I do not mean to be rude but Mwandishi alipaswa kutumia jina zima la huyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji throughout the article kwa sababu anapoandika 'Chizi' peke yake ananikwaza.
Tukumbuke tunaongelea ATCL kubaki shirika la ndege bila kuwa na vitendea kazi vya kufanikisha utolewaji wa huduma ya usafiri wa anga ambayo ndiyo core b'ness.
Halafu unasoma maelezo ya utetezi yanatolewa na 'Chizi'.I've failed to tame my sense of humor.
Nautakia kila la kheri uongozi wa ATCL katika kuendelea kuitia serikali gharama ya kukodi ndege kutoka kwa mashirika binafsi kwa kodi za watanzania ili kujionyesha kwamba wako hai ilhali ni maiti.
Pia ukarabati mwema wa hiyo scrap moja iliyobakia.
Miaka 50 ya uhuru.Wamethubutu kufilisi ATCL kwa ufisadi na hujuma,wanaweza kuendelea kuwabebesha mzigo walipa kodi na wanasonga mbele bila ya kuwa na ndege.
CCM Oyeee!!