Nakubaliana nawe kuwa waislam wanaofanya ugaidi kwa kuegemea kwenye imani ya kiislam ni wachache sana. Mimi siamini kama wanafika hata hiyo 5%. Lakini hata hao waislam wachache wanaofanya ugaidi kwa mgongo wa uislam, kilicho kibaya sana, ni kuwa huwasikii viongozi wa kiislam wakisimama na kuwakana na kuwatangaza kuwa wanafanya kinyume cha mwongozo wa uislam. Fikiria kama kule Nigeria, vikundi vya waislam vinaenda kushambulia na kuwaua wakristo wakiwa kwenye ibada. Watu ambao hawajawafanyia chochote dhidi ya uislam wao. Lakini humsikii kiongozi hata mmoja wa waislam au mataifa yakiislam yakikemea ushetani huo, au yakiwaelekeza waislam kuwa vitendo hivyo siyo mafunzo ya uislam. Hiyo unataka ilete tafsiri gani?
Vifungu ulivyonukuu kwenye Biblia, siyo msingi wa ukristo. Hicho kifungu kinachoelekeza kuwaua waMaleki, ni wakati wa Agano la kale, ni kipindi cha kabla ya Ukristo. Nikueleweshe kidogo: Wakati wa Agano la kale, Mungu aliwaadhibu wanadamu pale pale wanapokosea. Aliwaadhibu kupitia matukio ya kiasili kama vile mafuriko, moto, matetemeko, au hata kwa njia ya vita. Agano la kale liliagiza 'jino kwa jino, jicho kwa jicho', lakini Agano jipya ambalo ndiyo msingi wa Ukristo, Yesu alisema hivi,"Imeandikwa kwenye Torati, jino kwa jino jicho kwa jicho, lakini mimi nasema samehe hata 7 mara 70. Imeandikwa kwenye Torati, umpende rafiki yako umchukie adui yako, lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu maana kama mkiwapenda marafiki zetu na kuwachukia maadui zetu, mna tofauti gani na wasiomjua Mungu, kwa maana wasiomjua Mungu nao huwapenda marafiki zao na kuwachukia maadui zao". Huo ndio utimilifu wa Torati aliouleta Kristo. Baada ya Kristo, Mungu hawaadhibu watenda dhambi hapo hapo, anawasubiria mpaka siku ya hukumu. Ndio ule mfano wa Kristo unaosema yaache magugu na ngano vikue pamoja mpaka siku ya mavuno, ambapo ngano itawekwa ghalani, magugu yatachomwa moto.
Hiyo nukuu yako nyingine ya kusema Yesu alisema hakuja kuleta amani bali vita, hakumaanisha vita ya kupigana bali alimaanisha ugomvi katika familia, ndiyo maana anasema Baba atagombana na mwanae, mtu na kaka yake au dada yake. Akimaanisha kuwa kutokana na mafundisho yake, wapo wanafamilia watayapokea, wakati wanafamilia wengine watabakia na dini yao ya kale ya kiyahudi, na hivyo kusababisha ugomvi wa kifamilia. Lakini hakuna mahali popote kwenye ukristo ambapo wakristo wameelekezwa kuwaua wasio wakristo auwasioupokea ukristo. Hiyo ni tofauti na uislama ambao kwenye Quran kuna maandiko mengi yanayohamasisha vita na mauaji dhidi ya wasio wakristo. Lakini hiyo haimaanishi kuwa waislam wote ni wauaji. Kinachosaidia ni kuwa wapo miongoni mwa wakufunzi wa uislam wanaojitahidi kutoa tafsiri iliyo tofauti na kuwataka kuwaua wasio waislam wakisema kuwa kifungu hicho ni pale waislam wanaoshambuliwa. Lakini wapo wanaotafsiri kuwa agizo la kuwaua wasio waislam ni la wakati wote, hao ndiyo wanaofanya ugaidi maeneo mbalimbali tunayoyashudia. Na kwa kiasi kikubwa ni waislam wa madhehebu ya Shia.