Nawezaje kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?!

Nimesema ukifeli sio ukijifelisha!! yaan nimechukulia kwamba utakuwa umejishikiza mahali, lakini pia una ujasiriamali wako unafanya hivyo balance ya mambo yote matatu impact inaweza kuwa kubwa kwenye Masomo kuliko hayo mambo mengine mawili.
hivyo kufeli ni incase isiwe nia yako.

Kwa maelezo yako ni kwamba mzee anapendz uje kujiajiri baada ya Kusoma phamarcy wewe unataka Kujiajiri kabla; Hivyo wewe na mzee wako mna common Interest isipokuwa kwa muda tofauti hivyo kumwin kwa kitu nilichokwambia ni rahisi sana.
Sawa mkuu Asante sana.
 
Tabia za mzee wako siyo tabia za mababa Kama angekua baba ingekua ameshakutimuaga hapo nyumbani siku nyingi sahivi unakula mlo mmoja kwa siku na maji mingi had msosi unaogelea tumboni ila dingi yako anatabia za Daddy hata ufikishe miaka 60 bado atakuona mtoto tu na atakupa kila kitu

Yani kwa kifupi si unamjua Le mutuz? Eeeh dingi yako anakuandaa kuwa Le mutuz katoboa miaka 60 ila bado mtoto yuko kwa baba
 
Ukimaliza iyoo kozi tafuta kazi alafu simamia ndoto zako Mimi Mzee alitaka nisome famasia Ila Mungu alinipa kazi mapema nikaachana na wazo lake alipiga kelele Ila ndyo nilishaamua cha Kwanza toka Kwanza mikononi mwake ujipangie ndoto zako bila kutegemea pesa yake
 
Ukimaliza iyoo kozi tafuta kazi alafu simamia ndoto zako Mimi Mzee alitaka nisome famasia Ila Mungu alinipa kazi mapema nikaachana na wazo lake alipiga kelele Ila ndyo nilishaamua cha Kwanza toka Kwanza mikononi mwake ujipangie ndoto zako bila kutegemea pesa yake
Vizuri sana mkuu Asante sana Kwa ushauri na Hamasa
 
Kwan kuwa na duka la dawa sio ujasiriamali? Mbona mzee kakushaur kitu kizur au kwako wewe biashara lazima iwe duka la nguo
 
Kijana huhitaji kusomea Pharmacy ili uweze kufanya biashara ya Pharmacy, Ili uweze kufanya biashara ya Pharmacy unachohitaji ni hela tu, hapo Baba anataka kukupeleka mchomo, Komaa na msimamo wako mkuu Dunia ya sasa bila ya kukipigania unachokitaka au kukiamini utaishia pabaya sana. Mimi ni mhanga mkubwa wa hayo.
 
Issue ni kurudi Tena chuo miaka mingine mitatu kitu ambacho siko tayari kufanya.
Kwan kuwa na duka la dawa sio ujasiriamali? Mbona mzee kakushaur kitu kizur au kwako wewe biashara lazima iwe duka la nguo
 
Kijana huhitaji kusomea Pharmacy ili uweze kufanya biashara ya Pharmacy, Ili uweze kufanya biashara ya Pharmacy unachohitaji ni hela tu, hapo Baba anataka kukupeleka mchomo, Komaa na msimamo wako mkuu Dunia ya sasa bila ya kukipigania unachokitaka au kukiamini utaishia pabaya sana. Mimi ni mhanga mkubwa wa hayo.
Pole sana mkuu.
Lakini Bado una nafasi ya kufanya kile unahitaji
 
Naoam
Habari zenu Wana Jamiiforums.
Mimi ni kijana ambaye umri wangu upo kwenye mid 20's.

Nipo chuo kimoja hapa nchini ambapo nasomea kozi ya uuguzi.

Nia na madhumuni ya kuleta Uzi huu ni kuomba ushauri kuhusu ni jinsi Gani ninaweza kushikilia msimamo wangu kuhusu Nini nataka kwenye maisha yangu bila kuwafanya wazazi wahisi kama nimewadharau.
Iko hivi...

Baba yangu ndiye anayenisomesha mpaka sasa, hivi karibuni nilipokuwa likizo ya kumaliza mwaka wa pili kuingia mwaka wa tatu wa masomo hapa chuoni Mzee wangu alinishauri kwamba nikimaliza kozi Hii ya nursing (diploma) nirudi Tena chuo kusomea Tena kozi ya pharmacy miaka mingine mitatu (diploma). Hoja yake ni kwamba nikifanya hivyo baadaye naweza kujiajiri Kwa kufungua pharmacy yangu Mimi mwenyewe na kwamba pharmacy ni biashara inayolipa vizuri sana.

