Nchi nyingi za Afrika zasema hapana dhidi ya Marekani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111360857907.jpg

Tukiuliza kama kuna nchi yoyote ambayo inajaribu kutawala dunia, watu wengi watajibu ni Marekani. Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imedai "kurudi tena Afrika", lakini kwa lengo halisi la kudumisha nguvu zake za kijeshi, kiuchumi na kiteknolojia. Juu ya hilo, nchi za Afrika zinajua vya kutosha.

Mgogoro kati ya Russia na Ukraine uliochochewa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi umeleta matatizo makubwa ya nishati na chakula barani Afrika, lakini badala ya kuangalia changamoto zinazozikabili nchi za Afrika, Marekani inazilazimisha kuchagua upande, na hata baraza la wawakilishi la nchi hiyo lilipitisha sheria ya kutambua mawasiliano kati ya nchi za Afrika na Russia ni "kula njama" na kukabiliwa na vikwazo. Ni kawaida kwa nchi za Afrika kuwa na mitazamo tofauti kuhusu mgogoro huu kwa kuangalia maslahi yao tofauti. Akizungumzia shinikizo hilo kutoka Marekani, waziri wa uhusiano wa kimataifa na ushirikiano wa Afrika Kusini Bibi Naledi Pandol alimwambia mwenzake wa Marekani Antony Blinken moja kwa moja kuwa, "Sisi ni nchi huru. Hakuna jambo ambalo ninalichukia zaidi, kama kuniambia nini nchi yangu inapaswa kufanya."

"Dola ni fedha yetu, lakini ni shida yako." Maneno ya kiburi ya aliyekuwa waziri wa fedha wa Marekani John Connally yamethibitishwa kwa miongo kadhaa. Kudumisha nguvu ya dola ndio kulinda nguvu ya Marekani. Mwezi Machi mwaka 2011, Marekani na washirika wake walifanya mashambulizi ya anga dhidi ya jeshi la serikali ya Libya, na kuupindua utawala wa Gaddafi. Mbali na mambo ya siasa za kijiografia, pendekezo la hapo awali la Gaddafi la kutotumia dola ya Marekani kwenye biashara pia linachukuliwa kuwa moja ya sababu za kushambuliwa kwa Libya.

Mbali na mfano huo mkubwa, ni kawaida kwa Marekani kuhamishia nje msukosuko wake wa ndani ya nchi na kuharibu utulivu wa kiuchumi na kifedha wa nchi nyingine. Mwaka jana, Marekani ilipandisha viwango vya riba mara saba ili kutatua tatizo la mfumuko wake mkubwa wa bei, lakini hasara zinakula sehemu nyingine duniani. Takwimu zimeonesha kuwa mwaka 2022 wastani wa mfumuko wa bei barani Afrika ulifikia 13.5%, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi katika muongo mmoja, ambapo Zimbabwe ilishuhudia kiwango cha mfumuko wa bei wa asilimia 256.9% kutokana na vikwazo vya Marekani na nchi nyingine za Magharibi vinavyoshusha thamani ya sarafu yake. Sasa, wanasiasa na wachumi zaidi na zaidi barani Afrika wanazungumzia juu ya kupunguza utegemezi kwa dola. Mwaka jana, mfumo wa malipo wa Afrika PAPSS ulizinduliwa rasmi mjini Accra, Ghana. Hii ina maana kwamba nchi za Afrika zinazoteswa na umwamba wa dola zimeanza rasmi "kuondoa dola".

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imetumia visingizio mbalimbali kushawishi na hata kutishia nchi za Afrika kutoshirikiana na makampuni ya teknolojia ya China. Lakini maneno haya ni kama “kumpigia mbuzi gitaa”. Kwa muda mrefu, kutokana na ukosefu wa teknolojia na vipaji, data muhimu za nchi nyingi za Afrika zimehifadhiwa nchini Marekani na Ulaya, jambo ambalo bila shaka linaleta hatari kubwa ya kiusalama. Baadhi ya nchi, zikiungwa mkono na kampuni ya China ya Huawei, zimejenga zenyewe vituo vyao vya data, jambo ambalo limechukiza Marekani. Ushahidi mwingi umeonyesha kwamba Marekani inatumia nguvu yake ya kiteknolojia kudukua taarifa za siri za nchi nyingine, hata za viongozi wa nchi washirika wake. Lakini bila shaka, madhumuni mengine ya Marekani kukandamiza makampuni ya teknolojia ya China ni kuhofia kwamba nafasi yake kama nguvu nambari moja ya teknolojia duniani itachukuliwa.

