Nawezaje kupata wafadhili katika shule yangu?

bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,016
4,961
Wakuu naomba msaada hapa tafadhali, nimeanzisha shule ya chekechea, na tayari imeshasajiliwa huku ikiwa na wanafunzi 40,

Sasa malengo Ni kuikuza shule kwa kuongeza wingi WA Madarasa, walimu na ofisi za walimu pamoja na vifaa vyote muhimu vinavyotakiwa katika maswala yote yahusuyo shule.

Sasa naomba kujua naweza pata wap au nitumie njia gani kupata wafadhili?
Shukrani
 
Nenda benki kakope dhamana weka majengo ya shule
 
Labda shule yako inalenga kusaidia au ni kwa ajili ya kuinua kipato.Mpango kazi wako ndio utakaoongoza ufadhili
 
Ufadhiri lazima uandae andiko linalonyesha maono yako yaani unataka katika kipindi cha miaka kadhaa shule yako iwe ya aina gani, na inatoa elimu ya aina gani na kwa watu wa aina gani bila kusahau makundi maalumu kwenye jamii ambao unatakiwa uonyeshe yatanufakaje kwa uwepo wa shule yako

Vinginevyo anza kwa ushauri wa post #3 kama alivyokushauri JFK wabongo ila unaweza ukafikiria pia kuanzisha program ya walimu wa kujitolea kutoka nchi mbalimbali
 
Tha

Thanks Mkuu ntazingatia ushauri huu pia
 
Iwapo utahitaji ushauri zaidi nitafute.
Nakupongeza kwa uthubutu.
Tunahitajika sasa sisi kama vijana kubadili mtazamo ktk ajira.
Tahadhari ninayokupa ni kuwa,kadri unavyojaribu kujikomboa kiuchumi ndivyo unavyoiongezea kazi akili yako ktk kutathmini yanayokuijia.
Ktk hili ongezea haya
~Wazo ni lako wengine tunashauri~
_Usiruhusu malipizi kwa lolote litakalokutokea,litumie kwa kujipa muda kulitafakari kulipatia ufumbuzi._
_Kuwa sikivu na mnyenyekevu huku ukifanya kazi kwa bidii.Heshimu watu wa rika zote kwa kuwa wafadhili wapo Kila mahalim
 
nnachoona bora upigike mwenyewe endapo umefanikiwa kuanzia huku chini mpaka usajiri ukiwa peke yako bora uendelee mwenyewe.
 
Back
Top Bottom