Nawaza kichwani, wanaojua nisidieni

Nawaza kichwani, wanaojua nisidieni

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,899
Hivi kama ikitokea mahala popote duniani kwamba Amiri jeshi anamshauri mkuu wa majeshi aende kusoma, halafu mkuu wa majeshi anakataa kwamba hahitaji kusoma. Halafu amiri jeshi yule yule anamshauri mkuu wa majeshi achukue nchi kwa nguvu, mkuu wa majeshi agomee mpango labda kwa kuwa haoni sababu.

Halafu mkuu wa majeshi anapokuwa amesafiri, amiri jeshi akimbilie kwenye chuo cha mafunzo ya maofisa wa ngazi za juu wa jeshi kwenda kuwa graduadisha na kuwapa nishani mbali mbali. Halafu mkuu wa majeshi anaporudi, agomee hizo nishani na gradudu kwamba imefanyika kinyume cha utaratibu na hivyo kuwanyang'anya hao waliopewa nishani kwamba wasubiri taratibu zote zitafanyika kwa utaratibu unaofahamika.

Hivi ikija kutokea hali kam hii duniani popote, ina maanisha nini? Suluhu y ahali kama ile inaweza kuwa nini?

Ni kupanuana mawazo na mitazamo kwa mambo mbali mbali ambayo wengi hatuna utaalam nayo. Kuelimishana na kujengeana ufahamu tu ukizingatia kwamba nidhamu na kanuni za jeshi huwa zimesokotana na zinakuwaga na masuala mengi nyeti na ya siri.
 
hi ni ngumu kutokea... hata ikitokea inategemea situation ilikuwaje..
1.kama amiri jeshi anaona yuko sahihi basi anaweza kumvua cheo mkuu wa majeshi ili kulinda usalama.
2.amiri jeshi akiona mkuu wa majeshi yuko sahihi basi anaweza kukubali huo utunukwaji wa nishani urudiwe upya.
... kimbuka amiri jeshi(rais) ndio mwenye mamlaka ya mwisho.
 
Tatizo kubwa ninaloliona ni Kuwa unataka kupanua ufahamu na kupata elimu kwenye hili jukwaa
 
Back
Top Bottom