Hata hivyo, nchi za Afrika bado zinafanya uwekezaji mwingi katika vifaa na miundombinu ya China. Mwaka jana, makampuni mawili ya simu ya Afrika yalizindua mitandao ya 5G inayojengwa na Huawei nchini Afrika Kusini na Kenya. Mwezi uliopita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Stergomena Tax alisema bila kuficha kwamba Tanzania inaikaribisha Huawei na imethamini mchango unaotolewa na kampuni hiyo kwa sekta ya TEHAMA nchini humo.

Maafa yanayosababishwa na vitendo vya umwamba vya Marekani kwa dunia nzima ni mengi yasiyoweza kuhesabika, lakini nchi nyingi zaidi za Afrika zinatekeleza ipasavyo "uhuru wa kujitawala" na kusema hapana dhidi ya vitendo hivyo. Kuna msemo wa kale wa Kichina usemao “Wale wanaokosa maadili watajitenga wenyewe.” Huenda hii ndiyo hali halisi ya Marekani ya leo.
 
View attachment 2533373

"Mgogoro kati ya Russia na Ukraine uliochochewa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi ..."

Hicho ni kichekesho cha karne na atakayekuelewa nacho ni mrusi wa Buza pekee.
 
Kinachoudhi zaidi ni ubinafsi wa kutowajali Viumbe wenzao wengi wamekufa Africa kwa corona, njaa stress za Ndoa na mahusiano, na kukata tamaa ya kuishi.

Yenyewe hayajali. Mimi naona wamevuka mstari. Ni heri ukraine iwe sehemu kamili ya urusi kuliko hujuma zinazoendelea na maafa uanayotokea duniani.

Na urusi kila siku anasema vikwazo vinaathiri nchi masikini sio yeye. Na ndio lengo la hao. Kimbe unaweza kugombana na mkubwa mwenzio ili kumkomoa yule mdogo ama mnyonge.
 
Wewe kwa nini uwe mnyonge wakati una miguu, mikono, kichwa na masikio? Dume zima unalialia kuwa wewe mnyonge? Pumbav
 
HUYU MTOA MADA NI KIBARAKA WA WACHINA, WACHINA NI WASHENZI ZAIDI YA WAMAREKANI. NDIO MAANA HATA WACHINA WENYEWE WANATAMANI KWENDA KUISHI NA KUFANYA KAZ MAREKANI NA ULAYA
 
"Mgogoro kati ya Russia na Ukraine uliochochewa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi ..."

Hicho ni kichekesho cha karne na atakayekuelewa nacho ni mrusi wa Buza pekee.
Huyu ni "chawa" mkubwa wa Mchina. Nafikiri analipwa kwa post kama hizi.
 
Hana uchungu na maisha ya watu yanayopotea bure.

Nini ambacho Ukraine kafanya kuhalalisha bouncer lile kumpelekea vita? Ukraine Kwa Russia ni kama katoto kadogo tu.

Kwa uhalali upi bouncer lile kukishambulia kitoto kidogo kwa mapanga na mikuki?

Halafu jamaa liko Buza linakenua.
 
"Mgogoro kati ya Russia na Ukraine uliochochewa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi ..."

Hicho ni kichekesho cha karne na atakayekuelewa nacho ni mrusi wa Buza pekee.
Aise kumbe na wewe hujui cho chote kuhusiana na Mgogoro wa Russia na Ukraine.
Fuatilia Containment Policy ya US kuhusu Russia utaelewa vizuri.
 
Back
Top Bottom