NBAA haijaundwa kuendeleza wahasibu bali kuwadidimiza

Ndugu watanzania na wahasibu wenzangu , napenda kuchukua nafasi hii adimu kwa kueleza kilio changu kuhusu hii bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu Tanzania (NBAA).

kWA KWELI BODI HII IMEUNDWA SI KWA LENGO LA KUENDELEZA WAHASIBU BALI KUWADIDIMIZA NA KUWAKANDAMIZA KABISA WASIWE WENGI KATIKA NCHI HII.

Wewe embu fikiria, mtu anafanya mitihani ya Module F kwa miaka kumi (10) na hapati hiyo CPA. Unafikiria nini hapa ?
Mwengine anakuja kupata hiyo CPA amebakisha miaka mitano tu ili astaafu. Hivi hii CPA maana yake nini ? Hivi watu wanaisoma CPA ili waende kuitumia Duniani au kuitumia kaburini? Sasa iweje kuipata kwake iwe mbinde ?

Tangu NBAA ianzishwe mwaka 1972 walioipata hawavuki watu elfu nne(4,000) hii ni pamoja na walioipata na tayari wameshakufa. Hivi kusomea CPA na "udaktari wa upasuaji wa binadamu " ipi ni fani ngumu zaidi ? Iweje CPA kuipata inakuwa mbinde ?

Vyuo vyote nchini kwa mfano pale Mlimani ukiangalia idadi ya wanafunzi waliohitimu wakati chuo kinafunguliwa na mpaka sasa idadi ya wanafunzi waliohitimu imeongezeka na wamehitimu watu wengi zaidi, yaani maelfu kwa maelfu.
Lakini siyo kwa CPA ni miaka 50 sasa tangu tupate uhuru lakini walioipata hiyo CPA hawazidi elfu nne.

Nauliza hiivi, hii bodi imeundwa kwa ajili ya kuwaendeleza wahasibu au KUWAKANDAMIZA wahasibu ?
Kaza n'nya dogo unafikiri maisha urojo! Google hata CPA ya marekani uone habari yake! Gangamala otherwise maisha nayo yakikupiga sijui utamlilia mkeo! Kuna madogo ndani ya mwaka wanalamba CPA sasa wao wachawi! Usipoijulia mitihani ya professional lazima uchonge ngenga kijana! Dogo langu limebakiza Contemporary Issues in Accounting alambe CPA wewe unalialia! Kaza n'nya hiyo wewe!!
 
Ndugu watanzania na wahasibu wenzangu , napenda kuchukua nafasi hii adimu kwa kueleza kilio changu kuhusu hii bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu Tanzania (NBAA).

kWA KWELI BODI HII IMEUNDWA SI KWA LENGO LA KUENDELEZA WAHASIBU BALI KUWADIDIMIZA NA KUWAKANDAMIZA KABISA WASIWE WENGI KATIKA NCHI HII.

Wewe embu fikiria, mtu anafanya mitihani ya Module F kwa miaka kumi (10) na hapati hiyo CPA. Unafikiria nini hapa ?
Mwengine anakuja kupata hiyo CPA amebakisha miaka mitano tu ili astaafu. Hivi hii CPA maana yake nini ? Hivi watu wanaisoma CPA ili waende kuitumia Duniani au kuitumia kaburini? Sasa iweje kuipata kwake iwe mbinde ?

Tangu NBAA ianzishwe mwaka 1972 walioipata hawavuki watu elfu nne(4,000) hii ni pamoja na walioipata na tayari wameshakufa. Hivi kusomea CPA na "udaktari wa upasuaji wa binadamu " ipi ni fani ngumu zaidi ? Iweje CPA kuipata inakuwa mbinde ?

Vyuo vyote nchini kwa mfano pale Mlimani ukiangalia idadi ya wanafunzi waliohitimu wakati chuo kinafunguliwa na mpaka sasa idadi ya wanafunzi waliohitimu imeongezeka na wamehitimu watu wengi zaidi, yaani maelfu kwa maelfu.
Lakini siyo kwa CPA ni miaka 50 sasa tangu tupate uhuru lakini walioipata hiyo CPA hawazidi elfu nne.

