Nchi hii imeshindikana,tubadilike

choga mkuu

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
283
110
Ndugu wanajamvi?

Jana tuliona uteuzi wa makatibu tawala ambao umeendelea kuthibitisha kuwa nchi haijui inaelekea wapi. Uteuzi huu na hata unaofuata unaendelea kukatisha tamaa maana wateule wanatia mashaka,mfano mwanafunzi wa taasisi ya elimu ya watu wazima ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM tawi hilo kateuliwa kuwa katibu huko Liwale.Hii inaonesha wasiwasi mkubwa huko tuendako.
 
Ndugu wanajamvi Jana tuliona uteuzi Wa makatibu tawala ambao umeendelea kuthibitisha kuwa nchi haijui inaelekea wapi . uteuzi huu na hata unaofuata unaendelea kukatisha tamaa maana wateule wanatia mashaka ,mfano MWANAFUNZI WA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA ambaye kwa sasa ni mwenyekiti Wa ccm tawi hilo kateuliwa kuwa katibu huko LIWALE , . Hii inaonesha was was mkubwa huko tuendako.

Shinda uchaguzi kwanza ndiyo ubadilishe!
 
Kwahiyo mtu akihitimu elimu ktk taasisi hiyo hafai kushika nyadhfa fulani?
 
Ndugu wanajamvi Jana tuliona uteuzi Wa makatibu tawala ambao umeendelea kuthibitisha kuwa nchi haijui inaelekea wapi . uteuzi huu na hata unaofuata unaendelea kukatisha tamaa maana wateule wanatia mashaka ,mfano MWANAFUNZI WA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA ambaye kwa sasa ni mwenyekiti Wa ccm tawi hilo kateuliwa kuwa katibu huko LIWALE , . Hii inaonesha was was mkubwa huko tuendako.

Sijajua lengo la mada yako ni nini lakini nakubaliana na wewe kwa jambo moja: Baadhi ya walioteuliwa hawajawahi kufanya kazi za utawala au utumishi, nawafahamu vijana watatu. Hii ni hatari, nina hakika Rais JPM hajajua namna anavyochezewa na baadhi ya watu wanaohusika na uteuzi...District Administrative Secretary ni nafasi nyeti wilayani...unamchagua mtu aliyebobea katika masuala ya utumishi na utawala na wengi ni lazima wawe within the establishment...sasa ukimteua mtu kwa kuwa tu alikuwa anaandika kwenye mitandao au anapiga picha za kampeni na kupost kwenye mitandao hiyo ni hatari...Narudia hiyo ni hatari...ukimchagua mtu kuwa DAS kwa kuwa aligombea ubunge na hana sifa nyingine za elimu katika uongozi na utumishi ni hatari...wapo baadhi walioteuliwa kuwa ma-DAS mimi binafsi sina shaka nao hata kidogo...lakini wengine, NO, NO, NO...hata hivyo nawapongeza wote inawezekana Mungu atawasaidia.... lakini ni dhahiri kutakuwa na kilio kikubwa katika utumishi huko wilayani....
 
Kwa unavyojua ninan alishinda kihalali uchaguzi Wa oktoba 25? Zanzibar unavyojua nan alishinda uchaguz?

Unaweza kuamini unavyotaka kuamini lkn Dunia nzima inajua kwamba raisi wa JMTZ ni Dr.Pombe Magufuli chini ya CCM!
 
Ndugu wanajamvi?

Jana tuliona uteuzi wa makatibu tawala ambao umeendelea kuthibitisha kuwa nchi haijui inaelekea wapi. Uteuzi huu na hata unaofuata unaendelea kukatisha tamaa maana wateule wanatia mashaka,mfano mwanafunzi wa taasisi ya elimu ya watu wazima ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM tawi hilo kateuliwa kuwa katibu huko Liwale.Hii inaonesha wasiwasi mkubwa huko tuendako.
Ulitaka wateuliwe wanaogomea hata bunge! Je wakigomea kufanya kazi za wananchi itakuwaje?
 
Sawa, ila aliyeshinda ni nan? Sijauliza rais Wa Tz ni nan , aliyeshinda ni nan?

Raisi wa JMTZ ndiye aliyeshinda Uchaguzi, kwa mujibu wa Katiba ya JMTZ, wasimamizi wa Kimataifa (AM,SADC,AU,EU,USA,Uchina ) ambayo imeelezea jinsi ambavyo raisi wa JMTZ anapatikana!
 
Tunatengeneza taifa litakalo ignore ushindani na utashi na kukumbatia kujipendekeza
 
UTUMISHI wa umma hauendani na uchaguzi, unaendana Na SHERIA, kanuni Na taratibu Za UTUMISHI wa umma

Ndiyo hapo sasa kama una malalamiko na haupendi jinsi mambo yanavyofanywa njia pekee ya wewe kulibadilisha ni kushinda Uchaguzi kwanza ili uweze kuweka Serikali uitakayo!
 
Kuna msemo usemao, Old is Gold. Actually u can not sweet away the old system abruptly. That's why there is transitional period jaman. Sisi vjana tunataka madaraka lkn bdo hatujawa wazoefu kupata cha kujifunza kwa wazee watu. Ukubwa dawa oooooh!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom