Nchi kwanza chama baadae na kinachoendelea Arusha

Nchi kwanza chama baadae na kinachoendelea Arusha

......SIO VIBAYA KWAKUWA UCHUNGUZI UNAONYESHA WANAOITWA NAPE NI WALE WASIONITUKANA, HII NI SIFA NJEMA, KEEP ON DOING IT GUYS
Hawa si umewatuma, na wanafanya kazi inayokuridhisha lazima uwasifu.
 
nape
usitafute cheap popularity kwenye mambo ya msingi yanayohusu nchi, ccm imekuwa kama genge la watu wachache ambao wako kwa maslahi yao ndio maana inapofikia suala la kweli wanapiga kelele za kila aina na pia puhakikisha kuwa ukweli unapotoshwa ili tu kulinda maslahi ya genge. Ingekuwa ccm iko kwa maslahi ya taifa ni mambo mangapi ya msingi wanapotezea?


1. Bajeti ya kisanii
2.bei ya mafuta yanapanda kila siku
3.madai kuwa uchumi unakuwa huku hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu(usanii tu)
4.kutenga zaidi ya asilimia kumi ya bajeti kwa kulipana posho tu( hii ni hujuma) je serikali ya nyerere iliwahi kufanya hivi?
5.kupandisha kodi za magari kinyemela na kuwapa mzigo watanzania ili tu mlipane posho kubwa kwa kodi zao.
6.richmond to dowans ,dowans to symbion!


na mengine mengi.


kuna maslahi ya nchi hapo? Majimbo mangapi ya uchaguzi mlichakachua bila kujali matakwa ya wananchi! Utaifa gani huo? Si maslahi ya ccm na watu wachache hayo?
Maslahi ya nchi yaendane na matakwa ya wananchi na si matakwa ya ccm.
Cdm wameona kuwa wananchi wanadharauliwa, hawana mtetezi wakiwahurumia wananchi nyie mnasema wachochezi! Kwa kuwa kwenu mwananchi hana thamani!
Mpaka lini? Nape tumia ubongo wako vizuri funua macho yako uone ukweli na si ushabiki wa chama.
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE
Umesema wananchi kwanza chama baadae.Wananchi wapi unaowazungumzia kwa unafiki kuwa Leo unawaonea huruma!!!?Wewe umekuwa msemaji wa Chadema siku hizi!!!?Kama ni wananchi kwanza vipi kwa polisi waliowaua raia kama kuku Arusha,Nyamongo,Mbea na kwingineko kote!!!!????Acha unafiki kwenda kule mnyonyaji mkubwa wewe
 
Ndugu Nape,

Kiongozi makini hana hofu na matusi bali hujifunza kutokana na hayo matusi, ukiona watukanwa ujue wanakutukana wamechoshwa na uongo wenu, ona ukweli kwamba huna hoja na nchi imesha washinda sasa, mambo ya Chadema Arusha ni madogo sana na Chadema wanayashugulikia vizuri mpaka sasa, kuna mambo ya msingi ambayo tunategemea nyie myashugulikie badala yake mnakaa kulilia tu kama watoto.

Shughulikia Ufisadi hilo ndilo tatizo la msingi katika chama chako.
 
NAPE , tazama watoto wa Kitanzania wamavyohangaika kutafuta elimu, CHADEMA SI TATIZO KATIKA NCHI HII, tuambia je nini chanzo cha uduni huu, ni taifa kukosa viongozi makini na mahiri ama ni ccm kuzeeka vibaya
29197_400623731810_667886810_4633324_7620348_n.jpg
 
......SIO VIBAYA KWAKUWA UCHUNGUZI UNAONYESHA WANAOITWA NAPE NI WALE WASIONITUKANA, HII NI SIFA NJEMA, KEEP ON DOING IT GUYS

Using multiple IDs for self publicity is shameful! Bora hata ungezitumia ku-publicize MAGAMBA yenu. Aibu!
 
Ivi ni lini ccm imesimamia wananchi?
Mmetuletea maendeleo yapi wakati mnaendelea kutuibia kila siku?
 
