Mwanakijiji, SIUNGI MKONO hoja yoyote inayolenga kumpa kuongeza kipato kwa sekta moja na nyingine kuwa hoi. Kama ambavyo siungi mkono wabunge kuongeza posho zao NAPINGA DAKTARI KUOMBA aongezwe mshahara.
Hoja zangu ni kwamba hakuna fani iliyobora zaidi ya mwingine, daktari ni muhimu sana, lakini anajua vifaa anavyotumia zinatengezwa na wahandishi (aibu kwamba ni wa nje ya TZ), anajua anatumia mifumo mbalimbali ya kompyuta kufanya uchunguzi, anajua yeye amekuwa dakatari kwa hiari lakini vile vile wote tusingeza kuwa madaktari ndo maana tukagawana kwa hiari hizi fani, lengo ni kuhakikisha tunasaidiana kwa pamoja kujenga nchi na watu wake. KIPATO ni kidogo ama kwa ajili ya wizi wa Serikali na Wazungu au kwa maana tu ya kidogo hivyo ni vema kama Serikali inapandisha mishahara itumie formula fulani kupandisha kwa Watumishi wote.
SIKUBALI SEKTA MOJA KUWA BORA KULIKO NYINGINE NAAMINI KATIKA MGAWANYO WA KAZI, hivyo maslahi yakaribiane kwa sekta zote, hasa kwa ukweli kwamba soko na mfumko wa bei ni moja tu kwetu sote