Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

shaurimbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
1,915
Reaction score
2,337
Habari wadau.

Naona watu wote wanaonizunguka hawana furaha kabisa ni kama watu waliokata tamaa.

Nikiangalia status za watu social network, ofisini, kwenye dala dala.. na hata mtaani kwangu watu wapo kimyaaa wana huzuni tele.

Hii ni changamoto kubwa sana kwa magufuli kufanya kazi kwa bidii kurudisha furaha kwa mamilion ya watanzania.

Kiukweli leo ni kama kuna msiba wa taifa.
 
mtoa mada upo sahihi kabisa. ...taft ambazo zimewahi fanywa hapo juzi kati zinaonesha tzn ni nchi ya 113 ambayo watu wake hawana furaha....nahis tuna amani ya nje lkn ndani ya mioyo ya watu hakuna amani
 
Nilikuwa Nazi 1 DSM ,mji UK kimya kabisa
 
Nilikuwa MNazi 1 DSM ,mji UK kimya kabisa
 
Kweli mpaka maofisini tena ofisi nzito furaha zilianza kutoweka tangu Matokeo ya wizi yakijumlishwa. Ni majonzi.
 
Hata huku ni kimyaaaaaa jamani raisi hata watu hawafurahiiii tatizo sio maguful tatizo ni ccm
 
Kuna dude la CCM limekuja linaniuliza eti vipi , nikamwambie naomba usinitafitie kesi, nitakufumua nikafie jela.

Alafu nisikie pumbavu lolote linakuja kuomba pesa ya kununua mbegu za shamba eti nitakupa mazao yakikomaa, pumbavu, nenda kapige push up Lumumba upate pesa.
 
Nilikuwa maeneo ya Mwenge nilichokiona nimebaki mdomo wazi!watu walibaki kimya kwa mshangao!hakuna aliyeshangilia!Magufuli una kazi kubwa ya kurudisha imani kwa watanzania!
 
hata mbeya nimeona kimya tu....ingawa kuna kikundi kidogo ambacho watu walikuwa kama wanakishangaa tu kwa kufurahia matokeo ya Magufuli kuwa Rais, nimeona kidogo pale Lumumba na Chato kwa Mheshimiwa. Ila pande zingine nyingi watu wapo tu hawana jipya, inaonekana wamekata tamaa na hawaoni kama kuna matumaini...nimeamini EL alipendwa sana, yaani hapa JPM ajitahidi tu kuwaridhisha watu....yaani hakuna shangwe nchi nzima...why??? wajitafakari.
 
Acheni kujifariji. Magufuli hahitaji tabasamu wala kelele za mtu. Anasema yeye ni kazi tu. Wengi hawana furaha kwa sababu walidanganyika na nyomi. Wakasahau nyomi sio kura. Sasa rais keshapatikana wala hahitaji tabasamu lako. Anataka ufanye kazi tu.
 
Raisi wa roho za watu na si fisadi wa Democracy....
 
Yaani ni shida. Maofisini, Mitaani na hata ukipanda daladala unaona kila mtu kimyaa. Nyuso hazina furaha kabisaaa. Yaani ni zaidi ya msiba.
 
Back
Top Bottom