Lakini Mimi binafsi Kwa upande wangu siko tayari kufanya hivyo kwasababu malengo niliyojiwekea Mimi ni kwamba baada ya kumaliza hii diploma ya nursing nitafute ajira inishikize Kwa miaka kadhaa huku nikiwa nafanya shughuli za ujasiriamali pembeni Kisha biashara zikiwa nzuri na nikiona Nina kipato Cha kueleweka niachane kabisa na ajira ya uuguzi nijikite Moja Kwa Moja katika biashara kwasababu moyoni mwangu nawiwa kuwa mjasiriamali mkubwa tu, Maana hata hii kozi ya uuguzi ninayosomea sasahivi sikuitaka kabisa, nilipomaliza kidato Cha nne nilitaka nikasome business administration au kozi za masuala ya entrepreneurship Ili baadaye niweze kujiajiri katika biashara na ujasiriamali kwani ndoto zangu ni kumiliki kampuni yangu binafsi. Lakini Mzee wangu alipinga vikali wazo hili akisisitiza kuwa kozi za biashara hazina tija na wapo wengi wanaozunguka mitaani na vyeti vyao bila ajira miaka nenda Rudi na Wana degree kabisa.

Nilijaribu sana kumwelewesha kwamba lengo langu si kutafuta ajira Bali ni kujiajiri mwenyewe kutokana na elimu nitakayopata lakini hakukubaliana kabisa na Mimi.

Baadaye akanitafutia vyuo vya afya na kufanikiwa kupata nafasi katika kozi Hii ya uuguzi chuo Fulani hapa nchini na Mimi Kwa kuepuka kumkwaza nikakubali kuja kusoma japo haikuwa passion yangu kabisa!

Sasa kinachofanya nije kuomba ushauri ni hiki...

Mzee wangu ni mtu ambaye anataka akiongea kitu basi ufanye kama alivyokwambia yeye, ukitaka kufanya tofauti anakuona kama mbishi, unampuuza au unamdharau!

Of course Baba yangu ni mtu mmoja mzuri sana kwasababu ana upendo wa ajabu Kwa wanae yupo tayari kufanya chochote na ku sacrifice Kila kitu Ili kutupatia kile ambacho yeye anaamini kuwa ni Bora katika maisha ni mtu mwenye upendo wa ajabu sana na familia yake na watoto wake na Kwa Hilo nimemfanya kuwa role model wangu. Shida yake ndio hiyo Moja hataki uende tofauti na anavyotaka yeye.

Mimi Kwa upande wangu siamini kama kusoma saaana ndio kufanikiwa na ninataka nikimaliza hii diploma nianze kupambana na maisha sasa lakini yeye anasisitiza kuwa diploma ni level ndogo sana Kwa maisha ya sasa.

Of course inaweza kuwa kweli lakini Mimi naamini katika ndoto zangu na malengo Yangu na sitaki Tena kuendelea kupoteza muda kukaa darasani maana umri unazidi kwenda Mimi sio wa kuendelea kumtegemea mzazi Tena lakini nikimwambia hataki kabisa kuelewa.

Sasa wanajamvi shida yangu ninaomba mnisaidie nitumie mbinu Gani kumwelewesha na kumshawishi Mzee wangu akubali Mimi nifuate kile nilichojipangia katika maisha yangu lakini bila kumkwaza na kumfanya ahisi kama nampuuza au kumdharau?

Nawapenda sana wazazi Wangu sitaki kuwakwaza lakini pia sitaki kunyimwa opportunity ya kupambania malengo niliyojiwekea katika maisha na natamani pia wazazi wanipe Uhuru wa kujiamulia ninachotaka katika maisha yangu pia!

Nimepanga nikirudi home nikazungumze nae kuhusu hili lakini nashindwa kujua nitumie mbinu Gani kumuelewesha Maana najua nikishikilia uamuzi wangu tunaweza kuishia kupishana kauli kitu ambacho sitaki kitokee kwani pamoja na hayo sitaki kumkwaza.

Sasa naombeni ushauri wadau ni vipi naweza kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?

Asanteni nawasilisha.
Naona mzazi anatka kutimiza ndoto zake kupitia kwako. Kuwa na msimamo itakuwa ujinga mkubwa utoke usome nursing hlf usome famacy. Mwambie Kama kumilik duka Unaweza bila kusomea... Mweleze usifikirie kutomuudhi. Mwache akasirike, we utumize ndoto zako. Atakuelewa baadaye.

Kama ni ufamasia somea ADDO, somea umiliki....biashara umeisha ndan ya mwezi.
 
Asante sana mkuu kwa mchango wako, uzuri tulishayamaliza na tukakubaliana hivi hivi kama ulivyoshauri.
Sema ndio hivyo sasahivi kozi yenyewe imesitishwa na hatuoni dalili zote kuwa itaanza upya lini




Naoam

Naona mzazi anatka kutimiza ndoto zake kupitia kwako. Kuwa na msimamo itakuwa ujinga mkubwa utoke usome nursing hlf usome famacy. Mwambie Kama kumilik duka Unaweza bila kusomea... Mweleze usifikirie kutomuudhi. Mwache akasirike, we utumize ndoto zako. Atakuelewa baadaye.

Kama ni ufamasia somea ADDO, somea umiliki....biashara umeisha ndan ya mwezi.
 
nikikumbuka vile mzee wangu alinambia nikasomee clinical officer baada ya kuhitimu kidato cha nne miaka ya 2000"s nikaleta ujuaji wangu leo niko job (sio serikalini) ila naishi kwa mashaka kama digidigi

maisha ni yako,ila biashara si lelemama mkuu alafu unaweza fanya biashara ukiwa na famasi yako
 
Back
Top Bottom