Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?

Na hakuna anaetaka kujadili hili
huu ni mwiko mkubwa demokrasia

Hili swala gumu...

Idara ya Usalama wa Taifa ina stake kubwa sana kwenye siasa. Kiuhalisia chombo hiki kinapaswa kuwa independent and doing a continuous job ya kulinda nchi regardless of the times.

Hebu tuchukue mfano wewe ungekuwa Mkurugenzi wa hii idara halafu ukaamua kuacha watu wafanye siasa watakavyo i.e wachague hata watu ambao unafahamu kuwa hawana maadili, huoni kama utakuwa ume-fail kwenye jukumu la msingi?

Mimi naamini tunawahitaji kwenye processes ndani ya vyama. Making sure kunakuwa na vetting ya kutosha, wanapaswa kufahamu kuliko sisi. Na ifanyike kwenye vyama vyote, kuwe na uadilifu wa kutoa wasiotufaa, ila baada ya hapo waachwe wakafanye siasa in a level playing field.

It's a difficult balancing act
 
ai
Hujaona connection ya Magufuli na Ngeleja na TISS ambayo
RaiaMwema waliisema?

Hakuna kitu hapo.Wanamsafisha Mukulu.Ngeleja ni mwizi tena kuliko hTa huyo Lowassa.Kitengo hicho kimeratibiwa ndani ya CCM kwa manufaa ya viongozi wachache.Huko ndani ya CCM kuna kitengo cha usalama lamini si TISS.Kaka siasa za Afrika ni majungu,uongo,mauaji yaani ushenzi wote uko huko.
 
TISS included!

Jamani siamini ila najua CCM wanakitengo cha usalama lakini hapa tukiwaincule Tiss tunawaonea.Hili limetengenezwa na ukoo w.kifalme ili kuisafisha wakatengeneza stori ya tiss.
 
Nasikitika kusikia usalama wa taifa 'kitengo' mlihusika kukatwa majina ya wagombea urais ccm.Tiini matakwa ya umma.

Unapokuwa na umma ambao akili zao zimejaa upofu kama wewe lazima wahusike tu. Maana hamumjui huyo mgombea nyie ndo maana mnaongea utumbo utumbo hapa.
 
Usalama wa Taifa au TISS kama wanavyoitwa ni moja ya majeshi ya nchi kama vile Polisi, JWTZ, Magereza au JKT. Watumishi wa majeshi haya kwa mujibu wa Katiba ya nchi hawapaswi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Lakini chini ya zuria ni wanachama. Hii nathibitishwa na mifano ya watumishi wengi wa majeshi haya kuteuliwa kushika nafasi za uongozi wa kisiasa kama Issa Machibya na J. Agustino Ramadhani kugombea kwa nafasi ya uraisi kupitia CCM.
Usalama wa taifa wana sub standards sana.
Wanaacha mambo muhimu ya nchi wanafanya siasa.
Hiko Kitengo kinatakiwa kijulikane ni kina nani hasa?
Wao ni kama nani watuamulie rais wa nchi?
 
unauhakika na ulichoandika!? Au ni chuki na mihemuko ndo inakusumbua!?
 

Uko sahihi kiasi fulani. Lakini usichanganye nchi na mifumo. Mambo ya Urusi/China yana tofauti kubwa na yale ya Marekani/Ugiriki. Kote kuna hivyo vinavyoitwa vitengo lakini miundo, majukumu na mamlaka ni tofauti. Kwa Urusi na China kama hapa kwetu, vina mamlaka kamili (absolute powers). Hata kuhusu uamuzi wa matokeo ya kura katika chaguzi za kisiasa. Yaani vinaamua hesabu ya kura aliyopata kila mgombea na chama. Ndio maana hapa kwetu hicho kikundi kinahakikisha ni yule mgombea anayekubalika na wenyewe ndani ya CCM pekee ndiye anayeshinda u-rais na si vinginevyo.

