Nchi imekauka, mambo hayaendi...

Awamu hii mtu hafanyi biashara ili apate faida
Anafanya biashara ili alinde mtaji wake tu
Kila kukicha ni bora ya jana,ndio kwanza ni miaka mi3 tu,bado miaka 7 inatusubiri.
Safari hii nikunyooshwa hadi ukiitwa unaitikia “Abeee!!!”[emoji38]
Kama kweli, kabla ya Serikali inayoongozwa na Magufuli, watu walitajirika, utajiri ungeonekana kila mahali. Lakini kila kona ya nchi vijijini umaskini ulinuka huku mijini tukishuhudia majumba ya fahari, maduka makubwa yenye bidhaa za nje, na utitiri wa machinga wakitembeza bidhaa za nje.

Isitoshe huduma za jamii ziliendelea kudorora kiasi cha kufanya ongezeko la rushwa ili mwananchi aweze kuzipata.

Ndiyo nchi tunayotaka iendelee kuwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi nilikuwa napiga stori na jamaa zangu fulani ni mafundi ujenzi. Jamaa anasema ameshakaa miezi 8 bila kupata tenda yoyote ya kujenga hata ukuta wala choo. Kiukweli hali ni mbaya sana mtaani. Ila kuna watu wanasema wanaolalamika walikuwa wapiga dili.
 
Acha kulia lia, kila sehemu hivi hivi, hujui kinachoendelea duniani wewe, unadhani viongozi ndo wanaleta raha?
Angalia pia Venezuela, hapo Zambia hadi wamebadirisha currency, Nigeria vivyo hivyo nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kulikuwa na nafuu, sasa hivi hali mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa.

Kama ni mgonjwa basi katoka wodini kapelekwa ICU
 
kwa hiyo mkuu umepata unemployment benefit kwa huyo shemela?
 
Ple kwa kuwa uzembe umekutawala Fanya Kazi utaona tofauti
Watu wengi hukimbilia kusema fanya kazi. Ushajiuliza wafanye kazi gani? Hakuna binadamu yyte asiyependa kufanya kazi na asiyependa hela. Watu wapo vijiweni nenda ukawaambie kuna kazi ya kuchimba choo uone watakavyokukimbilia. Watu wanafanya kazi lkn hela haionekani.
Tumia kichwa chako kufikiri lkn ukitumia kichwa cha wanaccm ndiyo matokeo yake haya utaishia fanyeni kazi.
Masikini utakuta ww hapo ni muajiriwa, unasubiria mwisho wa mwezi pesa ingie kwenye account. Km umeajiriwa acha hiyo kazi halafu ingia kitaa ufanye kazi maana huku kazi ni nyingi sana
 
Acha kulia lia, kila sehemu hivi hivi, hujui kinachoendelea duniani wewe, unadhani viongozi ndo wanaleta raha?
Angalia pia Venezuela, hapo Zambia hadi wamebadirisha currency, Nigeria vivyo hivyo nk

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana tena pole sana.
Nyie ni wale watu wanaopenda kujifananisha na watu wengine. Ww ukiwa masikini halafu ukimuona jirani yako masikini roho yako inaridhika.
 
Kipindi cha kikwete mgonjwa alikuwa wodini ila kwa kipindi cha Makufuli mgonjwa kapelekwa ICU
Huoni mpaka Ruge amekuwa omba omba
 
Yani Frame zimefungwa kama vile hazijawahi kufanyiwa biashara mpaka Makufuli yamepata kutu...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ila magu kukaza anazidisha mamaee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana naona umejibu kwa mhemuko kuliko uhalisia wenyewe. Nafikiri lbd utakuwa jiwe mwenyewe au ni mwanaccm anayetetea chama chake.
Wazungu wanasema NO RESEARCH NO RIGHT TO SAY. Alichokiandika bibie na ww kipo tofauti kbsa km kwenye mtihani una marks 2 za kupotezea wino. Soma tena alichoandika bibie halafu soma ulichokiandika ww. Kwa watu km nyinyi ndiyo maana ikawekwa dvn 5
 
Naishi Dar, mtaani ninakoishi ni mtaa wa wafanyabiashara,ukweli kabisa, wengi wamejenga awamu hii, maghorofa na nyumba nzuri nzuri, Binafsi toka mwaka jana nimeingia kwenye ufugaji wa kuku wa nyama, kawaida nilikuwa nafuga kuku wa kiswahili nilikuwa napata pesa, lakini sio kama kuku wa nyama, ndani ya wiki 4 ukiuza hawa kuku Unaiona pesa na unafanya kitu.
 

Siyo kila mtu ni mfugaji wa kuku wa nyama.!

Ni majuzi tu mzigo wa vifaranga ulikuwa adimu ni balaa!. Kodi kodi kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…