Nani kakuambia kupindisha sheria na kanuni na kugawana vyeo ni msingi wa kuweka nchi mbele?hiyo ni tafsiri yenu CCM
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE


Acha pumba hizo. Mngelijua hilo mngemshauri JK aachie Ngazi kwa manufaa ya Taifa kwanza, kwasababu kwanza hakuchaguliwa na wananchi; pili bado nchi imemeshinda. Kazi yake ni kusafiri safiri tu na kubembea nje na wakati ndani yake mambo yanaenda vibaya..... Umeme hakuna na hakuna ndoto ya kupatikana hata miaka 10 ijayo kwani hakuna mipango na hata iliyopo haiendani na ukuwaji wa mahitaji....pato la Taifa linapungua huku matumizi yakiongezeka hii inatokana na misamaha isiyo na Tija na kutokuwa na mikakati ya makusudi ya kuibadili TZ toka kwenye nchi ya consumer country to producer country.....huduma duni za Afya, Elimu, Makazi, Miji isiyopangwa Na mengi mengineyo.......
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?
Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE

Mheshimiwa Nape kauli yako inatia mashaka kuhusu uadilifu wako. Uadilifu ni kitu consistent na unapoona mtu anakwenda back and forth hofu ya kutomwamini inazidi. Unapotoa kauli kuna wakati zinakurudi bila kudhamiria.

Nchi kwanza chama baadaye nikauli ya dhihaka. Suala la Arusha ni dogo sana kama tunataka kuitanguliza nchi kwanza.
CCM wangefuata tarataibu bila ubabe wakakubali kukaa meza ya majadiliano, vifo na majeruhi visingetokea. Kama mkurugenzi wa uchaguzi Arusha angetenda haki bila kushawishiwa na serikali ya chama chako ingekuwa nchi ikwanza.
Hata pale alipotokea Kada mwenzako Lowasaa na kusema utafutwe muafaka, chama chako kilimzogoa! nchi kwanza wewe unaipata kutoka wapi.

Nchi kwanza haianzii uchaguzi wa Arusha. Njia hii ya mkato wa kutaka umaarufu inadidimiza na kuwadhalilisha vijana waliotegemea kuwa ungekuwa na mchango tofauti na wenye mwelekeo wa nchi kwanza. Inaonekana tayari kilevi cha madaraka kimeashakuingia katika damu, ulevi ambao ni mbaya kuliko wa pombe kwani unaondoa heshima na utu wa mtu.

Mikataba ya madini, IPTL,Richmond, Dowans, Kagoda, meremeta, Tangold, Kiwira, Deep green, BAE,ujenzi BoT, pesa za kunusuru uchumi ni mambo yanayoliumiza taifa hili sana. Kashfa hzio peke yake zinaweza kutoa bajeti ya nchi.
Mwenyekiti wako, Waziri mkuu wako, Spika wako, Mwanasheria wa serikali yako, Katibu mkuu wa chama chako, wewe mwenyewe, Wabunge wa chama chako, Mkurugenzi wa PCCB wa seriklai yako wote mumeungana pamoja katika kuficha na kuwatetea waovu wanaolimaliza taifa kiuchumi na kimaadili bila haya wala soni. Mnakaa vikao vya kutafuta maeno ya kutughilibu kama vile, uchunguzi bado, kutoingilia madaraka, haki itendeke, tunafanyia kazi ili mradi tu muwakingie kifua wahalifu kudharau watu milioni 40.

Nape unafahamu fika pesa za kodi za masikini anayeishi kwa mlo mmoja ambaye mtoto wake haendi shule na asiye na mategemeo ya baadaye zinatafunwa na ninyi ndani ya serikali kwa kibali cha CC/NEC ambayo wewe ni mshiriki. Yote haya yanafanyika mchana na ukiyaona kwa macho yako mwenyewe, LEO UNAPATA WAPI USHUJAA WA KUSEMA NCHI KWANZA, endapo wewe na kundi lako mumeshindwa kuiweka nchi kwanza?

Nape unafahamu kuwa hujuma ndizo zinalipeleka taifa kwenye giza tororo! unajua dhuluma ya kupokea posho kwa kulala bungeni, unajua kuwa mashangingi yanaitafuna serikali bila huruma, leo unasema nchi kwanza! white elephant!

Wezi wa kuku wanafikishwa mahakamani na wengi tayari wapo keko, wezi waliokubuhu wa mali za umma mnawaita 'wanaochafua chama', badala ya kuwafikisha mhakamani mnaenda Dodoma katika mahakama ya kujivua gamba. Ghiliba hii umekuwa unapita nchi nzima ukiihubiri kana kwamba ukiiba na kuachia madaraka ndiyo nchi Kwanza!! Nape Nape, tafadhali usituchefue, tuna hasira ya kupigika kimaisha kutokana na uzembe uliokubuhu ndani ya chama na serikali amabayo wewe ni mshiriki muhimu, unapokuja na kauli za mzaha kama hizi unatudhalilisha na kututia hasira zaidi.

Kuliko kutafakari uchaguzi wa Arusha, nakuomba utafakari yafuatayo.
Hakuna aliyejua kaburu ataachia South Africa aliyoikalia miaka 500.
Hakuna aliyejua kuwa Idd Amin, Mobutu, Bokasa watafariki katika dhalili kubwa kiasi kile.
Hakuna aliyejua ukuta wa Berlin utavunjwa siku moja.
Hakuna aliyejua dola kubwa ya Urusi itaparaganyika na hakuna aliyejua kuwa Mubarak na Ben ALi wataondoka kwa dhalili.

Tuachie sisi tufikirie nchi kwanza, wewe enenda kwenye vikao vyenu mkapange mikakati ya kutetea wahalifu kwa njia ya gamba. Sisi tutatetea nchi yetu na hakika ni nchi yetu.
 
Kuliko kutafakari uchaguzi wa Arusha, nakuomba utafakari yafuatayo. Hakuna aliyejua kaburu ataachia South Africa aliyoikalia miaka 500. Hakuna aliyejua kuwa Idd Amin, Mobutu, Bokasa watafariki katika dhalili kubwa kiasi kile. Hakuna aliyejua ukuta wa Berlin utavunjwa siku moja. Hakuna aliyejua dola kubwa ya Urusi itaparaganyika na hakuna aliyejua kuwa Mubarak na Ben ALi wataondoka kwa dhalili. Tuachie sisi tufikirie nchi kwanza, wewe enenda kwenye vikao vyenu mkapange mikakati ya kutetea wahalifu kwa njia ya gamba. Sisi tutatetea nchi yetu na hakika ni nchi yetu.Haya yanatosha! Na hitimisho ni kwamba hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, na mbio za sakafuni huishia ukingoni...bila shaka kuna hatua chache sana kufikia ukingo huo."Adhabu na mwisho wa Uovu ni aibu"
 
HIVI mnataka NIJIBU NINI? MATUSI MNAYONITUKANA MIE MPUMBAVU? USHAURI WA BURE KWENU NYOTE MNAOISHIA KUTUKANA,KUKEJELI BADALA YA KUKEJELI NA KUTUKANA MKICHOKA ACHENI KUCHANGIA THREAD ZANGU, HAKUNA MTU ANALAZIMISHWA KUCHANGIA NDO MAANA WAKATI MWINGINE NAWAANGALIA TU MNAVYOTUKANA.

WAPO AMBAO KWELI WANA HOJA NA MIE NAWAHESHIMU SANA, LAKINI WA KUTUKANA NA KUKEJELI PAMOJA NA KWAMBA NAJUA HAWAZIDI WAWILI NA IDs KIBAO WACHA WAENDELEE KUTUKANA NA SIONI SHIDA NITAKAA NA KUSOMA MATUSI YENU.

KARIBU KILA MTU HAPA ATAITWA NAPE......SIO VIBAYA KWAKUWA UCHUNGUZI UNAONYESHA WANAOITWA NAPE NI WALE WASIONITUKANA, HII NI SIFA NJEMA, KEEP ON DOING IT GUYS

Nape, nchi iko vitani, wananchi wapo vitani. Maisha ya watanzania wa leo hayaeleweki. Kila kona ni ufisadi na kila siku ni kituko kipya kutoka kwa watawala. hakuna anayeonyesha hata ile chembe ya nia ya kujua matatizo yetu wacha kuyatatua, na wale vijana ambao wengi walidhania wana uelewa wa matatizo ya kizazi cha sasa kuliko wazee wetu mambo yanakuwa magumu kuliko jana. Wanakuwa mavuvuzela badala ya kutatua.

Ni kweli hata mimi sipendi utukanwe, ila nakuomba na wewe uwe makini kwenye mambo makini. Kama kweli umekaa darasani tena karne hii ya 21 ni wazi huwezi kupenda mambo ya ulaghai na uhuni, kama unavyochukia kutukanwa hapa. Je unajua swala la Arusha ni matusi ya vitendo ambapo wewe unaliona ni jema? Kuna matusi ya aina nyingi, maneno, kuandika, ishara, vitendo nk. Wewe umeanzisha topic ya matusi kwa kizazi cha sasa. Kupora demokrasia na kupora muafaka-vyote ni matusi ya nguoni.

Kuanzia kaskazini mwa afrika mpaka kusini, mashariki mpaka magharibi mwa afrika watu wanakufa kwa kulilia na kugombania demokrasia ya kweli. haki ya kuchaguliwa, kulindwa, na heshima, pamoja na usawa mbele ya sheria. Mgawo sawa wa keki ya Taifa. CCM wametumia hila, wizi, ulaghai, wamepindisha sheria za uchaguzi Arusha. Watu wamechukia wameamua kupigania haki kwa kutoa uhai wao. CCM hao hao wanakuja na kununua watu watatu wakidai muafaka umefikiwa. Kweli wewe unaoona hapo kuna wananchi kwanza?????

Nape kumbuka Raisi aliyepo madarakani mpaka leo hakuna anayejua matokeo zaidi yake mwenyewe, kwa sababu matokeo yalitengenezwa. Wewe kwasababu unatumia kodi zetu kuishi, na kazi uliyopewa ni kutetea wizi wa demokrasia ili kulinda tumbo ndio maana unaongea lolote bila kupima hali halisi ya watanzania wa leo.

Swala la Arusha ni reflection ya taratibu zetu za uchaguzi, kama mmeweza kuzulumu kwenye uchaguzi wa watu wasiozidi 30. Je kwenye mamilioni mnafanyaje?? Ni wazi kama unapenda watu wako utapenda kuwafundisha haki na usawa na kuheshimu sheria tulizo jiwekea. Unapotaka kuwa kiongozi lazima uwe na misimamo, kuna wenye misimamo ya haki, na utawala wa sheria. kuna wenye misimamo ya kifisadi, wizi na ulaghai. Na kuna wenye misimamo ya ukweli uwazi . Wewe umechagua ulaghai kwa gharama za muafaka unaokulinda wewe. Kama mnapenda muafaka kwanini msifikie muafaka na Mapacha watatu, mgawane kugombea 2015.

Tuache unafiki na siasa za mkato. Nape aanza kuangalia uhalisia wa demokrasia yetu, utaheshimika. Ila kama utaendelea kutumika kama dodoki utajuta. watanzania wana njaa kubwa ya haki mbele ya sheria zao.
 
