea uongo na kuwa wazushi.
 
huo ubunge wenyewe ametumia gharama kubwa sana kuupata dhidi ya Mbogoro wa chadema,halafu aachie uwaziri kiraisiraisi na ukizingatia kila mwanaccm alieko serikalini ana madudu yake.....huyo itakua ngumu sana kuachia nafasi.
 
Kauli ya nchimbi kwa kusema Mwandishi Daudi Mwangosi ameuwawa kutokana na bomu la machozi ambalo halikulipuliwa kitaalamu, ni kauli angalau inayo kidhi haja. Na hivyo ndivyo inapaswa kwa IGP pia kutamka kwani naamini Nchimbi ametaarifiwa na IGP. Hivyo IGP na RPC Iringa wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kwa kuongea uongo na kuwa wazushi.

Hapo nakuunga mkono kwa sana
 
Eti waziri wa Mambo ya Ndani, wakati hata JKT hakupita yaani hajui hata itifaki ya Kijeshi-polisi. Ndo maana anatoa sababu za kijinga kabla hata hajawasiliana na RPC husika. Anafanyakazi kama "remote control". Hii ndo Tanzania bwana, chini ya serikali ya awamu ya 4 na viongozi dizaini ya Nchimbi wapo kibaaaao!!!
 
Asubiri tuandamane kumkurupua oiosini ajiuzuru kwa mauji ya makusudi ya ya raia wema
 
Utamaduni wa kuwajibika pale mambo yanapoharibika kwetu sisi watanzania bado ni nadharia. Waziri Nchimbi pamoja na IGP Mwema walipaswa kujiuzulu nafasi zao haraka, RPC Kamuhanda alipaswa afikishwe mahakamani kwa kosa la mauaji pamoja na askari waliokuwa wakimpiga marehemu Mwangosi.
 
Wenzangu mnaojitambua naomba msaada katika hili:

''waziri wa mambo ya ndani mh. Nchimbi kwa kupitia televisheni amesema kwamba ...Yule mwandishi wa habari wa channel 10 aliuwawa kwa bomu la machozi"

hii ni siasa ua ni nini?????????
 
Emmanuel Nchimbi mpaka sasa hujaona sababu ya kujiuzulu? Je unafurahia mauaji haya?

Mbaya zaidi unakuja na matamko yenye utata kuhusu haya mauaji. Hivi ni lini viongozi wa nchi hii mtaacha kuwa wanafiki na msiopenda kuwajibika. Na mbona matukio ya wananchi kuuawa na polisi yameongeza sana baada ya wewe kupewa hii wizara? Kwa nini tusiamini kwamba ulipewa hii wizara kwa kazi ya kuua watanzania? kwa nini tusiamini kwamba wewe ndio unatoa maagizo ya mauaji haya.

Nasikikia una mpango wa kugombea urais 2015, hivi ukipewa madaraka si ndio utachinja watu hadharani. Hii haikubaliki, Nchimbi lazima uondoke!!!!

Nimekuwa nalifikiria hili suala tangu mauaji ya Morogoro. Ni kwa nini tangu huyu mh. aingie hapo wizarani mauaji yamekuwa mengi? Inawezakana amewekwa hapo kwa dhumuni maalum? Nilimsikia kupitia vyombo vya habari wakati fulani akiwa anaongea kwenye shughuli zake za chama huko Songea kwamba kwa sasa wamewadhibiti wapinzani kwa kiasi kikubwa! Kama kudhibiti kwenyewe ndo huku kwa kuangamiza watu basi maisha ya watanzania yapo hatarini hakika!
 
Kwa chukihii munayo ipandikiza kwa wananchi Musipo wajibika mutaitengeneza Tanzania mbaya yenye visasi.

Igunga mtu alichinjwa mpaka kufa hatujaona lolote linalo endelea.
Viongozi wa siasa wamevamiwa na majambazi na kupigwa sana tena mbele ya polisi katika Campaign hatuoni lolote
Morogoro mtu kapigwa risasa Majibu ni blabla
Na Mwandishi wa Habari ameuwawa kwa bomu na Polisi wanafahamika (Munatupa report kuwa ni kitu kilichotupwa na wananchi)

Tuachane na hayo je wajane na watoto wanao achwa yatima kwa uzembe na chuki za maaskari munao watuma kwenda kuhatarisha maisha ya wananchi, munawajengea mioyo gani? je Tukizalisha kizazi chenye chuki na kisasi kwa polisi tutaishi kwa amani?

Kwakifupi Amani ya nchi hii inaharibiwa na Selikali (WAZIRI NA IGP SAID MWEMA MUWAJIBIKE)
 
tumelalamika vya kutosha...nasubiri miujiza ya mungu maana tumeshindwa(nimeshindwa)kufanya ya libya,misri,tunisia,syria...naona kama tumeshindwa,so sad
 
hakuna atakayejiuzulu hapo...sio utamaduni wa walafi wa madaraka,mwinyi alitakiwa ajiuzulu matokeo yake kabadilishiwa wizara...hajiuzulu mtu,..
 
:A S 465:Kama ingekuwa ni rahisi sana kwa watanzania kureact against aina hii ya unyanyasaji sidhani kama haya yote yangefikia huku.. hawa polisi wamezoea kuuwa wananchi wasiyo na hatia.
Na majambazi wanashirikiana nao
 
Back
Top Bottom