Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,810
- 11,978
Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam, jana 20/01/2022 imetupilia mbali pingamizi la awali lililowekwa na Jamhuri dhidi ya Shauri la Kikatiba lililofunguliwa na Baraza la Wadhamini la NCCR-Mageuzi linalopinga kitendo cha jeshi la Polisi kuzuia kufanyika kwa mikutano ya vyama vya Siasa nchini.
===
NCCR-MAGEUZI: Tunapenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa, Mahakama Kuu Dar es Salaam, Kesi iliyofunguliwa na Chama chetu cha NCCR-Mageuzi Kesi Na 27 ya 2021 ambayo tumewashitaki (Mwanasheria Mkuu, IGP, RPC Kanda Maalum DSM, RPC-Ilala, na OCD-Ilala, imeendelea chini ya Jaji JOHN MGETTA ambapo Mahakama imetoa maamuzi ya pingamizi lililowekwa na serikali.
Mahakama chini ya Jaji MGETTA imetupilia mbali pingamizi la awali lililowekwa na serikali.
Shauri litatajwa tena mbele ya jopo la majaji watatu tarehe 7 Februari 2022 Saa 8:00 Mchana, Mahakama Kuu Dar Es Salaam, kwa ajili ya kupanga tarehe ya kuwasilisha hoja za msingi za namna Jeshi la Polisi (@tanpol) lilivyokiuka Katiba na sheria za nchi.