Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Nikibahatika kukutana na Mh rais wa JMT nitamtaka ajibu maswali haya bila kumung'unya maneno. UTANGULIZI: Mtoto ni zao la baba na mama.JMT ndiye mtoto mwenyewe na 26/4/2012 anafanya sherehe ya birthday kwa kufika umri wa miaka 48 ya kuzaliwa. MASWALI:- Je! Yupo wapi baba watoto(Tanganyika) ikiwa mama watoto(Zenji) yupo?.Je mzazi huyu alikufa au kafichwa tu?.Kama kafa,je aliugua nini, au uzee?. Je!Kwanini mama watoto(Zenji) hafi?.Mh rais naomba majibu. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania............ NAWASILISHA
 
Mimi kama MtanganyikaHALIS Napenda nipate zaidi response ya wazenj km Katiba Mpya na wengineo.Je Zenji mnaona ufahari sana kututawala kiaina sie tuliodanganyika na huu muungano feki?.
 
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitabiri yote haya! Alisema kitu kama hiki:-

Itafika hatua watu watagawanyika mpaka kwenye ngazi ya familia. Mtaanza kusema sisi ni wazawa wa kwanza na wao wa pili. Sisi wa Baba na wao wa Mama. Tunapoelekea huku tutaanza "Sisi ni JF Premium Member, wao ni Junior Member na hawalipii.Yanayotuunganisha ni makubwa kuliko yanayotutenganisha.

hebu taja bila kusita ni yepi yanatuunganisha? Ni vile vizazi vya watumwa toka Tabora kwenda kuuzwa Z'bar. Kama ni hao vizalia wanaweza kurejea unyanyembe bila taabu tutawapokea. Lakini kwa mujibu wako ni yepi yanatuunganisha?
 
Mimi kama MtanganyikaHALIS Napenda nipate zaidi response ya wazenj km Katiba Mpya na wengineo.Je Zenji mnaona ufahari sana kututawala kiaina sie tuliodanganyika na huu muungano feki?.
Swali lingine ni kwa nini mwaka jana wakati wazanzbari wanajadili muungano na kuamua kuuvunja kwa kutambua Zanzbar kuwa nchi JK alikaa kimya, lakini inapofika muda watanganyika nao wajadili tunawekewa mipaka? Hadi sasa katiba ya Zanzbar inacontradict katiba ya muungano. kazi iliyopo ni kuliweka sawa hilo. Na ili kuliweka sawa hilo options ni mbili tu! kuirejesha serikali ya Tanganyika au kufuta kipengele kinachoitambua Zanzbar kuwa ni nchi ili tubaki na Tanzania moja tu
 
Inaonekana zenj inapendelewa na kubebwa sana
 
tunastahili kuidai tanganyika yetu kwa nguvu zote; wazenji ni watu wasio na fadhila kwa watu bara
 
Mimi naomba Serikali zote mbili kama wanavyosema wanasiasa waitishe KURA ZA MONI kwa watanzania kama muungano uwepo au usiwepo, kuanzia hapo hatutalalamika teeenaaa!!. Happy Muungano
 
tunastahili kuidai tanganyika yetu kwa nguvu zote; wazenji ni watu wasio na fadhila kwa watu bara

Eti wanajiita nchi,sasa inanipa utata iwapo vita ikitokea,je Shein anaweza kuamuru KMKM na JKU kuingia vitani?.Au ndo ule mtindo wa rais wa jmt atawasiliana na rais wa smz kabla ya kuyaamuru majeshi?.Je kwanini asiwepo rais wa Tanganyika ili naye apate haki sawa ya kushauriana na rais wa JMT?.
 
Mimi naomba Serikali zote mbili kama wanavyosema wanasiasa waitishe KURA ZA MONI kwa watanzania kama muungano uwepo au usiwepo, kuanzia hapo hatutalalamika teeenaaa!!. Happy Muungano

Mkuu inaniuma sana kutoiona tanganyika yetu ya 1961-1964.
 
Nasikia mara ohhhh, wabara wanatuonea, wabara wanatudharau. Sisi si wabara, ni watanganyika bana!

Muungwana haachi asili. Nia yangu si kuanzisha thread ya kupinga muungano, bali sipendi kuitwa mbara na ndio maana ninasema sisi sio wabara, ni watanganyika. Ukisema Tanganyika ni jina la kikoloni, basi kataa pia majina ya Tabora, Mwanza, Dar es salaam, Tanga na mengine mengi yanayopatikana katika ramani iliyochorwa na mkoloni.

well said Crucifix
 
Jamani naomba na nyie wadau mchangie hili,hivi kwanini wazanzibari wakisema wanataka serikali yao iliyo kamil hawatishwi na watu wananyamaza lakini huku tanganyika mtu akisema hilo inakua nongwa
ninavyoelewa hata sisi bara tunahitaji ile serikali yetu ya tanganyika mbona tumemezwa?mbona kule kuna serikali vipi hii tanganyika yetu?
 
Ni kweli mkuu kama hawatakubali kurekebisha mfumo wa muungano yaani wa serikali tatu, afadhali tubaki na tanganyika yetu. Na si kuwasikiliza kila kitu hao wazanzibar!
 
mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui

nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu

kwa hiyo;

mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu

maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua

nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?
So captivated in fantasy!
 
Kipindi nipo sekondari nilikua namshangaa mbunge wa makete kipindi hicho Tuntemeke sanga(R.I.P)alivyokua anakwaruzana na mwalimu Nyerere akidai Tanganyika,Sipingi muungano ila nakereka na baadhi ya mambo yalivyofichwa na kuufanya muungano uonekane wa kihuni,kwa mujibu wa waasisi wa muungano wanadai muungano ni wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar ndo ikapatikana Tanzania, zanzibar bado nchi ndani ya muungano kizungumkuti kipo kwenye kuitambua Tanganyika kama ni nchi hai au mfu maana iliyopo sasa ni Tanzania na zanzibar.

Mifano Hai
- Uingereza ni muungano wa nchi 3 ambazo ni Wales,United kingdom na Scotland na bado zipo

Wanaofaham vizuri kuhusu huu muungano hebu mnijuze Tanganyika yetu iko wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom