Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?




Kama Kikwete mpole na msikivu hakuweka tume huru ya uchaguzi
utegemee Magufuli ambae ni jeuri mwenye kiburi aje alete tume huru ya uchaguzi?
seriously?
 

Hii inaonyesha uhusika wa moja kwa moja wa UWT kwenye chaguzi za JMT. Kura zetu hapa zina usalama gani?
 
ai
Hujaona connection ya Magufuli na Ngeleja na TISS ambayo
RaiaMwema waliisema?
 

Ninavyosoma mjadala unaoendelea inaonyesha hicho "Kitengo" ni zaidi ya chama, hivyo kura haiwezi kukiondoa labda tuwaze namna nyingine

(Nirekebishwe nilipokosea )
 

Enzi za chama kimoja sawa. Kwa zama hizi ambazo CCM ni chama dola hii ni hali isiyokubalika kidemocrasia. Reforms zinatakiwa kuwa na professionalized UWT.
 
Ninavyosoma mjadala unaoendelea inaonyesha hicho "Kitengo" ni zaidi ya chama, hivyo kura haiwezi kukiondoa labda tuwaze namna nyingine

(Nirekebishwe nilipokosea )

UKAWA ni kama hawajui wanachofanya nimaigizo tu
KITENGO ndio final say wa maamuzi ya nchi
 
Kama Kikwete mpole na msikivu hakuweka tume huru ya uchaguzi
utegemee Magufuli ambae ni jeuri mwenye kiburi aje alete tume huru ya uchaguzi?
seriously?
Kwani sio kitengo tena ni mtu mmoja sasa??!!!
 
Nyani Ngabu ume nail tu ....

Watu huwa nawaambia Uchaguzi mkuu ni ule wa Dodoma
October ni maigizo tu hawaelewi
cha kushangaza wapinzani nao wanashiriki haya maigizo vizuri saana
halafu watakuja kulalamika later..wanashangaza

I just don't get it. I just don't.

The opposition will never win the presidency under the current conditions. Never.

And that fact is as audible to the deaf as it is visible to the blind.

That's how obvious it is.

Tuliingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kubadili katiba. Iliyokuwepo iliwekewa viraka tu.

Mbona Afrika Kusini walipotoka kwenye Apartheid na kuingia kwenye demokrasia ya kweli walibadili na katiba?

Imagine serikali ya ANC ingekuwa inatawala kwa kufuata katiba ya Makaburu....

Tulipaswa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi na a brand new set of rules that is apropos for the new system.

Siyo kuja kuanza kuhangaika na katiba mpya miaka 20 na kitu baadaye.

Mimi nina imani kama tungeaza afresh hiyo 1992 basi huenda sasa hivi tungekuwa hata tushapata rais kutoka nje ya CCM.
 
Hili ni la waandishi wa habari ni tatizo kubwa,ila kuna tatizo pia la jamii yetu kupenda ku entertain ujinga na upumbavu wa waandishi wetu na watangazaji.
Huwa nasema,ktk fani inayohitaji watu bright na smart upstairs ni fani ya habari!Hawa watu wanapanda mambo kwenye vichwa vyetu,na kutia nuru faham zetu.Kama wakiwa ni wajinga,wapumbavu,wasio na ethics za fani zao,na wasioweza kutetea wanachokiamini,watakua wanajenga jamii ya ovyo isiyofikiria na inayo gamble na maisha yao kama tunavyoona jamii yetu ya Tanzania.Scope ya uelewa ya waandishi wetu ni ndogo sana.Wakowapi waandishi watakao hoji vitu vya ndani na vya msingi vitakavyookoa taifa letu?Wakowapi waandishi watakao kua wakiandika au kutangaza vitu vinavyo outsmart akili ndogo za wana siasa wanaotaka kurubuni wananchi?
Wako wapi waandishi watakao hoji watawala na kuwashinda kwa hoja juu ya maswala muhimu ya taifa letu?
Vyombo vyetu vya habari vimekua brain washing mashine badala ya kuwa taa taa kwa jamii.Yanahitajika mapinduzi makubwa!
 

Na wewe ni mwandishi au?
 
Kwani sio kitengo tena ni mtu mmoja sasa??!!!

