gillard
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 227
- 165
Kwa nini namlaumu na simlaumu Rais Magufuli
Labda nianze kwa kusema yanayotokea leo ni matunda ya yaliyotokea jana. Waswahili wanasema, "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" na "usipoziba ufa utajenga ukuta"
Kwanini simlaumu Rais Magufuli
Tuangalie matukio haya ya utekaji katika awamu iliyopita, wakati wa utawala wa Rais kikwete tutakumbuka, kwa mfano utekwaji wa aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Dr. Steven Ulimboka na aliyekuwa mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda. Matukio haya mawili yameacha sintofahamu hadi leo hii, wanaolinda usalama wetu wameshindwa kabisa kutwambia adui ni nani, ili na sie wengine tuchukue tahadhari gani dhidi ya huyo adui, hata wahusika wenyewe wameshindwa kuueleza umma kwa undani nini hasa kilitokea licha ya kuahidi kufanya hivyo (siawalaumu). Hayo ni mawili tu kati ya mengi ya hovyo kabisa kuwahi kutokea katika nchi yetu wakati wa utawala uliopita, sitaki hata kukumbuka ya Mwangosi(RIP), kamanda Zombe vs wale wafanyabiashara ya madini (RIP).
Wakati Mzee Kikwete anaondoka madarakani alisema, “Naiacha Nchi ikiwa salama” Nadhani dhana ya kuiacha nchi salama kwa marais wetu ni kuiacha ikiwa haina nchi adui. Lakini kwa mtazamo wangu usalama wa chi ni pamoja na kwanza wananchi wenyewe kuwa salama ndani ya nchi. Nchi ni watu na watu hawa wanatakiwa kuwa salama kuanzia kwa adui wa Ndani kama watekaji, majambazi, maradhi, ujinga nk. Nataka kusema nini hapa, Mzee wetu Kikwete amemuachia Rais Magufuli nchi katika hali tunayoiona sasa, walewale waliozoea kufanya awamu iliyopita wanaendelea kufanya yao, si ndivyo walivyolelewa, si hata Rais anaona sawa tu?
Kuna kasumba katika nchi hii tokea enzi za Mwalimu Nyerere kwamba Usalama wa Taifa vikiwemo vyombo vingine vya dola ndiyo wenye nchi, kwamba wanaweza kufanya watakavyo, sasa sijui ni katiba gani au sheria gani zinawapa nguvu dhidi ya wananchi. Na bahati mbaya katika bunge letu miaka kenda sasa watu hawa hawaguswi hata kama wanahatarisha maisha ya raia wanaowalinda, au kwa kuwa wanalinda maslahi ya kikundi fulani cha watu kwenye ballots? Hapana Hapana Hapana, sisi wananchi ndio wenye nchi na mnafanya vurugu kwa kodi zetu.
Kwanini namlaumu Rais Magufuli
Ulitwambia mwenyewe kuwa wewe upo kwa ajili yetu wanyonge na moja ya maneno yako yaliyopenya kwenye mioyo yetu na kukuona mkombozi ilikuwa “Msema kweli ni mpenzi wa Mungu” na ukatuahidi kuwa hutatuangusha, lakini nahisi hata hujatubeba, mana ili kuangusha shurti ubebe kitu.
Kama Rais wa chi una wajibu kwa kila mwananchi hadi yule wa chini kabisa, nikupongeze kwa kupiga simu kwa kuongea na yule mama aliyeunguzwa kwa maji moto na mumewe kumpa pole nakumsaidia na kuagiza mumewe akamatwe. Lakini najiuliza, ina maana yaliyotokea clouds TV hukuyaona? Kupotea kwa Ben Sanane hujasikia? Kutekwa kwa Roma? waziri mstaafu kutolewa bastola hadharani Mbona uko kimyaaa?? Huoni kama kuna tatizo kubwa katika suala zima la ulinzi wa nchi yetu? Kama uliweza kuwa na muda wa kuangalia shilawadu kama ulivyokiri mweyewe, kufuatilia vipindi vya clouds fm(sina hakika kama bado unaendelea ), kujibu vijembe vya kwenye mitandao kwa ajili ya kumtetea mtu mmoja tu unashindwaje kuonyesha kujali na kuchukua hatua au basi kusimama na kukemea haya mambo yanayowagusa watanzania walio wengi? Ulisema, “I wish I could be IGP” nilidhani kusema kule uliona uozo wa vyombo vyetu vya usalama?