Binafsi nakushauri tumia busara zaidi unapokuwa unazungumzia mambo ya chama chenu kuliko kupita here and there kuzungumzia mambo ambayo hamyawezi kutekeleza,mfano issue ya mafisadi tayari imeshakuondolea uaminifu kwa wananchi.Ni matokeo ya kukurupukia issues,CCM wamekuweka hapo ili uweze kuvuta vijana nasikitika kukuambia kuwa vijana wasomi wa leo hawadanganyiki kirahisi ,fedha mnazowapa watachukua lakini maamuzi yanabaki kuwa yao.Nakushauri kwenye ukweli sema ukweli usiingize siasa wakati watu tupo gizani,wengine wanashinda njaa n.k
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE

salaam Bwn Nape, kwanza nakuomba uwe unaleta mada iliyoshiba ili hata atakayeingia Jf miaka mia ijayo aone uyu ndugu alikuwa anajielewa, ila kwa hoja zako ni fupi na haziwezi kukidhi mahitaji ya mtu mpya yani ni kama kwamba unaongea na mtu ambaye mnachat kenye ujumbe mfupi yani sms, pili ikumbukwe kuwa kila jumuiya ina mamlaka kamili na sheria zake, kwa iyo usitegemee muilazimishe chadema kama chama ikubali mawazo yaliyoingizwa kinyemela kwa madiwani. Ivi siku ile mlipowapinga na kuua watu wawili jan 5th pale arusha, kuna diwani mlimuua?je aliyekuwa anaratibu maandamano ya kudai haki ni hao madiwani 11? Je kwanini mugawane madaraka wakati mlidai cdm waongo? Je baada ya kugundua dhambi mlizofanya mnaamua kugawana madaraka au? je kesi ya maandamano inafutwa? je kwa iyo si sheria bali mnaamua kugawana mnavotaka? Tunapoelekea tutaanza kuvikataa vyama vyote vya siasa maana vyote viimeanza kuwa popo. Watanzania wanachezewa akili. unadai taifa kwanza?ivi yule diwani wa kusini aliyedai chiligati avue gamba mbona mlimsimamisha udiwani?? Hakuwa na utaifa kwanza?? ujue hapa jf si pa kuleta masihara kiongozi wangu!!! Nakutakia kazi njema.
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE

hii inadhihilisha jinsi gani viogozi wa ccm are dangerous and bad...............siasa zao ni za hila na udanganyifu! .....ni watu wamevaa mask usoni lkn ni mbwa mwitu!! Kwa kiongozi mwenye dhamira njema hawezi anzisha thread ambayo anajua ndani yake kuna hila na udanganyifu!! really bad!!
 
Mbona nasikia kuna baadhi ya madiwani wa ccm waliukataa muafaka huu na walihoji ni kigezo gani kilitumika kuwachagua hao madiwani wachache wa-wa represent madiwani wengine katika kikao cha maridhiano kwa mkuu wa wilaya?
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE


mkuu naona umekimbia Facebook umekuja kwa wanaume. Karibu sana. Ila kumbuka hapa jamvini pumba zinapewa zero tolerance.
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE

Nape katika hili la nchi kwanza chama baade nadhani dhana hii unaifahamu isipokuwa unatafuta kuitumia kwa maslahi ya ccm.

Nchi hii ina mambo mengi sana ambayo yamekuwa yakifanywa na ama kupitishwa na bunge lenye wajumbe wengi wa ccm kwa ushabiki na maslahi ya ccm badala ya wananchi. Kwahiyo kama ungekuwa muungwana na ili upate moral authority ya kuinyooshea kidole chadema basi ulipaswa kuanza na chama chako kwanza, kwenye mabaraza mbalimbali ya madiwani lakini zaidi kwa wabunge wa ccm. Ningeweza kukubaliana na wewe endapo ccm mngekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi kwanza.

Kwa kumalizia nikitumia maneno yako mwenyewe uliyozungumza kupitia radio deustch welle jana jioni niseme tu kwamba, hii hoja umeiokoteza barabarani, ama kwenye kijiwe cha ghahawa.
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE

sitakuwa na shaka yeyote na mada yako ya wanacnhi kwanza chama badae ukinijibu haya maswali yafuatayo.
1, ni kasoro gani zimejitokeza hadi kufikia hayo makubaliano ya muafaka?
2, kwanini chama chenu kikubali maridhiano kama kweli sheria za uchaguzi zilifuatwa?
3, unataka kuwa mshauri wa CDM? km jibu lako ni ndiyo, vua gamba lako na uende shule ukaongeze elimu yako then utaajiriwa na CDM.
 
Back
Top Bottom