NCCR ilishinda kwa mtaji wa Chadema Kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR ilishinda kwa mtaji wa Chadema Kigoma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by nngu007, Apr 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  KATIKA historia ya uchaguzi wa vyama vingi mkoani Kigoma, Oktoba mwaka jana NCCR-Mageuzi imeandika historia kwa kutumia mtaji wa wanachama wa Chama cha
  Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuibuka washindi.

  Duru za kisiasa mkoani humo zimethibitisha kuwa kati ya wabunge wanne wa NCCR-Mageuzi, wawili walikuwa viongozi na wanachama wa Chadema. Chadema ilipoteza viongozi hao na
  wanachama wake kutokana na sababu nyingi zikiwamo za kusimamisha baadhi ya wagombea
  walioenguliwa au kuachwa na chama tawala au na vyama vingine.

  Upande wa pili wa kushindwa kwa chama hicho, kunatokana na kunyemelewa na mdudu wa migogoro ndani ya chama, migogoro ambayo ilisababisha baadhi ya viongozi wa chama
  hicho kususia wagombea na kushindwa kuwanadi.

  Kutokana na mtafaruku huo ndani ya Chama, baadhi ya vijana waliokuwa wamejipanga kuingia bungeni, waliamua kuihama Chadema na kuingia kugombea ubunge kwa tiketi ya NCCR
  –Mageuzi.

  Wabunge wa NCCR- Mageuzi ni Felix Mkosamali wa Muhambwe, David Kafulila wa Uvinza, Mosses Machali wa Kasulu Mjini na Zeitun Buyogela wa Kasulu Vijijini. Si kwamba NCCR-Mageuzi haikuwapo mkoani humo; ilikuwamo lakini haikuwa na wanachama wengi hivyo wa kuweza kukipa ushindi mkubwa kiasi kile.

  Chama chenye wanachama wengi mkoani humo ni CCM ikifuatiwa na Chadema, ndipo kidogo kinakuja NCCR, Chama cha Wananchi (Cuf) na Sauti ya Umma (Sau) yenye wanachama
  wachache kabisa.

  Hivyo ushindi wa NCCR – Mageuzi katika majimbo hayo manne mkoani Kigoma, mawili yakiwa
  Kasulu, moja Kigoma na lingine Kibondo, ni mtaji wa wanachama wa Chadema. Ushindi huo ulitokana na migawanyiko ndani ya Chadema iliyoinufaisha NCCR nyakati za lala salama.

  Ushindi huo ni sawa na mechi ya mpira, mshindi wa kweli ni yule anayeibuka na magoli mengi zaidi dakika ya tisini ikishafika. Unaweza kudhani umeshinda kabla mechi haijaisha, dakika za
  mwisho mambo yakageuka.

  Ndicho kilichowakumba Chadema. Chama kiliwaandaa wanachama kisaikolojia, lakini kutokana na mgawanyiko kuwasimamisha wagombea waliosuswa wasiouzika, wapigakura wakawachapa bakora kwa kuwachagua chipukizi wa NCCR-Mageuzi.

  Miongoni mwao ni Mkosamali ambaye ni mbunge kijana zaidi kuliko wabunge wote nchini.
  Mmoja wa wananchi wa Kigoma, Hamad Ahamed anasema kwamba pamoja na kura zao kuwapa wagombea wa NCCR-Mageuzi bado wao ni mtaji wa kambi ya mageuzi, wao wanaipinga CCM wala si chama kingine cha upinzani.

  Hivyo mwaka mwingine ikitokea kuwa NCCR- Mageuzi imewachefua dakika za mwisho watakipigia kura chama kingine kiwe Cuf au Sau, ambavyo ndivyo vyenye matawi mkoani
  humo.

  Sau kinawika Ujiji na vijiji vinavyozunguka makao makuu ya mkoa, Cuf wapo Uvinza, Nguruka na maeneo mengine ya Kigoma Vijijini. Mwenyekiti wa NCCR, James Mbatia kwa kutambua fadhila za watu wa mkoa huo kumpa wabunge wanne, ameamua kuwatembelea na kuwashukuru wapiga kura mkoani humo.

  Katika ziara yake hiyo, Mbatia aliwapa asante wabunge wake na watu waliokipigia kura chama chake na kuibuka na ushindi katika majimbo manne. Nzuri zaidi katika majimbo hayo manne ni kwamba mmoja wa wabunge hao ni mwanamke ambaye kutokana na uhodari wake, amechaguliwa kuwa mmoja wa makamishna saba wa kumshauri Spika Anne Makinda.