Huko Marekani, Ulaya Magharibi (EU block) na kwingineko kwenye mlengo sawa wa kidemokrasia km Japan na Korea Kusini, hivyo vikundi havina mamlaka kiasi hicho. Vinaweza kuangusha baadhi ya wagombea wanaoonkena hatari kwa mustakabali mkubwa wa taifa lakini, hatimaye, ni hesabu halisi za kura zilizopigwa na wananchi ndizo huamua ni nani na chama kipi ndio mshindi kati ya wagombea waliopitishwa na tume (huru) ya uchaguzi. Tena hufanya hivyo kimkakati sana si wazi kama huku kwetu ambapo hawajali kazi zao kujulikana. Kwa wenzetu, utasikia tu habari ya "conspiracy theories" katika mambo kama hayo.

Ndio maana kwa wenzetu, kura katika uchaguzi bado zina maana sana kuonyesha kukubalika au la kwa vyama na wagombea wake. Wanaweza hata kuendesha "opinion polls" zinazoshawishi kuonyesha mwelekeo wa umaarufu wa vyama na wanasiasa wake katika mazingira mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kiusalama, n.k. Huku kwetu hatuna hizo zaidi ya kuangalia ni nani anakubalika zaidi na rais aliyeko madarakani (na familia yake), wafanya biashara wakubwa, kamati kuu ya chama, n.k. ili tuhitimishe uwezekano wake kufika popote kisiasa. Vyama vya upinzani ndio hatuvifikirii kabisa. Ni kama vile vyama hivyo, wafuasi na mashabiki wake vimebakia kuwa "jokers in the pack"!
 
Napenda substance iliyoko kwenye uzi wako,ila umetumia maneno makali mno.
Unapokuwa na umma ambao akili zao zimejaa upofu kama wewe lazima wahusike tu. Maana hamumjui huyo mgombea nyie ndo maana mnaongea utumbo utumbo hapa.
 
Mkuu sometimes inabidi. Sababu watu wanalalamika sana hawajui hata hatari wanazoepushwa nazo

Hujaelewa kitu kabisa
Mimi binafsi nimempinga Lowasa humu sana
hapa ishu si Lowassa..ishu hapa ni kikundi cha watu kuwa na nguvu ya kuchagulia watu Rais
tuseme Lowasa hafai,Je Mwandosya hafai? Mahiga hafai?Augustine Ramadhan hafai?Mwakyembe hafai?Sitta hafai?
Mwele hafai?Monica hafai? why wao hawakupita tano bora?kitengo kilitumia vigezo vipi?
 
Mkuu sijakuzungumzia wewe.
 



Ahsante kwa your insight
 

Unawatetea sana KITENGO
kama vile unawajua au kuwaelewa sana
Au ndio 'utetezi wa wana Kitengo' ?ha haa
 


cc OLESAIDIMU Nyani Ngabu ....
naona jamaa kauliza very hard questions
 
Last edited by a moderator:

asante.
 
kama kitengo anachokisema kingunge ni kile kilichomng'oa jicho na kucha kibanda na ulimboka,basi kinajulikana.Kingunge alistaafishwa au kastaafu kwa hiari kitengoni?maana tukizungumzia unyama wa kitengo,kingunge alibobea humo!!!!now that they have turned on each other,dirty lingeries are washed in public now....the pirates' ship is sinking.
 
Hawajijui nafasi yao
badala ya kuwa 'loyal subject to the Republic'
wao nao ni loyal subjects to CCM......so shameful

The Boss,

Huoni kwamba kwa wao kupendekeza taarifa za kukatwa kwa Lowassa walikuwa loyal subject to the Republic?. Umewahi kujiuliza nini kingetokea endapo wangeruhusu Lowassa apitishwe?

Ndiyo 2005 walishindwa kutimiza wajibu wao, lakini mwaka huu wameweza. Isitoshe wao wako better placed kujua nyendo za ndani kabisa za wagombea wote.

By the way, hivi kwani vyama vingine wamezuiwa kutumia huduma za "kitengo" kupata taarifa sahihi za wagombea wao? Au ni muendelezo wa malalamio ya watanzania kama ilivyozoeleka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…