Kwenye maelezo yako umesema kwa kumuweka mtu anaweza leta hayo mabadiliko
Sasa Magufuli sidhanikama nimsikivu enough hata kwa hao KITENGO
na power ya urais inampa nguvu hata ya kukisuka KITENGO kwa malengo yake
ni gamble ambayo watu wenye uzalendo wa kutosha wasingeifanya
 



Ndio maana mimi nilisema humu UKAWA kushupali ishu ya

serikali tatu kwenye bunge la katiba ilikuwa haiwasaidii
walipaswa hasa kushupalia 'Tume huru ya Uchaguzi'
kama ajenda namba moja......wao walisusa bunge kwa ishu ya Tanganyika...
now we are back at square one
 
Kwa hiyo hiyo habari ya kwamba CCM inafuata demokrasia ni uzushi tu?

Mgombea urais wa CCM, na hivyo rais wa Tanzania do far, anateuliwa na watu wachache, halafu wananchi wanapigwa changa la macho kwamba wamemchagua?
 

Hapo ndipo pazuri sasa kama unaamini kitengo kinaweza kuamua na kumuweka mtu sasa swali ni kwa makubaliano yepi, kwanini kitengo kiingie risk ya kuweka "traitor" . . . . . .. Keeping a lion for a later kill??!! Why this mess??!!!

Kennedy was a president too, vested with power . . . .. Very same power. . .what happened? ?!!!

Kama kweli kitengo kinaendesha nchi basi hakika suala sio dice rolling. . . .
 
Na wewe ni mwandishi au?
Hapana Kinjekitile juniour,Mimi ni mchambuzi tuu ninayependa kufikirisha akili Yangu na ninayetamani mapinduzi ktk fani ya habari,kwani ina impact kubwa kwa jamii
Kazi kubwa ya chombo cha habari ni ku magnify kitu kwa manufaa ya jamii.Ila kama chombo cha habari kitakua kinatoa ujinga,kitakua kina magnify ujinga kwa hasara ya jamii na ndicho kinachotokea kwetu
 
Last edited by a moderator:

Na kwa nini niamini kwamba kina kitengo zaidi ya Kikwete, Mwinyi, Mkapa and their few cronies?
 
Mkuu, umeleta mada murua wakati huu lakini inayohusu yaliyo wazi kabisa. Sitaki kuamini kuwa hukujua hilo. Labda jina "Kitengo" tu.

Hii nchi miaka yote imekuwa ikiendeshwa na "clique" ya watu waliofanikiwa kuingia kwenye mzingo wa ndani wa utawala ulioshika hatamu za chama (CCM).

NA, kwa bahati mbaya (kwa wasiopenda kusikia), mbunifu na mwashi mkuu wa mfumo huo ni Mwalimu JKN mwenyewe akitumia fikra za watu kama Kingunge kwamba wachache (wenye mwanga zaidi - the vanguard) waamue kwa faida ya wengi hata kama hao wengi watakereka (katika ujinga wao).

JKN hakuwa na imani na uamuzi wa wengi (demokrasia), lakini alifanya hivyo kwa makusudi "mema" kwa taifa - si ya kujinufaisha kibinafsi. Leo hii, vikundi vya kimafia vimeuteka mfumo huo na kuuboresha (perfect) ili usimamie maslahi yao ya kibinafsi. Na vimehakikisha vimeishikilia CCM kama luba. Mtu yeyote asijidanganye kuwa anaweza iondoa CCM kwenye madaraka ya urais kwa kura za wananchi. Naamini hata kina Lipumba na Mbowe wanalijua Hilo.
 
Na kwa nini niamini kwamba kina kitengo zaidi ya Kikwete, Mwinyi, Mkapa and their few cronies?

Sijui hiyo habari ya gazeti la Raiamwema uliisoma
inasema Usalama wa Taifa walimfuata Ngeleja ili atumie nguvu zake
kwa wajumbe wa Zanzibar kumuwezesha Magufuli kuteuliwa

'Usalama wa Taifa' gazeti hili ni credible Mwenyekiti ni Jenerali Ulimwengu
 
Kama Kikwete mpole na msikivu hakuweka tume huru ya uchaguzi
utegemee Magufuli ambae ni jeuri mwenye kiburi aje alete tume huru ya uchaguzi?
seriously?


nawashangaa sana wanaofikiri magufuli atafanya chochote kupendeza wananchi, hana hulka hiyo. Yeye ni mbabe, atafanya kitakachompendeza with impunity!

Muombe vitakavyompendeza viwafurahishe na nyie.kinyume na hapo wananchi imekula kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…