Nakusudia kuiburuza Sekretarieti ya Ajira (Utumishi) na Serikali Mahakamani

Inanda

Member
Dec 6, 2020
62
128
Kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani, Tanzania pia ilianzisha chombo cha kusimamia na kudhibiti taaluma ya uhasibu. Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ni Taasisi inayosajili na kusimamia Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu na kudhibiti taaluma ya Uhasibu nchini.

NBAA Ilianzishwa kwa sheria ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu sura ya 286 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002. Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ipo chini ya Wizara yenye dhamana ya fedha. Bodi ilianzishwa mwaka 1972 na kuanza kufanya kazi zake rasmi kuanzia tarehe 15 Januari 1973.

NBAA ndio chombo kinachotunga, kuendesha na kusimamia mitihani kwa wale wanaohitaji kuwa wataalamu wa uhasibu na wakaguzi wa hesabu yaani CPA na CPAPP. Masharti ya chini kujiunga ili kuanza kufanya mitihani ya NBAA (minimum entry requirements), inaruhusu Cheti cha mtihani wa elimu ya Sekondari (CSEE) chenye angalau ufaulu wa crediti tatu na kufaulu Hisabati na Lugha ya Kiingereza.

Mwenye hiki cheti ataanza kwa kufanya mitihani ya ATEC 1. Akifaulu, ataenda level ya pili ambayo ni ATEC 2. Akifaulu ataenda ngazi ya tatu ambayo ni Intermediate level, Akifaulu intermediate level ataenda ngazi ya mwisho ambayo inaitwa Final stage (Final level). Akifaulu hii ngazi ya mwisho ndio anatunukiwa cheti cha kuwa CPA(T).

Sasa acha nirudi kwenye hoja yangu ya msingi. Kuna vijana wengi huamua kusoma CPA baada tu ya kumaliza elimu ya secondary. Vijana hawa huwa wana CPA lakini hawana diploma wala bachelor’s degree. Tatizo linakuja kwenye ajira za serikali zinazoendeshwa na Secretariat ya Ajira (Utumishi).

Vijana hawa mara nyingi huwa hawaitwi kwenye usaili kwenye nafasi zinazohitaji sifa ya kuwa na degree au diploma. Na hata ikitokea wameitwa (hata sielewi kama huwa wanawaita kimakosa au kuna baadhi ya watendaji wa utumishi wana taarifa sahihi na wengine hawana) huwa wanazuiwa kuingia kwenye chumba cha usaili pale kwenye ukaguzi wa vyeti kwa sababu hawana degree.

Sasa huwa najiuliza inakuwaje serikali ianzishe mfumo wa kuruhusu watu wasome CPA kwa watu wenye elimu ya sekondari halafu inashindwa kuwatambua pale wanapohitimu hiyo taaluma ya CPA, au serikali inategemea hawa vijana waajiriwe na nani? Funny enough sector binafsi hazina longolongo kabisa na mtu mwenye CPA, Sector binafsi zinatambua umuhimu na thamani ya CPA ila serikali ambayo ndio mwanzilishi na msimamizi wa hii taaluma haiwatambui hawa vijana wenye CPA kwa sababu hawana degree.

Hili swala tumeshalilalamikia sana NBAA lakini NBAA majibu yao ni kwamba Utumishi huwa wanafanya makosa kuwazuia watu waliohitimu intermediate level kufanya usaili kwa wenye sifa ya kuwa na bachelor’s degree, maana yake ni kwamba intermediate level ni sawa na bachelor’s degree.

Nimekusudia kuiburuza serikali na utumishi mahakamani kwa hasara iliyonisababishia. Wanilipe gharama zangu zote za kusoma CPA. Haiwezekani waruhusu tusome CPA tukiwa na Elimu ya sekondari halafu watubague kwenye ajira. Wanategemea nani atuajiri wakati ni wao wenyewe ndio walianzisha huu mfumo?

Kwa nini wazidiwe kututhamini na kututambua na sector binafsi ambao hata sio walioanzisha huu mfumo? Walianzisha huu mfumo kwa ajili ya sector binafsi? Wao serikali ndio ilitakiwa wawe wa kwanza kututhamini kuliko hata sector binafsi.

Utumishi nawaburuza mahakamani kwa hoja hizi tatu:

1.Kunisababishia gharama za usafiri na malazi kwa kunishort list kwa ajili ya usaili lakini wananizuia kuingia kwenye chumba cha mtihani kwa sababu sina degree, kwa nini wanishortlist kama wanajua sina cheti cha degree?

2.Kuna wakati hata kwenye usaili hawaniiti kabisa kwa sababu sijaambatanisha cheti cha degree. Kama NBAA walishawataarifu kuwa intermediate level ni sawa na degree, kuwashitaki kwa kuniathiri kisaikolojia kwa nini hawaniiti kwenye usaili wakati cheti cha intermediate level nimeambatanisha.

3.Kuna nyakati unaweza ukamkuta msimamizi au mkagua vyeti akakuruhusu kuingia kwenye chumba cha usaili kwa hichohicho cheti cha intermediate level. Sasa mtu unabaki kujiuliza inakuwaje wakati mwingine wanakuruhusu na wakati mwingine wanakuzuia, je hii ina maana hili swala linajulikana kwa baadhi ya watendaji wa utumishi na baadhi hawalijui?

Na kama linajulikana kwa nini Utumishi isiwatangazie wafanyakazi wake wote kuwa intermediate level ni equivalent to degree ili kuondoa huu mkanganyiko? Hivyo napanga kuwashitaki utumishi kwa huu uzembe.

4. Cha mwisho nitaiomba mahakama iilazimishe serikali itoe tamko rasmi iuambie uma wa Watanzania kuwa hizi level za NBAA ni equivalent na nini kwenye level za elimu ya Tanzania.
 
Una hoja ya Msingi sana. Kuna haja ya Professional Bodies kukaa pamoja na Serikali kuoanisha Qualifications wanazozitoa na Mfumo wa Elimu unatambulika na serikali.

Kuna kesi iliwahi kutokea kwenye Taasisi moja Jamaa alikuwa na diploma akafanya mitihani ya Bodi akapata CPA. Alipomaliza akaomba kusoma Post graduate kwa kutumia CPA akapata na kumaliza.

Aliporudi kwa mwajiri kumuonesha cheti cha Post graduate ili abadlishiwe muundo wakamkatalia kwa kuwa hana cheti cha degree.

Swali likawa Chuo kilimruhusi vipi asome Post graduate kama hakuwa na sifa?

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
NBAA ni miyeyusho tu, naunga mkono kuishtaki Gov

Bodi zingine ili uruhusiwe kufanya mtihani ni lazima uwe umehitimu mafunzo husika ama ngazi ya Cheti, Diploma au Degree na kufaulu.

Hapo ukiwa na elimu ya Cheti unaruhusiwa tu kufanya mtihani wa ngazi ya cheti, na hakuna njia ya mkato kufanya mtihani wa ngazi inayofuata(Diploma) bila kuhitimu hiyo ngazi(Diploma).

Sasa nashangaa huu utaratibu wa NBAA wa kupitisha watu njia za panya hadi wanapata CPA bila kusoma ngazi ya Shahda.
 
Kwa hiyo walianzisha huu utaratibu ili hawa vijana waajiriwe na nani?
Hili ndio tatizo la mfumo wa elimu Tz. Kila mhitimu lengo lake la kwanza ni kuajiriwa.

Mfumo wa Elimu haumwandai mhitimu kuweza kujitegemea.
 
Kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani, Tanzania pia ilianzisha chombo cha kusimamia na kudhibiti taaluma ya uhasibu. Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ni Taasisi inayosajili na kusimamia Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu na kudhibiti taaluma ya Uhasibu nchini.

NBAA Ilianzishwa kwa sheria ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu sura ya 286 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002. Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ipo chini ya Wizara yenye dhamana ya fedha. Bodi ilianzishwa mwaka 1972 na kuanza kufanya kazi zake rasmi kuanzia tarehe 15 Januari 1973.

