Nawezaje kupunguza gharama za umeme kipindi hiki cha mgawo?

dfreym

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
342
87
Habari, bila shaka Wote tunajua changamoto tuliyonayo watanzania kwa sasa hasa katika suala la mgao wa umeme , ambao umegeuka mwiba kwa wajasiliamali wengi.

Changamoto niliyonayo ni matumizi makubwa sana ya Fedha hasa katika kununua mafuta ya Petroli. Ambapo kwa mzigo nilionao Jenereta inatumia mafuta ya sh. 15000 kuzalisha Kw 2000 - 2500, kwa masaa manne tu. Sasa hebu pigia hesabu umeme umekatika masaa 12. Na sometimes TANESCO wanakata umeme masaa 10 mpaka 24, mara 3 - 5 kwa wiki. Ni gharama za juu sana kwangu. Kiufupi ni "headache"

Nimejaribu kutafuta ushauri kwa watu wakanishauri mambo makuu 3, ambayo napenda msaada wa ushauri wa ziada ili nifanye maamuzi kupunguza hizi gharama.

1. Nimeambiwa nitafute Genereta za Diesel ni nafuu kulinganisha na za Petrol .

2. Nitafute mashine ambazo huwa zinatumika kuendesha kinu cha kusaga zile za diesel kisha nitafute pia na motor ya kufua umeme kisha nifunge nitaweza kuzalisha umeme kwa gharama nafuu sana kwani hazili mafuta.

3. Nitafute Power tiller ya (diesel au petrol) kisha niifungie motor ya kuzalisha umene pia nitaweza kuzalisha umeme kwa gharama nafuu Sana.

Kiufupi nahitaji mawazo zaidi na ushauri zaidi nini nifanye. Ili kupunguza gharama hizi za mafuta ya Genereta maana naelekea kufilisika.

NB.
NILIJARIBU KUFUATILIA SOLAR NIKAAMBIWA GHARAMA ZA KUFANYA SYSTEM INSTALLATION NZIMA NI KATI YA MILIONI 9 -11, KUZALISHA UMEME HUO. NIKASHINDWA NIKAACHA.

2. SIFANYI BIASHARA YA KUSAGA. NINAONGELEA NAMNA YA KUZALISHA UMEME KWA GHARAMA NAFUU.
 
Namba 1, 2 na 3 zote sahihi.

Ila kumbuka gharama za uendeshaji wa biashara zikipanda nawewe unapaswa kuwachaji wateja wako ziada ya gharama.

Kwa mfano

Kama unasagisha unga za watu binafsi uwe na bei mbili, bei ya kuzalisha kwa generator na bei ya kutumia umeme tanesco.

Bei ya kuzalisha kwa generator unatakiwa uigawe ili usiathirike kwa namna yeyote ile.

Kama ukisaga kawaida mfano gharama za kuendesha mashine kwa saa limoja inakugharimu 200, na ukitumia generator inakugharimu tuseme 400, hii inayozidi inabidi wateja waifidie.

Kama biashara yako ni kuzalisha unga wa kufungasha hapa hamna ujanja inabidi uendane na ratiba ya umeme, kwa maana kama umeme upo nyakati za usiku hakikisha vijana wanapiga mzigo ili kuepuka kupunguza production capacity ya kiwanda chako.
 
Weka machine ya mafuta mkuu, nilikua nikiziona kijijini zamani, nahisi zitakua na ulaji mafuta nafuu, kuliko kutumia generator.
 
Back
Top Bottom