Nauliza hiivi, hii bodi imeundwa kwa ajili ya kuwaendeleza wahasibu au KUWAKANDAMIZA wahasibu ?

Naunga mkono hoja,unayosema ni ya kweli ni bora ukasome CPA ya somalia utaipata kuliko bongo
 
CPA sio lelemama, inahitaji m2 uelewe na sio kukariri. Vyuon unafaulu kwa kudesa, chabo n.k. Nbaa hivyo vipo hakuna. Yahitaji kuelewa zaid. Kaza buti utatoka tu. UDSM kuna Dr. Alikuwa anatufundisha accounting, Alipata Phd yake uganda, mpaka tunamaliza chuo hana CPA, Kila akikanyaga wanakula kichwa. Mbaya zaid dr, mwenzake (DR. ASSAD) head of account dept ndie chairman wa NBAA.
 
teh teh, duuuu, lakini tatizo la mitihani ya CPA,nadhani ni muda wa maandalizi ndio watu hawana.... otherwise wengine wanakurupukia mamboooo. Histolia inaonesha watu wengi walikuwa wanasoma masomo ya biashara walikuwa hawalipendi somo la hisabati, sasa ukienda kwenye hiyo degree za biashara lazima uzijue hizo hisabati vizuri, ni balaa kwako kwani utalazimika kutumia nguvu sana kuoma, tena kwenye CPA ndio kabisa hesabu lazima, sas huyu mtu asiyekuwa na msingi mzuri wa hesabu atafaulu vipi? utafiti kuna watu waliosoma engineering wakifanya CPA wanafanya kwa muda mfupi sana, ingawa wanafanya mitihani mingi zaidi....kabla ya kulalamika jiangalie uko kundi lipi?
 
ushindwe na ulegee
CPA huwezi kupata kama
- unasoma kwa kukariri
- ulifauli chuo kiujanja ujanja k.v kudesa
- mvivu wa kusoma vitabu
- unapania mtihani. unajifanya uko bize na CPA. umeacha kujirusha, hutaki kuangalia mpira, eti na pombe unaacha! n.k
- maktaba unapaona kama kituo cha polisi
After all ulilazimishwa kusoma uhasibu? kwa nini usingesoma sanaa au linguistic?

Nenda kapime akili yako nadhani huijui NBAA vizuri unachosema siyo kweli kabisa. Mfumo wa hao jamaa ni mbovu sana na ndio maana wanaopata hiyo CPA wanapata pass tu yaani C wakati vijana walifaulu vizuri vyuoni.Mbona NECTA watu wanapata Division 1 na wakati anayetunga mtihani siyo anayekufundisha.NBAA wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Board zingine za professionals hapa nchini ktk fani za udaktari, sheria, uhandisi n.k kwa kufanya hivyo watajua mapungufu yao.Pia waache tamaa ya pesa huwezi kutunga mtihani wakafaulu Less than 20% halafu ukajisifu wewe ni mtaalamu nadhani utakuwa na matatizo katika mfumo wako mzima wa usimamizi na utunzi wa mitihani.
 
Unataka CPA watu wapate kama MBA???? Pole sana...10 years????? mhh opportunity cost ya kusoma hyo CPA mbona kubwa sana? uneanza degree ingine kama Economics ungekuta umeshamaliza na Master juu
 