Wanaokudanganya na kukupotosha watakuja hapa na kusema mbona kuna waziri wa mambo ya ndani ana kazi gani, kuna mangapi wewe umeyatolea tamko bila hata kumhusisha waziri husika? Lile la mwakyembe na vyeti vya kuzaliwa kwenye ndoa ni mfano tu. Isitoshe hili ni tatizo lililo juu sana ya mawaziri wenye dhamana, linahitaji kauli yako mkuu. Kwa hali iliyopo sasa inanikumbusha uzi wa mwanakijiji hapa jamii forum kuhusu usalama wa taifa, bofya hapa kusoma. Ni vigumu kuwaza kama usalama wa taifa na pia majeshi yetu wapo kwa ajili ya watanzania au wapo kwa maslahi yao binafsi. Kwenye mambo yote maovu yahusuyo watu wanalaumiwa wao, ufisadi wao, kushiriki kuiba kura wao, ujambazi wao na no one says anything, it’s like “to hell”. Sasa kwa nini mheshimiwa usiyaangalie na kuyakemea haya majipu manene hivi?
Mwisho Mh. Rais, unapozungumzia kunyosha nchi nielewacho mimi ni kukuza uchumi, kupiga vita na kuziba mianya ya rushwa, kuleta nidhamu ya kazi, kulinda rasilimali za taifa, kuboresha maisha ya watu na kulinda usalama wao na mambo yanayofanana na hayo. Lakini nataka niseme tu, yapo uliyofanikiwa mfano nidhamu ya kazi, watu sasa angalau wanaogopa kupokea na kutoa rushwa, kudhibiti matumizi mabaya na asiyefanya kazi na asile, hongera. Lakini, rasilimali watu ndio itakayokufanya ufanikiwe vizuri hayo yote na hayo makubwa zaidi ambayo ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu, ukimya wako ndio unfanya hao masikini ulioahidi kuwapigania wadhani hii ndio staili yako ya kunyosha nchi, na hivyo kuishi kwa hofu kila uchao. Na kama watu wanaishi kwa hofu usitegemee nchi kunyoka tegemea kupinda zaidi. Kwa hali hii hata hao unaowategemea waje kuwekeza nchini utawakimbiza, si unaona hata wawekezaji wa ndani wenyewe baadhi yao hawaeleweki sasa kila siku wanapunguza wafanyakazi?
Nashukuru hata CCM sasa wamenza kuyaona haya, mana yanarudi kuwatafuna wao pia, huko nyuma ilikuwa ukisema tu unaambiwa wewe huipendi serikali unashabikia upinzani, unapuuzwa na kuundiwa zengwe na hata kuswekwa ndani. Nina mengi ya kusema ntaendelea wakati ujao. Nimalizie kwa kumpongeza Hussein Bashe kwa ujasiri wa hata kuthubutu kutaja jina tukufu la TISS na kuwarushia tuhuma akiwa bungeni, ni nadra sana kwa mbunge wa CCM kufanya hivyo na hasa katika kipindi hiki cha naibu Spika pandikizi, Hongera sana. Nampongeza pia Zitto kabwe kwa kulisemea hili kupitia mitandao natumai atalifikisha bungeni pia.
Niwatakie siku njema na kazi njema, twende tukalijenge taifa sasa, japo naogopa sijui Noah ipo nje hapo