Nawaza tu Maisha bila Mapenzi yangekuwaje

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Najaribu tu kuwaza ndani ya kichwa changu haya maisha kama yasingekuwa mapenzi ingekuwaje, Dunia tungeiona Tamuuu, tungekuwa na furaha au mda mwingi tungekuwa tunahuzunika mi sijui nawaza tu.

Nani angekuwa anamkumbatia mwenzie wakati wa kulala tena wakati wa baridi kali, je shuka na blanketi zingekuwa ndo faraja yetu, kama ndivyo ingekuwaje bahati mbaya umepitiwa na usingizi na hujajifunika shuka wala blanketi nani angetufunika au ndo tungepigwa na baridi mpk tutakapoamka!!! Sina uhakika najaribu tu kuwaza.

Kama kusingekuwa na mapenzi inamaana mi leo nisingekuwepo, wala mtoto wangu asingezaliwa!!! Faraja ninayoipata kwa mtoto wangu nisingeipata maana mimi mwenyewe nisingekuwepo, dunia ingekuwaje wangekuwa wanaishi akina nani sijui mimi najaribu tu kuwaza.

Nikiumwa usiku wa manane ingekuwaje ndugu wangekuwa msaada kwangu? Wangeweza kutoka makwao mpk kwangu usiku wa manane kunisaidia? Nikitoka kazini nimechoka hoi nani angenipikia na kuniandalia chakula kitamu, nikilala fofofofo asubuhi na kuweza kuchelewa kwenda kazini nani angekuwa msaada wangu wa kuniamsha pale ninapopitiwa,? Najaribu tu kuwaza maisha yangekuwaje bila mapenzi.

Bila mapenzi nani angekuwa mshauri wangu wa karibu, mwenye kuwa tayari kufanya kil jambo ili nifanikiwe, nani angekuwa ananipa pole pale ninapoumia, nani angekuwa ananishikilia pale ninapotaka kudondoka nawaza.

Kusingekuwa na mapenzi wanawake wangekuwa wanajipodoa, wanashindana kupendeza, wangekuwa wanaweka limbwata kwenye vyakula, nawaza tu.

Kiukweli bila mapenzi kwa maoni yangu Dunia ingekuwa inaboa sana, tuyaheshimu mapenzi yanachukua Asilimia kubwa ya maisha yetu.
 
Naamini pasingekuwepo mapenzi juhudi zingepungua binafsi nafanya kazi kwa juhudi na maalifa ili kumtimizia mahitaji ya kipenzi changu maana kwa sasa hana mume wa mtoto asie kuwa mimi hivyo naĺazimika kufanya kazi kama mtumwa ili mama yangu aishi kama malikia
 
Yasingewezekana kwa wadada sababu wanapenda na kuamini kuna mapenzi,labda bila K ndo ingekuwa tatizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom