NBAA haijaundwa kuendeleza wahasibu bali kuwadidimiza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NBAA haijaundwa kuendeleza wahasibu bali kuwadidimiza

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MHASIBU HALISI, Dec 5, 2011.

 1. MHASIBU HALISI

  MHASIBU HALISI Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ndugu watanzania na wahasibu wenzangu , napenda kuchukua nafasi hii adimu kwa kueleza kilio changu kuhusu hii bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu Tanzania (NBAA).

  kWA KWELI BODI HII IMEUNDWA SI KWA LENGO LA KUENDELEZA WAHASIBU BALI KUWADIDIMIZA NA KUWAKANDAMIZA KABISA WASIWE WENGI KATIKA NCHI HII.

  Wewe embu fikiria, mtu anafanya mitihani ya Module F kwa miaka kumi (10) na hapati hiyo CPA. Unafikiria nini hapa ?
  Mwengine anakuja kupata hiyo CPA amebakisha miaka mitano tu ili astaafu. Hivi hii CPA maana yake nini ? Hivi watu wanaisoma CPA ili waende kuitumia Duniani au kuitumia kaburini? Sasa iweje kuipata kwake iwe mbinde ?

  Tangu NBAA ianzishwe mwaka 1972 walioipata hawavuki watu elfu nne(4,000) hii ni pamoja na walioipata na tayari wameshakufa. Hivi kusomea CPA na "udaktari wa upasuaji wa binadamu " ipi ni fani ngumu zaidi ? Iweje CPA kuipata inakuwa mbinde ?

  Vyuo vyote nchini kwa mfano pale Mlimani ukiangalia idadi ya wanafunzi waliohitimu wakati chuo kinafunguliwa na mpaka sasa idadi ya wanafunzi waliohitimu imeongezeka na wamehitimu watu wengi zaidi, yaani maelfu kwa maelfu.
  Lakini siyo kwa CPA ni miaka 50 sasa tangu tupate uhuru lakini walioipata hiyo CPA hawazidi elfu nne.

  Nauliza hiivi, hii bodi imeundwa kwa ajili ya kuwaendeleza wahasibu au KUWAKANDAMIZA wahasibu ?
   
 2. Kilimo

  Kilimo JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Naungana nawe kwa hicho kilio, ila pls inabidi tuiobserve NBAA kwanza kabla ya kulalamika maana ukiwauliza NBAA wanaweza kusema watahiniwa hawana concentration ktk kusoma na kujiandaa kwao kwa mitihani na hata hiyo NBAA inaweza kudai kuwa haihusiki na Review classes zinazotolewa kwa wanaojiandaa kufanya hiyo mitihani ya CPA, with these answers from NBAA its likely to graduate many students from any college because the one who instruct or provide lectures to students is the one who engage with exermining the candidates/students compared to NBAA, the one who exermines students, NBAA, is not the one who provide the tuitions to the students.

  Lets wait the time when them, NBAA, will start providing tuition !
   
 3. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bora na wewe umeliona hilo, mimi mwenzako nilishagundua mapema ya kwamba Tanzania kuna aina mpya ya UTUMWA kupitia nyanja za elimu. Yaani wanaifanya elimu iwe ngumu bila ya sababu yoyote, lengo ni kwamba waliosoma hawataki wengine nao wafike pale walipo wao. Ni sawa na viongozi wa siasa za bongo, hawataki wengine waje kutawala.

  Pale NBAA wenyewe wanatoka vitambi na kundesha magari ya kifahari, tena wanaingia kazini saa tatu na kutoka saa nane. Ikishafika saa nane mchana huwezi kupata huduma yoyote pale. Wana pesa za kumwaga tena za kutosha hasa, si wanajua tu, yakwamba hata ukifanya mitihani yao mara mia mbili hupati CPA ng'o ! Wewe watakulia pesa zako tu , basi.

  Kuna Kaka yangu mmoja alikuwa anasomea hiyo CPA mpaka alikuwa anaweka miguu katika ndoo ya maji baridi kwa muda wa miaka saba mfululizo lakini hajaipata hiyo CPA ng'ooo! Halafu cha ajabu hiyo NBAA yenyewe inashuhulika na maswala ya utoaji elimu na utungaji wa mitihani. Lakini haipo chini ya wizara ya elimu na hiyo mitihani inatungwa tu na watu tena hakuna mtu hata mmoja pale mwenye taaluma ya ualimu. Yaani hii fani ya kufundisha hapa bongo imevamiwa tu. Kila mtu anifanya bila kujua code of ethics zake. Tanzania ni nchi ya ajabu sana.

  Inafikia mahali mtu ukimwambia una CPA , anakuona kana kwamba ni malaika msaidizi wa Mungu. Mipango na malengo ya hii bodi itazamwe upya. Mimi niona kama ni mradi tu wa wakubwa kwa ajili ya kujipatia pesa za bure !

  Vilevile nimegundua kitu kingine ya kwamba hapa Tanzania kwa kupitia hiyo NBAA wameanzisha aina mpya ya UTUMWA . Ambapo mtu anaweza kusoma hadi kufa kwake , kisa eti CPA ! Loooh Bongo ni noma !
  Wizara ya elimu mpo wapi ?
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  hili bandiko lako hapa sio mahali pake. Wakianza wa bodi ya bar maids, bodi ya wakandarasi, bodi ya wauza mawese nao kuleta malalamiko yao jukwaa hili litakosa maana.
   
 5. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  sababu za kufeli ziko wazi na ni nyingi sana! Mi ninayo na nilifanya mtihani mara 3. Wapo wanaofanya mtihani mara 1 module E na F na wanafaulu! Utasingizia nbaa bure tu!, kaulize kama ACCA ni rahisi! Ningeandika mengi zaidi ila natumia simu!, kesho nitakupa mambo kwa urefu na mapana!
   
 6. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mimi naona kuna mapungufu kwenye hizi hoja zako ambazo nimezi-bold na kuziwekea namba:-
  Tukianza na hoja yako namba moja mimi naona si kweli. Kwa maana mbona watu wanasoma MASTERS tena online na wanagraduate ? Iweje kwa CPA tu ndo watu hawana concertration kwa miaka saba ? Hivi ni kweli mtu anaweza kulipa pesa yake tena ni Fresh mrom College halafu akawa hana concertation ? Sio kwamba NBAA ndo wanaobana wakusudikally ?

  Hoja yako ya pili nayo si kweli, NBAA ndo hutoa vibali kwa Tuition Providers wote hapa nchini. Ndio maana ukienda kujisajili kwa ajili ya mitihani, lazima fomu yako iwe na muhuri wa Tuition Provider wanaomtumbua wao NBAA. ILa cha ajabu aslimia 99.9 ya wanaofundisha wote hawana taaluma ya ualimu wala leseni ya kufundisha kutoka Wizara ya Elimu.

  Hoja yako ya tatu naona nayo haijakaa sawa, kwa maana kuna watu wanasoma Tanzania lakini mitihani wanafanya ya kutoka ulaya na wanafaulu vizuri tu kwa muda mfupi tu. Ila sio hapa NBAA wataalamu wa kugeuza watanzania wawe WATUMWA wa elimu. Unasoma miaka saba , unatoka bila bila ! Na ningeipata hiyo CPA ningejiita msaidizi wa Mungu ! Yaani duuuh, Bongo ni noma !
   
 7. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Eheeeee umenikumbusha kitu, hiyo ACCA kwa taarifa yako ndo rahisi kweli basi tu watu wanashindwa kuifanya kwa sababu ya ukosefu wa pesa hizo paund za uingereza. Hiyo bodi ya ACCA inaruhusu mtu kusoma somo moja moja tena uikfaulu hata somo moja wanarecord. Wadosi kibao wanasoma hiyo ACCA .

  Cha ajabu hapa Tanzania kupitia hiyo NBAA lazima ufanye masomo matatu na ukifaulu somo moja , basi wanafuta yote . Yaani unaanza upiya mpaka ufaulu yote au mawili. kwa nini ukifaulu somo moja hawalihesabu wakati umetumia resouces zako mpaka umefaulu hilo somo ?

  Nasema hivi NBAA ni UTUMWA wa elimu !
   
 8. K

  Kacharimbe JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ushindwe na ulegee
  CPA huwezi kupata kama
  - unasoma kwa kukariri
  - ulifauli chuo kiujanja ujanja k.v kudesa
  - mvivu wa kusoma vitabu
  - unapania mtihani. unajifanya uko bize na CPA. umeacha kujirusha, hutaki kuangalia mpira, eti na pombe unaacha! n.k
  - maktaba unapaona kama kituo cha polisi
  After all ulilazimishwa kusoma uhasibu? kwa nini usingesoma sanaa au linguistic?
   
