Pole sana aisee....
Mie nilikuwa nasaidia sana watu....najitoa kwenye jambo la mtu utadhani ni langu
Kuna kipindi nilupata shida nikawa nahitaji 200,000 tu kuongezea... kila nilomgusa alitoa sababu... nashukuru nilifanyikiwa kusolve ile ishu hata sijui niliisolvije...
Na matokeo menginge mengine nikaja gundua mie nikipata shida hawajitoi ila mie ndo nahangaikaaaaaaaaaaaaaaaa
hiyo ilinifanya nikapinguza hata idadi ya marafiki...
Na kabla sijamsaidia mtu najiuliza mara mbili....je nikipata tatizo hiyo mtu huwa anajitoa kiasi gani kwangu.......
Yaani ilinifanya nijifunze ubandidu.....
Me nikikopesha ndo sirudishiwi....na vile ndo sijui kudai....
Nikikopesha huwa natia nia kama nimetoa sadaka....
Kabla hujaandika hapa ungeniuliza wewe una tabia gani kwnye utoaji ningekujibu kama ulivyoandika!!!
Yaani naweza kumjua mtu 'mtoaji' kiasi fulani kupitia maandishi yake!
By the way......nilkuwa Kigoma nikakutafuta kuanzia Ujiji mpaka Uvinza sijakuona, nilkuwa nauliza 'mmeshamwona yule dada wa kinyamwezi aliyejaaliwa?'...holaa
Aliyotoa hiyo phrase ya tenda wema nenda zako nampenda sana...........
Sijawahi jutia kutenda wema........ Ninafanya tena na tena hata kama hakuna shukrani
Mi naomba tuwe marafiki tuu..
Yani nakwambia me nimerithi....Bi mkubwa wangu alikuwa anajitoa sanaaa...yani ile mtu akipata tatizo ye kashafika, home hapakauki wageni, watu wakiwa na kesi huko wanakuja atawahangaikia mpaka yanaisha, akiambiwa tatizo hat saa ngapi atatoka...halafu dizaini kama walikuwa wananusa..akiwa na hela tu, watu hao na matatizo...
Sasa mzee alikuwa bandidu, hapendi zile mishe...basi full kugombana..lakini bi mkubwa hajali...Mzee akawa anamwambia nawajua hawa hawana shukrani...Bi mkubwa wapi...ndo kwanza kageuka shirika la misaada...
Mzee akaja akafariki...Bi mkubwa yupo ndani eda, hana mishe, familia zetu zenyewe hizi za kimasikini...hali tete...tulikumbwa na njaa kama tuma somalia au Sudan....kwani ndo tulimuona mtu?
Wale ndugu walokuwa wanamiminika walikata...hata simu hawapigi...
Kuna mambo mengi yalitokea hapo kati hadi nikatamani kwenda kumfufua yule mzee nimwambie ulisema kweli...
Maisha yakasonga tukasimama tena....Kwani ndo kakoma? Ndo kwanzaaaa analiendeleza....yani hadi muda mwingine namkalisha chini namkumbusha mabaya tulofanyiwa...lakini wapiiii....!
Ndo kwanza najibiwa "Atanilipia Mungu"...
last time nilikuwa na viela si vya kuweka benki sasa kuna mshkaji ana biashara zake nikawa nimeshamsoma ana financial harassment inamsumbuwa kuwalipa casual Labour wake, nikamwambia mimi nina pesa hapa ila nina kazi nayo tarehe fulani utakuwa umeshakaa sawa nikupe hii, alifurahi sana nimempa ndio kimoja na niliambulia 50, 000/= tena hii ilibidi niombe kwamba nina shida na sina pesa. imagine pesa yangu halafu kulipa liwe ombi?
Huwa wanatoa volumes na volumes za ushuhuda, eti marehemu alikuwa mtu mwema, msikivu, msaada mkubwa kwa watu wake, anaejitolea, mpenda watu, saaa chache kabla hawajakupeleka nyumba ya milele! Ndio walivo hao!
Niliwahi kumsaidia mshikaji, alikaa garage miaka miwili tangu amalize A - level, ame-despair, nilipambana kibinaadam akaingia univ, tukapambana tena, akapata student loan! Shukrani yake alikwenda kunizushia kwa yf, kuwa nachepuka na kabinti ka 1st yr, mimi nikiwa 3rd yr! Nashukuru mungu, huo mlima nilivuka salama, ila sina hamu nae!
Charming lady, wee endelea na moyo huo huo, mengine mwachie mungu! wakati wewe wema wako unakucost, kuna watu roho mbaya zao zinawacost more!
Ndo maana nimemshauri aangalie tu aina ya watu wa kuwaweka Karibu....asiache kutoa...
Wanawake bandidu nao watamu kitandani lol
Hhahaha Bi Mkubwa wako yuko kama wangu.... mpaka tukamuita "Mkatoliki" nyumba haikauki wageni hasa wa mwisho wa mwezi.....
Wageni wanajaa wanalala hadi sebuleni...
Tulipoyumba weeeee walitutetaje... hadi kijijini
Tukaja tukanyanyuka hao wakarudi...Bi Mkubwa akasamehe kabisaaaa wala hana hata kinyongo hahahahah
Ikabidi watoto tuitane kikao cha dharura aisee...haiwezekani tujinyime wazee waishi vizuri halafu wengine watuletee udwanzi wakati tukipata shida hatuwaoni.... kikao kikaamua kila mtu atimuliwe... imagine mtu kaja simply kachoka kukaa kijijini...au anaacha mke anakuja "kupumzika"
Tulitimua woteeeeee
Ndo maana nakwambia njoo nikufundishe ubandidu... tena unamkatalia mtu huku umeweka sura ya huzuni kuonyesha upo pamoja nae ktk wakati mgumu anaoupitia
Hahahaaah nitakuja nianze course...manake hii roho nikiiendekeza nitakufa masikini...!
Ila kusema kweli ile hali ngumu nlopitia kidogo imenifanya niwe na roho ngumu kwa mbaliiiiii....ilinifanya nimjue yupi rafiki wa kweli na yupi mizinguo...
Ntakuja na madaftari....
Hivi mpaka leo hii watu hawajui maana ya TENDA WEMA WENDE ZAKO USINGOJE SHUKRANI?
Kwa kawaida unapofanya jambo lolote jema kwa mtu ukitarajia malipo hususan shukurani au fadhila halafu ikatokea tofauti utaumia sana, kwa hiyo Methali hiyo inatuasa kutotarajia kulipwa shukurani au kufanyiwa wema na wale tuliowafanyia wema kwa ili kuepuka kuumia kihisia.
Kwa hiyo kama unafanya wema igeuze kama sadaka na usitarajie malipo ya aina yoyote kwnai ile ni kama mbegu njema ambayo mavuno yake huja kwa njia ya ajabu.
Soma Law of Karma .................
Ipo hapa JF wewe Google utaipata
ha haaaaa, kama unamkopesha ambaye ana shidwa haswaaaaaa, ni barakaHata kukopesha watu ni baraka...uchoyo unapunguza sana baraka
Kwa nini sikukufahamu ukiwa mtoto mzuri? Ningefaidi kweli
Jamani bado upo nije, karibu sana babu.
Halafu babu naona uzi huu umekimbiwa selfish person nimejikuta pekee yangu wengine wote watoaji. Mniombee nibadilike kwa kweli.
ndo manakekauzu kama dagaa...lol
Kauzu
bado nimekubakizia nafasi yako ya kufaidi. lol