Naweza kupata chuo cha shahada

Naweza kupata chuo cha shahada

Mkuu, unakosea sana kusema hivo juu ya mwanao
Mimi siku nikiwa na mtoto siwezi kumsemea hivo
You got to be proud of your child
Am proud of him,but has shamed me !each and every thing i gave so as to achive his studies well ,unfortunately he held last postion in the class
 
Am proud of him,but has shamed me !each and every thing i gave so as to achive his studies well ,unfortunately he held last postion in the class
Usikate tamaa, mkuu
Mark my words ,inawezekana huyo kijana ako siku moja atafanikiwa kuliko waliopata div one

Nachokushauri wasilikilize member wakupe ushauri,na usimuoneshe mwanao kama umemkasirikia au kumdharau

Mimi nimesoma na watu ambao walifaa wamalize shule waka fail .na pia nilivofanya nao mitihani waka fail pia lakini hawakukata tamaa
Kuna mtu namjua anefanya mtihani mara 4 ana fail tu

Hata hivo uangalie na record zake huyo dogo labda ametereza tu
 
Kwa hayo matokeo hata vigezo vya zamani vya atleast two principal pass haendi (zamani two principal pass EE uaingia chuo tena kozi za sayansi za kumwaga)
 
Habari wakuu?naomba kujua mwanafunzi aliepata daraja la 15 kwa mchepuo wa CBG anweza pata chuo cha shahada?pia kozi zipi anaweza somea kutokana na ufahuru huo.....naombeni ushauri kwani hapa nilipo sina hamu na huyu mtoto,nmemupatia kila kitu lakini mtunda yenyewe ndo amekuwa wa mwisho darasa zima

Wazazi hupata changa moto sana. La kwanza wewe mwenyewe ukubali hayo matokeo hata kama hayakufurahishi. La pili hakikisha mwanao anayaelewa hayo matokeo na yana maana gani kwake. La tatu ndiyo kuangalia nini kifanyike-kurudia masomo au kwenda vyuo vya kati kwani kwa point 15 za NECTA hatakuwa na point 4 za TCU kwenda chuo. Hapo itabidi kuingia NACTE ili kuangalia koozi ziizopo kwa mtu mwenye ufaulukama wake na kuchagua iliyo sahihi au mbili tatu ambazo ukizileta hapa JF (elimu) nina hakika utapata ushauri kuntu. Pole kwa hili lakini haya ndiyo maisha yanayowasibu wazazi wengi.
 
Amepata S.S.D

S S D, umenikumbusha mbali wakati PCB ilivyoniadhirisha, na kunitunuku matokea ya namna hiyo.

By the way SSD ni point 16 na sio 15.
Kwahiyo kuna mambo mawili hapa, huenda huyo kijana wako hana point 15 au huenda hana SSD, angalia vizuri hayo matokeo mkuu.

A=1, B=2, C=3, D=4, E=5, S=6, F=7

SSD = (6+6+4) = 16.
 
mkuu..kama uwezo upo mpeleke akasome India au malaysia
 
my friend kwanza relax! ..........................(pia pole kwa yaliyokukuta, nawasiwasi ni wewe)

Vyuo ni vingi sana, inahitaji kutulia, leo matokeo yametoka, huwezi fanya maamuzi mazuri leo, pata muda, tafakari matokeo yaliyopatikana kisha angalia muhusika (au kama ni wewe) unapendelea kusomea nini, kisha tafuta vyuo utapata vingi,

binafsi dv iii.15 sio ya kukosa chuo!
Div.III ya 15 sio ishu, ishu ni je ana D mbili ambazo ni Principal Pass.
 
Am proud of him,but has shamed me !each and every thing i gave so as to achive his studies well ,unfortunately he held last postion in the class
Kila kitu mkuu hupangwa na Mungu cha umuhimu afanye kuapply kwa ngazi za diploma asome.
 
Haiwezekani in 2 years ukapata marks za mbumbumbu
PCM nikatoka na div 1
Sijawahi kukutana na MWANA-PCM mwenye majivuno kama wewe. Nina hofu na hiyo div 1 yako
Kwa masomo ya advance ya science miezi 19 ni michache mno.Tulio soma PCM mara nyingi tulikuwa tunaangukia kwenye kusoma PM zaidi kwa ajili ya calculation...

Kama una uwezo wa kumshauri huyo mzazi kozi ya kusoma mwanae naomba mshauri vizuri...
 
PCM nikatoka na div 1
Hongera kama kweli!
Ila ninavyojua Mimi elimu ya advance hasa kwa science inahitaji mtoto aweze kuwa Na Akili ya kudaka mambo haraka kuliko kawaida ndio anafanya vizuri!

Ndio maana Wengi wanaosoma science huwa wanapata div three!
Muda wa advance ni mchache kiasi kwamba wale ma slow leaner ni ngumu kupata matokeo mazuri ukilinganisha na olevel!

#NB

Usimuite mbumbumbu kwasababu ya hiyo div 1 yako sio tabia nzuri!!!
 
Back
Top Bottom