Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 701
Tungepata kundi kubwa la watanganyika wenye msimamo kama wako, wa Rev. Mtikila, wa G-55 na mimi na madai ya wazanzibari ya kupotea kwa mbia mwenza wa muungano basi kazi ingekuwa rahisi kuufahamisha umma wa Tanganyika.
Lakini kila nikifuatilia mijadala humu JF linalohusu kuirejesha Tanganyika ndani ya Muungano basi...list ya "influencial contibutors" kuanzia Mwanakijiji, Nguruvi3, JokaKuu, mkandara ,Miss judith wanasema hawataki hata kuisikia Tanganyika ikitajwa...Kasumba ya Mwalimu ya Tanzania ni nchi moja imewaingia vizuri na wanasahau kuwa Tanganyika na zanzibar zimeunganisha baadhi ya mambo tu. na kila sehemu kubakisha mambo mengi ya kila upande kuyashughulikia yenyewe...sasa vipi utabakisha mambo ya Tanganyika bila ya serikali na taasisi zake?
Wengine wanasema itakuwa ni kuitiA GHARAMA Tanganyika aka Tanzania bara.. hivi kuna kitu ambacho hakina gharama? Hasa kama kina manufaa? Na kama hakina manufaa/faida kwa nini tuwe nacho?, tuendelee kuking'ang'ania? Na hata kuzuia kisijadiliwe au kukosolewa?
Unajua, mimi hujiuliza kama Muungano wetu tungeu-model katika mfumo kama wa EAC basi hizi nchi nyengine zingekuja kujiunga nasi badala ya kuanzisha EAC mpya na kweli Muungano wetu ungekuwa wa kupigiwa mfano duniani. Lakini miaka 47 imepita sasa na hakuna nchi nyengine iliyotamani kuyeyuka ndani ya Muungano kama ambavyo Tanganyika imeyeyuka na kwa Sasa juhudi tunazofanya kuiyeyusha Zanzibar kwa kuelekea serikali moja.
Kuna watu wanapenda kusema Muungano wetu is unique...mimi sioni hii uniqueness isipokuwa naona utapeli tu na mazingaombwe au changa la macho. sijui itatuchukua tena miaka 47 kujua kuwa tunakawilisha na kujiongezea matatizo badala ya kuwa na ujasiri na kukabiliana na uhalisia wa siasa za kimuungano wa nchi huru!!???
Kwa bahati mbaya una uvivu wa kusoma na hata hapa Jf tumeeleza sana sababu ya utanganyika, lakini kama alivyosema mchangiaji mmoja kwamba sijui mna uji vichwani? pitia michango yote hapa jf soma na utajua kwamba watetezi wa utanganyika wanazo sababu, acha kutandia treni kwa mbele bana!Usidharau watu simply kwa kuwa wana mtizamo tofauti na wa kwako! Washabiki wa u-Tanganyika bahati mbaya sana haelezi faida zitakazopatikana mara baada ya kuanzisha Serikali tatu! Je, ufisadi utatoweka? Je, umaskini utaondoka? Je, vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 vitapungua? Kama hakuna majibu, basi sioni haja ya hiyo Serikali ya Tanganika ambayo nahisi itaongeza matatizo badala ya kupunguza!
Kwa maana hiyo Wazanzibar wapo sahihi wanaposema wanatawaliwa na Tanganyika?.Nonda,'
Umesahau kunijumuisha na mimi katika hilo kundi. Tanganyika tayari imo ndani ya Tanzania sasa mnataka Tanganyika tofauti ya nini? Rais wa Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania ni rais wa Tanganyika vile vile, sasa mnataka muwe na marais wawili? Hivi mkishapata rais wa Tanganyika, huyu rais wa Jamhuri ya Mwungano atakuwa na kazi gani? Atakuwa ceremonial tu kama rais wa Israel? Tanganyika imo ndani ya Tanzania, na mara nyingi nikisafiri kutoka Dar kwenda makwetu najisikia nimo ndani ya Tanganyika.
Ni kitu cha ajabu sana kuwa na nchi moja yenye mambo yanayofanana na mithili ya kinyonga.
Mawaziri wa Tanganyika wanaitwa mawaziri wa jamhuri ya muungano, tunawaudhi wazanzibari
Mambo ya Tanganyika (yaani yasio ya muungano) yanapelekwa kwenye bunge la Tanzania, na wabunge wa zanzibar hawatoki nje wakati wa maamuzi.
Baraza la mawaziri linapozungumzia mambo ya Tanganyika, sijui kama mawaziri wasiohusika wanatoka nje.
Jimbo moja zanzibari lina wabunge wawili, Tanganyika mmoja.
Hii ni mifano tu ambayo inalilia Serikali ya Tanganyika, na bunge lake:help:
Ukiniambia nizungunzie mabadiliko ya katiba bila kuzungumzia muungano unanidanganya.
hapo Vipi wana JF:noidea:
Hii ichi inaongozwa na watu wenye akili za kuku ni shida sana kuwaeleza haya wakakuelewa. Mazoea yamewalevya!
Ndugu, nichukue nafasi hi adhimu kuchukua maoni yenu juu ya muungano wetu. Hoja ya kujadili hapa inaitaji tutoe maelezo ya Tanganyika tuitakayo endapo Muungano umevunjika! Swali jingine linakutaka uchangie umuhim wakuwa na Tanganyika!
Kwani wewe ulitokea tanganyika ipi ? Ya pemba unguja,au tanga au mombasa kenya ? Inamana hujui mipaka ya tanganyika#? WACHA KUJITOA FAHAMU ZA AKILI. Tanganyika ipo na mipaka yake,burundi pia ina mipaka yake,na uganda wacha ujinga .Je, unazungumzia Tanganyika ipi, ya Mjerumani iliyojumuisha Rwana na Burundi au ya Mwingereza ambayo haikujumuisha nchi hizo! Ukitaka turudi nyuma turudi pale ambapo wakoloni walikuta tupo, yaani tawala za kichifu na kitemi, right?
Tanganyika ipo ndio hiyo hiyo muitaro tanzania bara,kwani tanzania ni ipi ? ZANZIBAR ina mipaka yake juzi tu ilishawatambulisha mipaka,sasa iliyobaki ndio tanganyika/tanzania.Jamani twaitaji maoni yenu juu ya tanganyika yetu. Je iko wap sehemu ya tanganyika ktk muungano wa tanzania?