Naweza kujenga nguzo za kibaraza kwa matofali ya kulaza?

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,720
107,836
Kwenu wataalam wa ujenzi. Naweza kujenga nguzo za kibaraza kwa matofali ya kulaza, yaani niachana na nguzo za nondo/zege? Juu nitaweka mkanda kama kawaida. Kiutaalamu ina madhara yoyote?
 
Sina hakika kama kuna madhara maana hii kitu nimeiona sehemu nyingi sana tu. Kwenye nyumba yangu architecture pia alidesign kibaraza cha matofali ya kulaza ila mimi sikupenda nikaweka nguzo. So, hakuna shida ila kuna maximum span baina ya nguzo na nguzo, kama span ni kubwa na panabeba weight kubwa itabidi uweke nguzo katikati au uweke tu cha zege na nondo kwa kuzingatia weight
 
Binafsi sina jibu ila sijawah kuwaza hilo considering the fact kuwa ni risk za nje nje reja reja unajitakia verand iwadondokee watoto wafe.
Kwanini usitumie mkuu?! Nondo moja ni 27k au 28k kwa mikoan.
 
Kwenu wataalam wa ujenzi. Naweza kujenga nguzo za kibaraza kwa matofali ya kulaza, yaani niachana na nguzo za nondo/zege? Juu nitaweka mkanda kama kawaida. Kiutaalamu ina madhara yoyote?

Mimi sio mtaalamu wa ujenzi lakini najua inawezekana kama utazingatia vitu hivi...

1. Eneo unapofanyia ujenzi lisiwe yale maeneo yanayosumbuliwa sana na cracks...

2. Kwa kuwa upande mmoja wa baraza utashikwa na ile beam inayozunguka nyumba, hivyo hizo nguzo za baraza zitahusika kubeba kiasi tu cha uzito wa slab (wataalam wa ujenzi pengine wana kanuni zao)

3. Umbali wa kutoka nguzo moja kwenda nyingine usizidi mita 4 (hii sina uhakika zaidi ya uzoefu, wenye kujua zaidi watarekebisha)

4. Baada ya ujenzi Slab isitumike kubeba mzigo kama matank ya maji...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom