Nchi wanachama wa UN waishauri Tanzania kuondoa sheria kandamizi na tozo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Nchi wanachaama wa Umoja wa Mataifa (UN) zimeishauri Tanzania kubadili sheria kandamizi ikiwemo Sheria ya Ndoa ambapo wametaka umri wa mtu kuingia kwenye ndoa uanzie miaka 18 kama ilivyo mataifa mengine.

Kuondoa adhabu ya kifo na kuwa na adhabu mbadala, pia kuruhusu Haki ya Kusanyika ili kukuza demokrasia. Kuondoa vipengele kandamizi kwenye Sheria ya Habari ya 2016, Sheria ya Makosa ya Mtandao 2016.

Ushauri huu umetolewa na nchi wanachama katika Mkutano wa UPR ambao hufanyika baada ya wadau wa Haki za Binadamu kutuma mapendekezo wanayotaka kuyaona katika sheria za nchi yao.

IKumbukwe wadau na wanaharakati hupewa muda wa kutuma mapendekezo ya mambo wanayotaka yarekebishwe nchini kwao na kuyatuma UN, mapendekezo huweza kutumwa kama mtu mmoja mmoja au kikundi ambapo kwa Tanzania, LHRC huwa inaratibu mashirika mbalimbali kuweka mapendekezo pamoja kuyatuma UN.

Baada ya mapendekezo hayo kutumwa na kusomwa ndipo nchi wanachama huzungumza kuhusu sheria hizo ambapo kikao kinaendelea na kwa sasa Tanzania ipo kikaangoni kushauriwa vitu vya kuviacha.​
 
tumeanza na kuondoa machinga ili wageni wakija wasiwe wanaogopa, hili nalo tutaliangalia
 
Back
Top Bottom