NBAA ndio chombo kinachotunga, kuendesha na kusimamia mitihani kwa wale wanaohitaji kuwa wataalamu wa uhasibu na wakaguzi wa hesabu yaani CPA na CPAPP. Masharti ya chini kujiunga ili kuanza kufanya mitihani ya NBAA (minimum entry requirements), inaruhusu Cheti cha mtihani wa elimu ya Sekondari (CSEE) chenye angalau ufaulu wa crediti tatu na kufaulu Hisabati na Lugha ya Kiingereza. Mwenye hiki cheti ataanza kwa kufanya mitihani ya ATEC 1. Akifaulu, ataenda level ya pili ambayo ni ATEC 2. Akifaulu ataenda ngazi ya tatu ambayo ni Intermediate level, Akifaulu intermediate level ataenda ngazi ya mwisho ambayo inaitwa Final stage (Final level). Akifaulu hii ngazi ya mwisho ndio anatunukiwa cheti cha kuwa CPA(T).

Sasa acha nirudi kwenye hoja yangu ya msingi. Kuna vijana wengi huamua kusoma CPA baada tu ya kumaliza elimu ya secondary. Vijana hawa huwa wana CPA lakini hawana diploma wala bachelor’s degree. Tatizo linakuja kwenye ajira za serikali zinazoendeshwa na Secretariat ya Ajira (Utumishi). Vijana hawa mara nyingi huwa hawaitwi kwenye usaili kwenye nafasi zinazohitaji sifa ya kuwa na degree au diploma. Na hata ikitokea wameitwa (hata sielewi kama huwa wanawaita kimakosa au kuna baadhi ya watendaji wa utumishi wana taarifa sahihi na wengine hawana) huwa wanazuiwa kuingia kwenye chumba cha usaili pale kwenye ukaguzi wa vyeti kwa sababu hawana degree. Sasa huwa najiuliza inakuwaje serikali ianzishe mfumo wa kuruhusu watu wasome CPA kwa watu wenye elimu ya sekondari halafu inashindwa kuwatambua pale wanapohitimu hiyo taaluma ya CPA, au serikali inategemea hawa vijana waajiriwe na nani? Funny enough sector binafsi hazina longolongo kabisa na mtu mwenye CPA, Sector binafsi zinatambua umuhimu na thamani ya CPA ila serikali ambayo ndio mwanzilishi na msimamizi wa hii taaluma haiwatambui hawa vijana wenye CPA kwa sababu hawana degree. Hili swala tumeshalilalamikia sana NBAA lakini NBAA majibu yao ni kwamba Utumishi huwa wanafanya makosa kuwazuia watu waliohitimu intermediate level kufanya usaili kwa wenye sifa ya kuwa na bachelor’s degree, maana yake ni kwamba intermediate level ni sawa na bachelor’s degree.

Nimekusudia kuiburuza serikali na utumishi mahakamani kwa hasara iliyonisababishia. Wanilipe gharama zangu zote za kusoma CPA. Haiwezekani waruhusu tusome CPA tukiwa na Elimu ya sekondari halafu watubague kwenye ajira. Wanategemea nani atuajiri wakati ni wao wenyewe ndio walianzisha huu mfumo? Kwa nini wazidiwe kututhamini na kututambua na sector binafsi ambao hata sio walioanzisha huu mfumo? Walianzisha huu mfumo kwa ajili ya sector binafsi? Wao serikali ndio ilitakiwa wawe wa kwanza kututhamini kuliko hata sector binafsi.

Utumishi nawaburuza mahakamani kwa hoja hizi tatu:
1.Kunisababishia gharama za usafiri na malazi kwa kunishort list kwa ajili ya usaili lakini wananizuia kuingia kwenye chumba cha mtihani kwa sababu sina degree, kwa nini wanishortlist kama wanajua sina cheti cha degree?

2.Kuna wakati hata kwenye usaili hawaniiti kabisa kwa sababu sijaambatanisha cheti cha degree. Kama NBAA walishawataarifu kuwa intermediate level ni sawa na degree, kuwashitaki kwa kuniathiri kisaikolojia kwa nini hawaniiti kwenye usaili wakati cheti cha intermediate level nimeambatanisha.

