PostGE2025 Nchi na kilio cha maji

PostGE2025 Nchi na kilio cha maji

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

iamwangdamin

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,176
Reaction score
2,053
Leo tunakumbushana jambo moja tu, hatuwezi kubadili tabia nchi bila kubadili tabia zetu. Ni jukumu letu kulinda mazingira, kutunza vyanzo vya maji, na kuheshimu ardhi inayotupa riziki. Tukifanya hivyo, tunalinda maisha yetu na vizazi vinavyokuja.

Tuchukue hatua kwa umoja na hekima. Dunia ni moja, na mustakabali wake upo mikononi mwetu. Mungu atubariki na atuongoze katika kulinda uhai wa mazingira yetu.

Tatizo la maji na mabadiliko ya tabia nchi si la taifa moja ni changamoto ya dunia nzima. Afrika, bara letu lenye neema, linaona wazi athari za mabadiliko haya , ukame unaoongezeka, mvua zisizotabirika, na vyanzo vya maji vinavyokauka. Tanzania pia inaguswa, mito inapungua, misitu inapotea, na maisha ya wananchi yanabadilika. #tanzania #mazingira #youth #africa
on saturday i got a little accident , lost my stuffs. so am kindly offline _20251211_121721_0000.png
 
Tuna viongozi vilaza na wala tusisingizie tabia ya nchi wala mazingira.

UAE ni jangwa ,mvua hakuna ,joto kama lote ,wakichimba chini wanakutana na mafuta lakini hawana shida ya maji hata kidogo.

Sisi tumezungukwa na mito,maziwa na vyanzo tele vya maji ,tuna misimu minne ya mvua ya kutoasha ,ukichimba chini mita kadhaa unakutana na dhoruba ya maji yet DAR NZIMA HAKUNA MAJI.

Halafu kutwa kumsifia Aweso Aweso NON SENSE ni KIAZI tu.
 
Je hatuwezi kuyachakata maji bahari yakafaa kutumika katika matumizi ya kawaida.?
 
Je hatuwezi kuyachakata maji bahari yakafaa kutumika katika matumizi ya kawaida.?
Huko ni mbali sana mkuu ,hiyo ni kwa watu ambao hawana other sources zaidi ya BAHARI ambapo ni UAE wao wamefanya hivyo...Sisi ukichimba chini tu unakutana na maji ya kutosha achilia mbali maziwa makubwa yanayotuzunguka.

tatizo letu kuu ni tumeweka MAJIZI aka MAPIGAJI kwenye sehemu nyeti ,wanawaza KUPIGA tu kwenye hiyo miradi.
 
Basi ipo shida mahala maana
Tungeanzia hapo kwanza mji mdogo wa DSM na kibaha kukosa maji ya safi na salama sio sahihi.

DSM ilibidi sio wawe na Maji safi na salama Ila walibidi kupewa special treatment kwakuwa uchumi wa nchi unatoka DSM .
 
Tuna viongozi vilaza na wala tusisingizie tabia ya nchi wala mazingira.

UAE ni jangwa ,mvua hakuna ,joto kama lote ,wakichimba chini wanakutana na mafuta lakini hawana shida ya maji hata kidogo.

Sisi tumezungukwa na mito,maziwa na vyanzo tele vya maji ,tuna misimu minne ya mvua ya kutoasha ,ukichimba chini mita kadhaa unakutana na dhoruba ya maji yet DAR NZIMA HAKUNA MAJI.

Halafu kutwa kumsifia Aweso Aweso NON SENSE ni KIAZI tu.
Ushasema wenzetu wana black gold. Ile pesa inafaa kufanya lolote . Bajeti yetu ndogo, taifa letu changa ndugu . InshaAllah tutafika.
 