  Kwa nyakati tofauti, Machali na Zaituni waliahidi kuwa chachu ya maendeleo na kukiendeleza chama mkoani Kigoma. Pamoja na kukidumisha chama, watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatetea maslahi ya wanachama na wananchi kwa ujumla, ili kuhakikisha haki zao, mfano za kuporwa ardhi zinarudishwa.

  Kitu cha ajabu si wanachama wa Chadema mkoani humo tu waliokiacha chama ‘solemba’ karibu na wakati wa uchaguzi, hata wanachama wa CCM walikipiga bakora chama chao kwa mtindo huo huo baada ya kusimamisha wagombea wasiouzika.

  Mtindo huo wa watu wa Kigoma, umeibuka pia katika sehemu nyingine nchini, ambapo wanachama wa vyama mbalimbali bila kujali itikadi zao waliamua kuchagua wagombea wa
  chama chochote walioonekana kuuzika.

  Uchaguzi wa mwaka jana, ulikuwa na msukumo wa aina yake, kwamba katika maeneo ambayo watu waliokuwa wamechoshwa na mbunge au wabunge waliotangulia, waliamua kuziacha pembeni itikadi za vyama na kumchagua mtu waliyeamini atatetea maslahi yao badala ya kupoteza muda bungeni.

  Mkoa wa Kigoma umeweka historia kutokana na uamuzi wa dakika za mwisho dhidi ya vyama ambavyo vilikuwa na sera, wafuasi na wanachama wengi.

  Vimejikuta vikipoteza majimbo kutokana na uchaguzi uliofuata zaidi hisia badala ya si uwezo au kukubalika kwa mgombea. Mfano hai ni katika jimbo la Muhambwe ambalo CCM ilimsimamisha Jamal Tamimu, Chadema wakamsimamisha Arcado Ntagazwa baada ya kujiengua CCM ambako alihudumu kwa miaka 25 na NCCR ikamsimamisha Mkosamali.

  Chadema ilishindwa kusoma alama za nyakati, kama ambavyo CCM haikubaini kwamba imechanga karata vibaya kwa kudharau nafasi ya wanachama katika uchaguzi.

  Kizazi kipya – vijana, ambacho ndicho wapiga kura wengi kinataka mageuzi; kinaona wazee hawawezi kuleta mageuzi, na kama chama kimoja kinasimamisha wazee basi ni rahisi chama hicho kupoteza jimbo hilo, kutegemeana na mhusika mwenyewe lakini.

  Ndicho kilichotokea katika jimbo hilo, wanachama wa CCM ambao wamekerwa na mfumo wa
  umangimeza, waliamua kuvunja kanuni na miiko ya chama, wakampigia kura Mkosamali, wakijikita katika misingi ya kuwa hiyo ndiyo damu chama itakayoleta mageuzi ya kweli jimboni humo.

  Wanachama wa Chadema ambao hawakupoteza muda kumpa ulaji mgombea wao, alihamishia
  nguvu zao kumuunga mkono Mkosamali, akashinda kwa ushindi wa kishindo. Katika majimbo mengine vile vile, wagombea waliokuwa wamepitwa na wakati, haikuwa rahisi kupenya
  kwenye tundu la sindano, hivyo wakaambulia kugalagazwa.

  Ushindi wa Kafulila, Machali na Zeitun pamoja na Mkosamali, umeipa uhai NCCRMageuzi
  mkoani Kigoma ambayo ilikuwa inachungulia kaburi kwa idadi ndogo ya wanachama.

  Ndiyo maana kutokana na ushindi huo, NCCR imeamka usingizini kwa nguvu mpya ya kushika majimbo mengi mkoani humo na kuanzia hapo cheche zimeanza kusambaa katika majimbo mengine ndani na nje ya mkoa huo.

  Siasa ni sawa na kuchanga karata, unaweza kuwa bingwa wa kuandaa karata, lakini mchangaji mzuri akishika, akakufunga bao, hilo ndilo lililowakumba Chadema kupoteza vijana wake dakika za mwisho.
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Mkono wa Zoka upo kwenye ushindi huu.
   
 3. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ok, kila lakheru NCCR
   
 4. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ninakubaliana na wewe kabisa. siyo Zoka peke yake bali alishirikiana na Zitto kutekeleza mpango huo. Kuanguka kwa CDM kule Kigoma kulichangiwa na Zitto. Kama hili ninalolisema siyo kweli, Zitto kama naibu katibu mkuu wa CDM na mbunge anayetokea Kigoma kupitia CDM atuambie alifanya jitihada gani kuhakikisha CDM inashindi.