Kwa maoni yangu CPA Exams zinataka mtu uwe kwanza na background nzuri ya uhasibu. Wewe kama chuo chako kimekuparaza tu kwenye uhasibu, then itakubidi uweke efforts zaidi ya wale waliobahatika kuivishwa vizuri. Mfano ni masomo kama auditing, financial, tax, entrepreneurship na managerial kwa miaka hiyo yalikuwa ni afadhali kwa wanafunzi wa mlimani kama wakiweka nguvu kwa sababu walikuwa na waalimu wazuri wa hayo masomo. Wakati the same mlimani students walikuwa na wakati mgumu kwenye International finance kwani ilikuwa ni optional subject kwa B.Com Accounting students (ingawa kuna Dr. Minja pale na ni mzuri) hali wanafunzi wa Mzumbe wao walikuwa ni mteremko kwenye International Finance (kwao ni compulsory) na mlima kwa hayo mengine. Kwa hiyo in short, college uliyotoka pia ni determinant namba 2 huku juhudi zako zikiwa ni determinant namba 1. Ndio maana ilikuwa kwa miaka mingi sana best students walikuwa wanatoka mlimani na mlimani kilikuwa ni chuo kinachoongoza kwa graduates wake kufaulu bodi; ukichunguza factor ya chuo ilichangia sana. Ila pia narudia tena, juhudi zako zina mchango mkubwa sana hata kama chuo ulichotoka kinamilikiwa na NBAA; sema tu chuo kitakupa urahisi au exposure ya vitu vingi kwenye fani.

Kuhusu ACCA nahisi kwa wao watu wanahisi ni rahisi kwa sababu wanakupa study / exam kits ambazo ukikomaa nazo vizuri, unaweza toka. Wakati CPA ni kama NECTA vile...unakamua kwa urefu wa kamba yako.

Nakubali pia in general NBAA kuna mapungufu as walipaswa kuangalia sababu za watu kushindwa sana mitihani na hata kuweka taratibu za kuwaivisha wanafunzi kabla ya mitihani. Sasa unakuta CPA Review Classes kibao lakini kwangu mimi ni kama other tuition centres, ambapo watu kibao wanakuwa nazo isipokuwa tu kwa CPA kunakuwa na requirements.
 
teh teh, duuuu, lakini tatizo la mitihani ya CPA,nadhani ni muda wa maandalizi ndio watu hawana.... otherwise wengine wanakurupukia mamboooo. Histolia inaonesha watu wengi walikuwa wanasoma masomo ya biashara walikuwa hawalipendi somo la hisabati, sasa ukienda kwenye hiyo degree za biashara lazima uzijue hizo hisabati vizuri, ni balaa kwako kwani utalazimika kutumia nguvu sana kuoma, tena kwenye CPA ndio kabisa hesabu lazima, sas huyu mtu asiyekuwa na msingi mzuri wa hesabu atafaulu vipi? utafiti kuna watu waliosoma engineering wakifanya CPA wanafanya kwa muda mfupi sana, ingawa wanafanya mitihani mingi zaidi....kabla ya kulalamika jiangalie uko kundi lipi?

Ndugu; , huwezi ingia kwenye uhasibu kama hujui hesabu. ... lazima wakutolee dirishani.... mtu kwenye kutoa unaweka kujumlisha..... lazima wakushike shati..
 
CPA sio lelemama, inahitaji m2 uelewe na sio kukariri. Vyuon unafaulu kwa kudesa, chabo n.k. Nbaa hivyo vipo hakuna. Yahitaji kuelewa zaid. Kaza buti utatoka tu. UDSM kuna Dr. Alikuwa anatufundisha accounting, Alipata Phd yake uganda, mpaka tunamaliza chuo hana CPA, Kila akikanyaga wanakula kichwa. Mbaya zaid dr, mwenzake (DR. ASSAD) head of account dept ndie chairman wa NBAA.

Duuhh, jamaa namjua; sema sasa naye nahisi alikuwa anajiamini sana. Unajua bodi haitaki ujuaji wala CV, inataka majibu kwenye mitihani. Ukileta 'you know nimekuwa mhasibu au mwalimu kwa miaka 40' - wao wanakula kichwa. Tena alianza toka kipindi Dr. Temu alikuwa anaishikilia NBAA....
 
SIZITAKI MBICHI HIZI

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
mkuu umenikumbusha mbaaaali sana. nitaiweka hii post kwenye maktaba yangu. Sizitaki mbichi hizi darasa la tatu! Naomba uni pm na Karudi Baba Mmoja toka Safari ya Mbali!

