Nawezaje kuwa Usalama wa Taifa?

Tafuta mshati wa kijani na lile kofia la kijani alafu uwe unavaa kila siku apo automatiki utakuwa ushakuwa usalama wa taifa
 
Mimi binafsi mjii ninao ishi 70% wanajua kabisa kwamba Ni A/usalama kabisa,
Licha ya kuwa na kazi yangu japo sio rasimi jamii inajua hivyo
Lakini pia hata akili yangu yani MINDSET yangu inaniaminisha kuwa mimi Ni usalama wa Taifa,

Kazi nyingne ninayo ifanya mimi Ni mwandishi wa habari wa kujitegemea so watu wanao niona Nikifanya shooting au recording mtaani ndo kabisa wanapitaga mbali na mimi,

Pamoja na hayo hii kazi naiweza sana maana nina uwezo wa kuongea na kila mtu hasa ninapo hitaji,
Naweza kuongea km mwandishi kumbe wakati huo huo nina chukua data,
Kitu kingine nina wadhifa flan kimakanisa so nahisi kazi hii ya usalama naiweza kwa asilimia 100.
Hivyo km kuna nafasi wasisite kuniita,
 
Narudia tena kusema ‘MFICHA MARADHI, KIFO HUMUUMBUA’

Habari za muda huu ndugu zangu, waungwana wenzangu. BIla shaka afya zenu ni njema na mnaendelea vema kabisa na majukumu ya kulijenga taifa letu la Tanzania.

HONGERENI SANA
  • Waswahili walisema “Mficha maradhi, mauti humuumbua”
Kauli hii ina maana kubwa sana, kama utakaa na kuitafakari utagundua ukweli wake. Kwani kama una dukuduku ambalo limekukwaza ama linakuumiza katika moyo ni vema ukalisema kwa wahusika ili huenda ukapata msaada ama ushauri juu ya jambo lako. Kwani ukiendelea kunyamaza unaweza kuathirika na hatimaye kupoteza Maisha na baada ya kufa kwako watu wakagundua tatizo lililokuuwa na watu kukulaumu (marehemu) huenda ungesema usingekufa.

AMA BAADA YA UTANGULIZI

Lengo la kuandika uzi huu wa heshima, napenda kuelezea dukuduku langu kwa umma huenda siku moja uzi huu ukasomwa na ambaye anaweza kulitatua tatizo langu na kupata ufumbuzi.

Nafikiri utakubaliana na mimi kuwa kila mtu katka Maisha yake huwa ana ndoto na kutamani awe mtu Fulani ama kufanya kazi Fulani, lakini mara nyingi ndoto hizo huishia kuwa ndoto tu na si halisi.

Natumia fursa hii nami kuelezea ndoto zangu ambazo nilikuwa, ninazo na nitakuwa nazo mpaka mwisho wa umri wangu.

Mimi nilitamani sana kufanya kazi katika idara ya USALAMA WA TAIFA

Ndio namaanisha usalama wa Taifa langu la Tanzania katika sekta yoyote ambayo wao watanipangia. Uzalendo ndicho hasa kilinifanya nipende kuwa katika kulitumikia na kulilinda Taifa langu kikamilifu.

Sikufanya jitihada zozote kwani sijui wapi naweza kupata suluhisho la hitaji langu, wala sikuwa / sina mtu ambaye ana uwezo wa kunifanikishia suala langu hili pendwa.

Leo nimeona niliweke wazi katika mtandao huu nambari moja hapa Tanzani najua baadhi ya wadau watakuwemo humu. Huenda wakanisaidia.

Najua baadhi yao watanibeza na kuongea maneno yasio na nidhamu, lakini hili kwangu nachukulia kama changamoto nyingine tu za kimaisha.

Naipenda TANZANIA, Nawapenda Watanzania,

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Kwa maswali Zaidi unaweza kuja PM
Usikute muanzisha mada ni TEETH sema anataka kukamata wavujisha siri.
 
Labda nikuweke sawa kwamba usalama wa taifa huanza kwenye jamii yako,je ulisha wahi kujitolea kuwa sungusungu pasipo kusukumwa au kuteuliwa na mjumbe? tuanzie hapo,maana kuwa usalama maana yake ni kuharifu au kutoa taharifa kwa vyombo vya ulinzi kama kuna watuhumiwa mtaani kwako,au we unataka kazi ya usalama wa msafara wa raisi?
 
Back
Top Bottom