Waandishi kama nyinyi ndiyo manaolididimiza TAIFA kwa kutotumia kalamu yenu vizuri! Hivi TZ kweli tunachangamoto mpaka tukose maji? Really? Like Serioslly? Au unataka UTEUZI? Waambie ukweli acha UPOTOSHAJI.
Sitaki uteuzi , nimeongea facts za dunia nzima , ujue kwa sasa dunia nzima inalia kuhusu mazingira na athari zake . Au huoni hata muelekeo wa kusema sote tutumie clean or renewable energy , my brother dunia ya sasa mambo yamebadilika pakubwa sana.
 
Dar kukosa Maji ni sawa na baba mwenye NYUMBA ununue Kuku jogoo aliyekomaa na wakati wa kula wakupe miguu ya jogoo

Ikiwa DSM inashikilia uchumi wa nchi kwa 80% je hatuwezi kuona Aibu kuwakosesha Maji

We don't need to find excuse on this
 
Je hatuwezi kuyachakata maji bahari yakafaa kutumika katika matumizi ya kawaida.?
Bahari ni kubwa , maji ni mengi , energy inayohitajika kuchakati kwenda maji safi kwa matumizi ya binadamu ni kubwa , nuclear energy ndio favorable i guess , ni mataifa machache yanatumia hii njia ila inafaa . Gharama ni kubwa
 
Ushasema wenzetu wana black gold. Ile pesa inafaa kufanya lolote . Bajeti yetu ndogo, taifa letu changa ndugu . InshaAllah tutafika.

Pesa gani unayozungumzia? Kuchimba kisima kila kata na kujenga tank kubwa la kuhifadhia maji kipindi cha dharura kinahitaji black gold? Kama tumeweza kujenga Sekondari kila kata tutashindwa kuchimba visima?

Tatizo tumeweka MAJINZI sehemu nyeti na wanachofanya ni KUJIPIGIA PESA tu kwenye miradi.
 
Magari ya kubeba propaganda za kufukia uzembe na kutokuwajibika kwa watawala.
 
Bahari ni kubwa , maji ni mengi , energy inayohitajika kuchakati kwenda maji safi kwa matumizi ya binadamu ni kubwa , nuclear energy ndio favorable i guess , ni mataifa machache yanatumia hii njia ila inafaa . Gharama ni kubwa

Gharama kubwa inafika sh ngapi ?

Tatizo letu unahisi ni PESA au maono?
 
Mnatupigia kelele tu hapa.

Tatizo linaeleweka ni kwamba vyanzo vya maji vumeharibiwa kwa kuchepushwa kwa maji, watu wamekata na wanaendelea kukata miti kwenye misitu ya asili wanatengeneza mikaa bila kukemewa na kuchukuliwa hatua.
 
Miaka 70 ya uhuru bado tunapambana na maji, hatujamtua mama ndoo kichwani... ilhali tumezungukwa na kila kitu iko haja ya kupata katiba mpya, inayorudisha madaraka kwa raia waweze kuweka serikali wanayotaka na kuitoa isipojielewa.
 
Mnatupigia kelele tu hapa.

Tatizo linaeleweka ni kwamba vyanzo vya maji vumeharibiwa kwa kuchepushwa kwa maji, watu wamekata na wanaendelea kukata miti kwenye misitu ya asili wanatengeneza mikaa bila kukemewa na kuchukuliwa hatua.
Asante kwa kufikiri kwa kina , swala la mazingira ni pana sana. Watu wengi wanaliona kama ni dogo ila mazingira ndio kila kitu. Mazingira yanayotuzunguka kuanzia miti, vyanzo vya maji , mabonde , milima , vyombo vya moto tunavyotumia , taka tunazotumia , wanyama tunaowala na kilimo vyote hivi vinaathiri maisha yetu . Joto limezidi duniani kote , barafu zinayeyuka sehemu mbali mbali za dunia . Visiwa na majiji vinamezwa kwa uongezekaji wa maji bahari. Mengi yapo , swala ni utunzaji wq mazingira , sote tunapaswa kuwajibika.
 
Back
Top Bottom