tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,647
- 29,012
WAZO LANGU:
Kwa spidi hii aliyoanza nayo Dr Magufuli, nina wasiwasi wanaCCM wenzake wanaweza kumuundia zengwe la kumfunga spidi gavana au kumuondoa kwenye reli kabisa.
Nasema hivi kwa kuwa wanaCCM wengi walikuwa wamezoeshwa vya kunyonga kwa muda mrefu pamoja na upigaji dili wa kutafuna rasilimali za taifa. Kwa kuwa Bw Makufuli haangalii sura, inaweza ikawawia vigumu panya wengi waliojaa ndani ya CCM kupiga dili zao kama walivyozoea ukajikuta wanamtafutia zengwe na kumfanyia ugaidi kama ule waliomfanyia Aboud Jumbe kule Zanzibar au kama vile walivyomfanya Sokoine. Nina wasiwasi sana kuwa huyu rais asipoangalia spidi yake anaweza kujikuta anawakwaza wazee wa kitengo, nao wakaamua kumwaga mboga ili wakose wote.
WanaCCM wengi wanajiona mchwa kuliko raia yeyote katika nchi hii na umchwa huu ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi wa juu. Sote ni mashahidi jinsi watu wanavyoangushwa katika ubunge na kisha kupewa vyeo vya ukuu wa mikoa, wilaya, nk.
USHAURI:
Please Dr Magufuli take extra care!
:israel: