Nchi haiwezi kuendelea kwa kutegemea walevi, wavuta sigara na wanywa soda!

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
Inasikitisha kuwasikia wengi wa wabunge wetu wakilalamika kwamba kwa nini mpango wa bajeti wa mwaka huu umeamua kuongeza kodi ya shs 50/ kwa lita ya mafuta ya taa, diseal na petrol badala ya pombe, sigara na soda kama ilivyo ada.. Wanaamini kwamba maendeleo ya nchi yetu yataletwa na kodi za walevi, wavuta sigara na wanywa soda. Kwa akili yao wanaamini kabisa kuwa hiyo ongezeko ya sh 50/ kwa lita ambayo ni mchango wao wa kupewa umeme utawafanya wananchi hawa kuwa masikini zaidi na kwamba mchango huo ungebebeshwa walevi na wavuta sigara. Wao wenyewe wabunge hawataki kuchangia kwa kupunguza kiinua mgongo chao bali wameomba na kukubaliwa kuongeza kiinua mgongo chao kwa asilimia 200% ya mwaka 2010. Ongezeko hili la kinua mgongo chao wanataka nalo litoke kwa walevi, wavuta sigara na wanywa soda / juice /chocolate! Hii ndiyo akili ya wabunge wetu. Wanaamini kuwa nchi kama China, Amerika, Singapore nk zimeendelea na zinandeshwa kwa kodi za walevi!

Kweli Katiba iliyopendekezwa bado inahitaji maboresho kwa baadhi ya vipengele. Moja ya vipengele hivi ni umuhimu wa mbunge kuwa na angalao shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu, hasa ikizingatiwa pia na kiwango cha mshahara, marupurupu na pensheni (230 m) inayoambatana na cheo hiki serikalini. Kukwama kwa kura ya maoni kuhusu Katiba inayopendekezwa 'is a blessing in disgust'. Inatupa fursa ya kuiboresha zaidi kwa masuala kama haya (achana na hayo ya serikali 2 ao 3 ambayo hayana masilahi yo yote kwa mwananchi wa kawaida) baada ya Uchaguzi Mkuu ujao.
 
Back
Top Bottom