Nchi za Afrika zasema hapana kwa Marekani moja baada ya nyingine

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212
VCG111104382483.jpg

Hivi majuzi, nchi mbili muhimu za Afrika zimesema hapana kwa Marekani.

Moja ni Kenya. Tarehe 19, Bunge la taifa la Kenya lilipinga shutuma za baraza la seneti nchini Marekani kwamba nchi hiyo "iliiacha Washington na kutafuta manufaa kwa Beijing", na ikaeleza wazi haki yake ya kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine yenyewe binafsi.

Nyingine ni Afrika Kusini. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, aliyezuru Marekani tarehe 21, kwa mara nyingine tena alikanusha madai ya Rais Trump ya "mauaji ya wazungu nchini Afrika Kusini" mbele ya waandishi wa habari katika Ikulu ya White House. Baada ya mkutano wao, serikali ya Afrika Kusini ilisema kwamba nchi hiyo “ilipaza sauti ya Dunia ya Kusini."

Mambo hayo mawili yanaonekana kutokea mtawalia, lakini yana uhusiano wa kimantiki na kuonyesha mwelekeo wa mabadiliko ya utaratibu wa dunia.

Kwa undani, katika ziara yake nchini China mwezi uliopita, Rais William Ruto wa Kenya alikosoa vita vya ushuru vilivyoanzishwa na Marekani, na kutumaini kuwa China na Kenya zitakuwa waundaji pamoja wa utaratibu mpya wa dunia ulio wa haki, jumuishi na endelevu. Alisema: "Tunatakiwa kutetea ushirikiano wa pande nyingi...kitu chenye manufaa kwa Marekani lazima pia kiwe kizuri kwa Kenya."

Marekani ilichukulia kauli hiyo ya Ruto kuwa ni ya "kuasi" na kutishia kutathmini upya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Ni wazi kuwa, Marekani sio tu kwamba hairidhishwi na rais Ruto, bali pia na China. Seneta wa Marekani Jeanne Shaheen hata alisema kwamba Wachina wanakula "chakula" cha Wamarekani. Lo! Wamarekani wanavua uso wao wa uwongo. Kwa Marekani, nchi za Afrika zimekuwa "milo kwenye sahani".

Kwa kiburi na ukosefu wa maadili wa Marekani, sio tu serikali ya Kenya haiwezi kukubali, lakini pia vyombo vya habari vya nchi hiyo pia vilishambulia kwa pamoja. Gazeti la The Standard lilichapisha tahariri ikisema kwamba kabla ya kutathmini upya uhusiano na Kenya, Marekani bora itambue vyema mamlaka ya Kenya na kanuni ya usawa na manufaa kwa wote katika uhusiano wa kimataifa. Tovuti ya Eastleigh Voice ilisema kuwa "Kenya haitaruhusu kuambiwa nani anafaa kuwa rafiki yake."

Kwa Afrika Kusini, shutuma za Trump za "mauaji ya wazungu" yamechukuliwa kuwa ni mchezo wa kisiasa uliodumu kwa nusu mwaka na kufikia kilele chake kwa njia ya "kumvizia" rais Ramaphosa hivi karibuni. Alipozungumza na rais Ramaphosa katika Ikulu ya White House, rais Trump alichukua karatasi aliyoandaa awali ya A4, ambayo ilionyesha miili ikizikwa. Trump alimwambia mwenzake kuwa, "Tazama! Kifo. Kifo cha kutisha." Rais Ramaphosa alikanusha kabisa madai hayo, lakini rais Trump alisisitiza kuwa picha hii ndio ushahidi.

Hata hivyo, siku chache baada ya hapo, shirika la habari la Reuters lilichapisha makala ikisema "Picha aliyoonyesha rais Trump ilipigwa na Reuters, lakini haihusu Afrika Kusini, ni hali iliyotokea baada ya vita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo."

“Huyu ndio Trump – amekithiri vituko na kuwarubuni watu kwa vitisho”

Kwa sababu ya historia ya ubaguzi wa rangi, takwimu zinaonyesha kuwa hadi leo, zaidi ya 80% ya watu milioni 63 wa Afrika Kusini ni watu weusi, lakini wanamiliki 4% tu ya ardhi, na sehemu kubwa ya ardhi iko mikononi mwa wazungu.

Ni wazi kwamba serikali ya Marekani haijali hata kidogo kuhusu usawa wa rangi. Juu ya hili, mkuu wa taasisi ya washauri bingwa ya AMEC mjini Johannesburg, Na’eem Jeenah alisema kwa matamshi makali kuwa: "Huu sio mzozo wa kidiplomasia, bali ni mfano wa matumizi ya nguvu inayojaribu kutumia nchi ya umwamba dhidi ya Dunia ya Kusini.”

Mwishowe, tutaangalia vipi?

Kwanza, iwe ni kuilazimisha Kenya "kuuchagua upande" au kuchafua jina la Afrika Kusini, nia ya kimsingi ya Marekani ni kuonya nchi nyingine ndogo kwa kushambulia nchi kubwa barani Afrika. Hata hivyo, jaribio hili sio tu lilipingwa moja kwa moja na nchi hizi mbili, lakini pia lilianika hadharani wasiwasi wa kimkakati wa Marekani kwa zama hizi: bila shaka inajua kwamba inapoteza uwezo wa kuamua mambo kwa nchi za Afrika.

Pili, kama Rais Ruto alivyosema katika ziara yake nchini China: "Afrika si kete ya mchezo wa chesi, bali ni mchezeshaji kete ya chesi." Kutoka uchumi wa Afrika Kusini kuimarishwa zaidi baada ya kujiunga na BRICS, hadi maisha ya wananchi kuboreshwa moja kwa moja baada ya Reli ya SGR kujengwa... miradi hiyo ina ushawishi mkubwa zaidi kuliko shutuma na vitisho vya Marekani. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Marekani kwanza ghafla "ilikata misaada" kwa nchi nyingi, na kusababisha shughuli za kijamii kuingia matatani katika nchi nyingi za Afrika, na kisha kutoza ushuru kwa dunia nzima, na kuathiri sana uchumi wa nchi za Afrika.

Katika hali hii, hakika itakuwa ni wazimu kwa Marekani kama ikitarajia kuona tabasamu kutoka kwa nchi za Afrika.
 
View attachment 3348389

Press conference ya Ramaphosa/Trump uliiona au umesimuliwa ndugu?

Ukweli mchungu si ni heri ya Zelensky/Trump kuliko hii ya huyu ndugu yetu?
 
Back
Top Bottom