3.Kuna nyakati unaweza ukamkuta msimamizi au mkagua vyeti akakuruhusu kuingia kwenye chumba cha usaili kwa hichohicho cheti cha intermediate level. Sasa mtu unabaki kujiuliza inakuwaje wakati mwingine wanakuruhusu na wakati mwingine wanakuzuia, je hii ina maana hili swala linajulikana kwa baadhi ya watendaji wa utumishi na baadhi hawalijui? Na kama linajulikana kwa nini Utumishi isiwatangazie wafanyakazi wake wote kuwa intermediate level ni equivalent to degree ili kuondoa huu mkanganyiko? Hivyo napanga kuwashitaki utumishi kwa huu uzembe.

4. Cha mwisho nitaiomba mahakama iilazimishe serikali itoe tamko rasmi iuambie uma wa Watanzania kuwa hizi level za NBAA ni equivalent na nini kwenye level za elimu ya Tanzania.
Kuondoa mzizi wa fitna soma degree kwanza ni kwa faida yakp mwenyewe,hata mm kama muajiri naprefer mtu mwenye kitu cha ziada Mwenye CPA na na mwenye kuongeza na kadegree atanifaa zaidi!!
 
Shida sio kusoma degree kwanza. Kwani wangeweka kigezo cha degree kama minimum entry ya cpa nani angelaumu?

Shida ni kwa nini serikali ilianzisha kitu hiki. Jaribu kuwa mwelewa unaposoma kitu.
 
Una hoja ya Msingi sana. Kuna haja ya Professional Bodies kukaa pamoja na Serikali kuoanisha Qualifications wanazozitoa na Mfumo wa Elimu unatambulika na serikali.

Kuna kesi iliwahi kutokea kwenye Taasisi moja Jamaa alikuwa na diploma akafanya mitihani ya Bodi akapata CPA. Alipomaliza akaomba kusoma Post graduate kwa kutumia CPA akapata na kumaliza.

Aliporudi kwa mwajiri kumuonesha cheti cha Post graduate ili abadlishiwe muundo wakamkatalia kwa kuwa hana cheti cha degree.

Swali likawa Chuo kilimruhusi vipi asome Post graduate kama hakuwa na sifa?

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
Serikali ya Tanzania inasikitisha sana. Yaani hakuna harmonization kabisa. Taasisi za serikali kama vile hazina maelewano.
 
Kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani, Tanzania pia ilianzisha chombo cha kusimamia na kudhibiti taaluma ya uhasibu. Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ni Taasisi inayosajili na kusimamia Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu na kudhibiti taaluma ya Uhasibu nchini.

NBAA Ilianzishwa kwa sheria ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu sura ya 286 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002. Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ipo chini ya Wizara yenye dhamana ya fedha. Bodi ilianzishwa mwaka 1972 na kuanza kufanya kazi zake rasmi kuanzia tarehe 15 Januari 1973.

NBAA ndio chombo kinachotunga, kuendesha na kusimamia mitihani kwa wale wanaohitaji kuwa wataalamu wa uhasibu na wakaguzi wa hesabu yaani CPA na CPAPP. Masharti ya chini kujiunga ili kuanza kufanya mitihani ya NBAA (minimum entry requirements), inaruhusu Cheti cha mtihani wa elimu ya Sekondari (CSEE) chenye angalau ufaulu wa crediti tatu na kufaulu Hisabati na Lugha ya Kiingereza. Mwenye hiki cheti ataanza kwa kufanya mitihani ya ATEC 1. Akifaulu, ataenda level ya pili ambayo ni ATEC 2. Akifaulu ataenda ngazi ya tatu ambayo ni Intermediate level, Akifaulu intermediate level ataenda ngazi ya mwisho ambayo inaitwa Final stage (Final level). Akifaulu hii ngazi ya mwisho ndio anatunukiwa cheti cha kuwa CPA(T).

Sasa acha nirudi kwenye hoja yangu ya msingi. Kuna vijana wengi huamua kusoma CPA baada tu ya kumaliza elimu ya secondary. Vijana hawa huwa wana CPA lakini hawana diploma wala bachelor’s degree. Tatizo linakuja kwenye ajira za serikali zinazoendeshwa na Secretariat ya Ajira (Utumishi). Vijana hawa mara nyingi huwa hawaitwi kwenye usaili kwenye nafasi zinazohitaji sifa ya kuwa na degree au diploma. Na hata ikitokea wameitwa (hata sielewi kama huwa wanawaita kimakosa au kuna baadhi ya watendaji wa utumishi wana taarifa sahihi na wengine hawana) huwa wanazuiwa kuingia kwenye chumba cha usaili pale kwenye ukaguzi wa vyeti kwa sababu hawana degree. Sasa huwa najiuliza inakuwaje serikali ianzishe mfumo wa kuruhusu watu wasome CPA kwa watu wenye elimu ya sekondari halafu inashindwa kuwatambua pale wanapohitimu hiyo taaluma ya CPA, au serikali inategemea hawa vijana waajiriwe na nani? Funny enough sector binafsi hazina longolongo kabisa na mtu mwenye CPA, Sector binafsi zinatambua umuhimu na thamani ya CPA ila serikali ambayo ndio mwanzilishi na msimamizi wa hii taaluma haiwatambui hawa vijana wenye CPA kwa sababu hawana degree. Hili swala tumeshalilalamikia sana NBAA lakini NBAA majibu yao ni kwamba Utumishi huwa wanafanya makosa kuwazuia watu waliohitimu intermediate level kufanya usaili kwa wenye sifa ya kuwa na bachelor’s degree, maana yake ni kwamba intermediate level ni sawa na bachelor’s degree.

Nimekusudia kuiburuza serikali na utumishi mahakamani kwa hasara iliyonisababishia. Wanilipe gharama zangu zote za kusoma CPA. Haiwezekani waruhusu tusome CPA tukiwa na Elimu ya sekondari halafu watubague kwenye ajira. Wanategemea nani atuajiri wakati ni wao wenyewe ndio walianzisha huu mfumo? Kwa nini wazidiwe kututhamini na kututambua na sector binafsi ambao hata sio walioanzisha huu mfumo? Walianzisha huu mfumo kwa ajili ya sector binafsi? Wao serikali ndio ilitakiwa wawe wa kwanza kututhamini kuliko hata sector binafsi.

Utumishi nawaburuza mahakamani kwa hoja hizi tatu:
1.Kunisababishia gharama za usafiri na malazi kwa kunishort list kwa ajili ya usaili lakini wananizuia kuingia kwenye chumba cha mtihani kwa sababu sina degree, kwa nini wanishortlist kama wanajua sina cheti cha degree?

2.Kuna wakati hata kwenye usaili hawaniiti kabisa kwa sababu sijaambatanisha cheti cha degree. Kama NBAA walishawataarifu kuwa intermediate level ni sawa na degree, kuwashitaki kwa kuniathiri kisaikolojia kwa nini hawaniiti kwenye usaili wakati cheti cha intermediate level nimeambatanisha.

3.Kuna nyakati unaweza ukamkuta msimamizi au mkagua vyeti akakuruhusu kuingia kwenye chumba cha usaili kwa hichohicho cheti cha intermediate level. Sasa mtu unabaki kujiuliza inakuwaje wakati mwingine wanakuruhusu na wakati mwingine wanakuzuia, je hii ina maana hili swala linajulikana kwa baadhi ya watendaji wa utumishi na baadhi hawalijui? Na kama linajulikana kwa nini Utumishi isiwatangazie wafanyakazi wake wote kuwa intermediate level ni equivalent to degree ili kuondoa huu mkanganyiko? Hivyo napanga kuwashitaki utumishi kwa huu uzembe.

4. Cha mwisho nitaiomba mahakama iilazimishe serikali itoe tamko rasmi iuambie uma wa Watanzania kuwa hizi level za NBAA ni equivalent na nini kwenye level za elimu ya Tanzania.
Cha kushangaza utumishi wanatambua ATEC II ni sawa na diploma na hawana tatizo kabisa.inapofika kwenye Intermidiate sijui wana changanyikiwa nini?
 
Back
Top Bottom