Pole sana kwa kukaririshwa. Ujinga wako ndio unaokufanya uone huo umaskini ulionao umesababishwa na CCM. Punguza starehe, punguza uvivu, punguza tabia ya kulalamika, tumia elimu uliyoipata kujiletea maendeleo, fanya kazi kwa bidii, kile kidogo unachopata kisave, vaa nguo zinazoendana na kipato chako, miliki simu zinazoendana na kipato chako, acha matumizi ya simu yasiyo na faida. Jiwekee malengo walau kwa mwaka mzima na mwaka ukiisha jipime kama umefikia malengo yako. Na la zaidi acha kuhonga. Ukifanya haya hutakuwa na lawama kwa CCM na maisha yako yatakuwa bora.