Wakuu CPA inataka uvumilivu na kujituma si suala la kufaulu tu manake ile kitu inaitwa profession sasa ukiamua kwamba msafara wa mamba na kenge wawemo itakuwa hatari. Jamani mkijitima na kusoma kwa bidii mtaipata hiyo CPA. Siku hizi kina Masters za kupeana tu huwezi kulinganisha na CPA ninavyosikia. Hakika kwa kweli kuna watu ambao wamesoma hiyo CPA kwa mika zaidi ya 15 lakini nijuavyo mimi ili ufaulu CPA siyo ukariri bali ujue na kuelewa masomo!
 
mkuu umenikumbusha mbali sana, kipindi nipo ATECII kuna jamaa alikuwa mkali sana wa accounts akawa anatufundisha sisi tuilotoka PCB apo alikuwa kakamatwa ilo somo kama mara 4 hivi na akitoa presentation sote tunamkubali lakini paper ikifika tuu anakamatwa yan sisi tulikuwa tunashangaa sana. mpaka tumefika module D ndo jamaa anakamilisha ilo somo la accounts ATECII.

SO SIJUI KUNA NINI APO. SABABU JAMAA ALIKUWA KICHWA BALAA CHA ACCOUNTS.

Examination techniques...!!! Watu kama hao wakizikosa utakuta wanakomaa na swali la accounts mpaka li-balance. Wakati wengine wanakamua yote 5 bila hata moja ku-balance na wanakuwa wamekula 50% ya maksi kila swali. Yeye anakomaa na 100% ya maksi 20, lazima abaki. Halafu kingine ni ujuaji, anataka kuleta kujua kwenye professional exams, wakati huku wanataka uwe direct kwenye point ukianza history of accounting wakati swali limekwambia tengeneza financial statements, nani atakuwa muda wa kusoma historia.
 
CPA sio lelemama, inahitaji m2 uelewe na sio kukariri. Vyuon unafaulu kwa kudesa, chabo n.k. Nbaa hivyo vipo hakuna. Yahitaji kuelewa zaid. Kaza buti utatoka tu. UDSM kuna Dr. Alikuwa anatufundisha accounting, Alipata Phd yake uganda, mpaka tunamaliza chuo hana CPA, Kila akikanyaga wanakula kichwa. Mbaya zaid dr, mwenzake (DR. ASSAD) head of account dept ndie chairman wa NBAA.
Huyu ni Masudi?i maana nami nafahamu DR Assad ndio alikuwa Msimamizi wake kwa ajili ya PHD
 
Pole Mhasibu. Kuna utaratibu wa kukataa rufaa kama hujaridhika na matokeo. Jaribu Huo utakusaidia
 
kwani hizo cpa zina msaada wowote kwenye kupata kazi au kupata maisha mazuri.

kama basic university degree imeshindwa kukusaidia hata upate phd 10 na masterz zote. hautatoka kimaisha
 
kwani hizo cpa zina msaada wowote kwenye kupata kazi au kupata maisha mazuri.

kama basic university degree imeshindwa kukusaidia hata upate phd 10 na masterz zote. hautatoka kimaisha

zamani zilikuwa dili ila saiv ubabaishaji mwingi unaweza ukawa nayo ukaonekana kama katuni tu!
 
Jaribu ACCA kama CPA imekataa ili tujua ni NBAA wenye shida au ni ubongo wako umejaa kamasi
kama CPA (T) imekushinda,usijaribu ACCA,kule ni next level,na ukiingia dunia yeyote wanakutambua!
 
Niombe radhi haraka , hatupo hapa kwa ajili ya kutukanana. Haiwezekani mimi na Masters yangu uniambie hivyo. Embu niombe radhi haraka !
Masters?..hiyo vijanawanasoma mzumbe...wamenyoa kiduku,suruali iko chini ya takoalafu ana ndoto za kuwa executive ?CPA ina mashiko kuliko iyo masters kwa waasibu!
 
kama CPA (T) imekushinda,usijaribu ACCA,kule ni next level,na ukiingia dunia yeyote wanakutambua!

Mkuu idaz nimetoa ushauri tu kwa mtu anayeikandia bodi kuwa inatunga mitihani isiyojibika.......mimi karibu nitakuwa retired FCPA
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom