Mimi, Msando simfahamu wala hatuko pamoja kwenye hilo kundi unalosema lipo. Najua angesema anamshtaki Chatanda wa CCM na Mwanasheria Mkuu mngempa misenks ya kudondosha thread hii. Yeye kaona mbali zaidi. Kagundua tatizo hilo hata kwenye chama chake lipo. Na sio kwa majimbo hayo mawili tu Tanzania hii. Alifumbie macho kwa kuwa linaigusa CHADEMA au afanye kile ambacho TAALUMA na dhamira yake inamtaka kukifanya?Mkuu sijaingiza siasa za vyuoni kama unavyodai. Nimejadili hoja yake kwa namna ambavyo mimi ninaona. Tatizo lenu kuna kundi fulani humu jamvini halitaki likosolewe. Na kwamba hoja ikitolewa na mmoja wa watu wa kundi hilo basi sisi wengine wote tuisifie na kuimwagia thanks. Tukiijadili kwa maono kinzani kinyume na vile mnavyotaka basi matatizo. Kama hivyo ndivyo basi waambieni mods wawaondoe wale wote wenye mtazamo tofauti na ninyi.