 9. n

  nyantella JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  1) hapo kwenye red kama mika kumi unafanya mitihani hupati CPA, wewe ni kilaza period!
  2) hapo kweney green, see 1) above
  3) hapo buluu, kwani lazima upate CPA? tafuta kitu ingine nafanana na hiyo!! acha kulalama mkubwa wewe sasa lol!
   
 10. M

  Mukubwa Senior Member

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 124
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Huu utaratibu wa mitahani ya bodi unasumbua kila mahali: kusajiri wahandisi ni soo pia, hata school of law watu hufanya mitaihani kwa mda mrefu kabla ya kupasishwa kuwa mawakili.
   
 12. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa. Wamewageuza shamba la bibi. Wanawavuna tu.
   
 14. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yaani unasomea CPA kwa miaka 10 bila mafanikio? You would have been better off kama ungekuwa unauza vitunguu. Tuache visingizio na kutaka vitu kwa njia za mkato. NBAA wana syllabus ya masomo yao na mitihani inatungwa from within the syllabus. Tatizo la wanafunzi wanasoma kwa kuegesha, na wamezoea kupewa maswali na waalimu wao vyuoni. Pia ni wavivu wa kusoma vitabu.

  Kuhusu ACCA kuwa rahisi lazima muelewe kuwa hawa jamaa wamekaa kibiashara zaidi ingawa mitihani yao pia ipo kwenye standard nzuri tuu. Kuruhusu watu wafanye mtihani mmoja mmoja kumepunguza ugumu wa kupata hiyo ACCA but again ukifanya mtihani mmoja mmoja utamaliza lini hiyo ACCA? ACCA wameamua kurahisisha upatikanaji wake baada ya kuona watu wengi wanaacha kufanya mitihani yao (Wakati wetu ACCA ilibidi ufaulu paper 3 za mwisho in one sitting otherwise wanafuta matokeo yote and you have to sit the papers again).

  Looking at the standard of questions between ACCA and CPA hakuna tofauti kubwa hivyo the fact that watu wanashindwa kupata CPA katika muda muafaka can be down to lack of good preparation and lack of concentration.
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  when....?
   
 16. MHASIBU HALISI

  MHASIBU HALISI Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ndo maana mimi nikasema hivi , katika tafiti zangu nimegundua kwa hapa Tanzania kuna aina mpya ya UTUMWA katika elimu !

  Kuwa na CPA haimaanishi kuwa wewe unajua kila kitu katika maswala ya uhasibu. CPA ni daraja tu, katika madaraja mengi ya elimu.Iweje kuipata kwake iwe mbinde ? Halafu kusomea CPA hakuna mikopo. Maana yake ni kwamba CPA ni moja kati ya vyanzo vya kuleta umasikini. Kwa maana ya kwamba, Resources nyingi mtu anatumia , halafu Work done is equal to zero !
   
 17. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Jaribu ACCA kama CPA imekataa ili tujua ni NBAA wenye shida.
   
 18. MHASIBU HALISI

  MHASIBU HALISI Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Niombe radhi haraka , hatupo hapa kwa ajili ya kutukanana. Haiwezekani mimi na Masters yangu uniambie hivyo. Embu niombe radhi haraka !
   
 19. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Endelea kusoma tu ndugu yangu, utaipata CPA siku moja. Nimewaona waliojiandaa vizuri wakifaulu na wengine wakifeli. Unajua tatizo ni kwamba vyuoni watu hufaulu kwa kuzima moto. Full kukariri hasa kama hujawahi kusoma masomo ya biashara sekondari.
  Kama hujaipata CPA usife moyo, kaza buti na isome kwa kuipenda na kuilewa.
  Unajua CPA/ACCA ni professional qualification exams wakati chuoni ni academic qualification exams. Sasa ukiwa unatumia style zile zile za chuo na ukaona hufanikiwi, badilisha style (Ila wengine wanakomaa na wanafanikiwa).
  Nadhani NBBA waendelee kufanya kazi yao ila wawe fair.
   
 20. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  mkuu umenikumbusha mbali sana, kipindi nipo ATECII kuna jamaa alikuwa mkali sana wa accounts akawa anatufundisha sisi tuilotoka PCB apo alikuwa kakamatwa ilo somo kama mara 4 hivi na akitoa presentation sote tunamkubali lakini paper ikifika tuu anakamatwa yan sisi tulikuwa tunashangaa sana. mpaka tumefika module D ndo jamaa anakamilisha ilo somo la accounts ATECII.

  SO SIJUI KUNA NINI APO. SABABU JAMAA ALIKUWA KICHWA BALAA CHA ACCOUNTS.
   
Loading...