  Wakati Zitto alipojipanga kugombea uenyekiti wa CDM aliwatumia kina Kafulila kumnadi yeye na walitumia media kwa kiasi kikubwa. Kina Kafulila wakati huo ni waajiriwa wa Sekretariet ya CDM taifa. Hivyo, baada ya kuondolewa kwenye ajira ya Sekretariet wao wakajiondoa kwenye Chama. Kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana Zitto alisema wazi wazi kuwa atamsaidia Kafulila katika harakati za ubunge bila kujibu swali(hata kama hajaulizwa) kuwa itakuwaje endapo katika jimbo hilo atakalogombea Kafulila kutakuwa na mgombea wa CDM?

  Hata hivyo kuna tetesi kuwa Zitto aliwanadi wagombea wa NCCR - Mageuzi badala ya wagombea wa CDM. Kama ni kweli, Je, Zitto alikuwana na lengo gani katika hilo?
   
 5. J

  Joshua Bukuru Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Niongezee tu kwamba, kigoma ni moja ya mikoa ambayo inapigania mageuzi na wana kigoma siku zote ni wana mapinduzi. Katika Tanzania yetu, ukiambiwa mabadiriko, utayakuta katika mikoa mitatu tu, kigoma, kilimanjaro na Pemba. Mikoa mingine inafuatia kwa mbali sana. Unajua, kigoma ni mkoa ambao ulisahauriwa katika maendeleo na mmekuwa mkitubeza kuwa ni mwisho wa reli na eneo la manamba enzi za ukoloni. Umanamba huu umeendelea hata baada ya uhuru na ndiyo maana CCM kimechukiwa sana kigoma, na nitahadhalishe hapa, 2015 mnaweza mkajikuta majimbo yote yanaangukia upinzani. Nini mfanye ili imani yenu irudi kwa wana kigoma? Peleka maendeleo na timiza ahadi zote ulizoahidi. Kigoma oyeeee!!!!!!! Kigoma is always for opposition!:yawn:
   
 6. s

  saguge Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba nguvu hiyo ni ya chadema ila katika hali ya kawaida ni lazima hatua kuchukuliwa kwa viongozi ambao hawafuati katiba,kanuni na utaratibu hata kama watatishia kuhama chama ili kulinda nidhamu ya chama .vinginevyo chama kitaharibika kikisubiri kujivua gamba.
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hili liko wazi
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Naungana na mtoa hoja kuwa ushindi wa NCCR ulitokana na vyama vingine(SI CHADEMA) kulumbana hivyo kupiga kura za hasira...!
  UBUNGO....angesimama NAPE jimbo lilikuwa la CCM
  IRINGA..... angesimama MWAKALEBELA jimbo lingekuwa CCM
  MUHAMBWE...asingesimama JAMAL TAMIM (ndugu wa damu wa dr. leakey mchambuzi wa soka kwenye TV) jimbo lingebaki CCM
  KAWE..... mtoto wa warioba alikubalika jimbo lingekuwa CCM(japo ameanza siasa za majitaka dhidi ya ccm)
  mifano hai ni mingi....ila nasema leo, katika majimbo haya....uchaguzi ukirudiwa hata leo.....SI CHADEMA SI NCCR ..majimbo yana wenyewe na wenyewe ni chama cha mapinduzi...!
  NB:
  hapa sijataja pemba,na majimbo mengine ambayo ni ngome kuu za vyama husika
   
 9. N

  Nanu JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  NCCR Mageuzi ni wapinzani pia. Hivyo wao kuchukua majimbo Kigoma ni sawa tu. Chadema waongeze nguvu 2015 waongeze majimbo mengi mengine hasa Zanzibar na Pemba pia. Wafanye kazi nzuri ktk ile mikoa waliyopata uwakilishi na wafanye propaganda nzuri ktk mikoa ambayo hawana wabunge!!! Hii itawaongezea majimbo. Hii kazi inabidi ianze sasa na siyo kesho! Wakijenge Chama from grass root na wasimamishe wagombea katika majimbo yote na kata zote!
   
 10. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mpira kam unaelekea golini huwezi kuliita goli maana hujui kitakachotokea ghafla. Dhambi huwa baada ya tendo , na mtenda dhambi ndo anagundua.
   
Loading...