Nawashangaa Sana masikini wanaoshabikia CCM

Nawashangaa Sana masikini wanaoshabikia CCM

Usifanye mchezo na njaa ndugu yangu.watu wakipewa ubwabwa tuu,kila inapotokea uchaguzi,kwanini wasiione CCM ndio Mungu wao.,mimi nafikiri kwanza wapinzania wangewekeza sana nguvu kuelimisha watu nini maana ya KURA..zina faida gani na hasara gani katika maisha yao.maana Watanzania wengi awajui bado umuhimu wa Haki zao,
 
Sielewi, mtoto wa mbowe au lowasa wanasoma shule za kata? Mbowe (chadema) kwa mabilioni wanayoamisha washawahi kujenga shule hata moja au kufanya chochote kama kuwasaidia wa Tanzania; kwa mfano kutoa scholarship kwa watoto masikini, kujenga kituo cha watoto yatima, kuwapa mikopo wa kina mama n.k vitu vidogo tu kama CSR kusaidia jamii inayowazunguka. Kama laah hawa watu wanautofauti gani na hawa CCM. Wewe hichi chama cha familia ya Mtei kimeku brainwash wenzio wanataka dola walipe madeni kutoka kwa wafadhili unadhani misaada wanapewa tu bure (hawa wanafanaya long term investment) . CCM, chadema wote wale wale na mwisho wa siku wa Tanzania 'wengi' wakifika kwenye chumba cha kupiga kura wanafikiriaga haya mambo, ndio maana wanampigia shetani wanaemfahamu au simba aliyeshiba.
 
Hivi Watanzania tumelogwa na Nani, Tunahitaji nini kufunguliwa macho kuona Udhalimu wa CCM. Ni familia gani ya Kigogo wa ccm inaishi maisha ya kawaida isipokua ya Mwalimu Nyerere?

Hata viongozi wa ukawa ukiwatizama hivi ni nani kati yao anayeishi maisha duni, anzia na sawalo, yemasu, wembo,ngenguki. Tunawashangaeni sana nyie mnaowashobokea! tena hao waliotoka ccm ndo kabisaaa, huyo ngenguki nadhani mnafahamu mwanaye wa kiume ambaye anasumbua sana hapo Dar kwa maisha yake ya anasa!
 
Wew unaonyesha huna msaada kwa nduguzo tu........ Wacha kusingizia uCCM na UKAWA hapa........ Watu wanakushangaa ushindwe kumsaidia nduguyo akipatwa na shida eti kisa anaipenda CCM.....????? YOU'RE A COWARD
Nina mama mmoja ndugu yangu ni maskini lakini ccm damu, juzi kaja anaomba hela kwangu nikamwambia kaombe ofisi ya ccm, duh mke wangu aliniwakia kwa kauli hiyo ikabidi yeye ndie ampe mimi nilishaondoka hapo. Ndio mwendo huo maskini nendeni ofisi za ccm ndio mkaombe hela.
 
Usimtolee mfano huyo aliyetelekeza mke na watoto akakimbilia kwa kimada mke wa mtu.
Huyo sio mfano bora kwenye jamii, uliza watoto wa mchepuko wake huo anawasomesha wapi?
Nyie mnadhani yule mama mwl kuamua kususa vigora ni mchezo? Hamumjui Pombe Nyie na vituko vyama!

Sijui inawezekana wapi mtu aliyeshindwa kutunza familia yake akaaminiwa kutunza taifa.
Katika moja ya vitabu vitakatifu imeandikwa: "Asiyewajali wa nyumbani mwake ni m-baya kuliko asiyeamini (Mungu)."

Masikini wanaoshabikia FISIEMU, wana kiu na haja ya kuona watoto wao wanasimamishwa masomo kwa kukosa michango ya shule ambayo ni mikubwa kuliko ada.
Wanapenda sana kuchangia mwenge.
Wanaburudika vilivyo kuhangaika kutafuta maji mchana na usiku, wala nishati ya umeme kwao si muhimu.
Wanafurahia kabisa watoto wao wanapobambikizwa kesi na kutupwa magerezani.

Maskini hao hufarijika sana mwaka wanapovuna mazao mengi yakaozea ghalani kwa kukosa masoko kwani serikali ya FISIEMU haitaki mazao yauzwe nje ya yeyote isipokuwa mafisadi walio ndani yake. Maskini hawa wanatamani sana umwagaji damu (kwa amani na utulivu) unaochagizwa na FISIEMU kati ya wafugaji na wakulima.

Maskini hawa washabiki wa FISIEMU wanapenda kugawiwa vivazi na fedha mwaka huu wa uchaguzi na hivyo wamesahau mateso yote yatakayowakabili kwa miaka mitano. Kutukanwa na kupuuzwa kwa wazee ni wimbo unaowaburudisha vilivyo hawa maskini, pamoja na udhalilishaji wanaoupata wagonjwa na hasa akina mama wajawazito hospitalini.

Maskini hawa wanaoshabikia FISIEMU watapata wapi burudani za harufu mbaya ya majitaka yanayotiririrka ovyo na magonjwa kama "kipinduapindu" yaliyotamalaki hasa jijini Dar es Salaam bila FISIEMU yao? Tena watakosaje uhondo wa kupita kwenye barabara zenye mahandaki zilizotengenezwa kwa fedha lukuki na mara kuharibika kwa kutekwa na makandarasi wahujumu wakiongozwa na mgombea wao? Ni lini watacheka maishani bila kuambiwa wapige mbizi kama hawana nauli za vivuko? Au wakojoe kama wanataka maji? Ni lini watasikia vitisho masikoni mwao kwa utumwa waliouzoea miaka zaidi ya hamsini? Nayo raha ya kuvunjiwa nyumba bila fidia wakaipate wapi bila kushabikia FISIEMU?

Mkuu usisahau kama hao maskini, moja ya faraja kubwa ni pale maskini anapodai haki yake, kesi yake ikapigwa kalenda miaka nenda miaka rudi. Angejuaje kazi za mahakama maskini kama huyu bila kwenda huko mara kwa mara na kutoa chochote? Pia kuna ile sifa kwa maskini ambao ndugu zao wanawekwa mahabusu kwa miaka na miaka wakingojea kesi zao zisikilizwe. Wakose yote haya, mmh mbona watakonda ndio maana wanaishabikia FISIEMU.

Ee bwana wee, maskini hawa wanaoshabikia FISIEMU, hawajachoka ahadi hewa. Si umejionea mwenyewe ahadi za yule "Zaifu" zinatolewa tena na huyu changudoa wa kiume? Yeye zake zinazidi trilioni 70 (yaani mara tatu na ushee ya bajeti ya mwaka huu ya serikali) lakini wamo tu hawa maskini. Zile za "Zaifu" maskini hawa walishasahau. Kama unabisha katoe ahadi ya kuhamia Dodoma uone jinsi watakavyoshangilia.

Wamesahau kuwa kwa uzembe wa serikali ya FISIEMU ambayo badala ya kuweka akiba chakula kingi kilichopatikana mwaka jana, mwaka huu njaa imetamalaki. Watakubali wapi kukosa udhalilishaji wa kugawiwa kilo moja kwa kila familia kwa wiki mbili au mwezi?

Maskini mashabiki masikini wa FISIEMU!
 
Wewe Unashinda Kijiweni Mtaani Kwenu Uchafu Kibao Unashindwa Kutake That Opportunity Kujiajiri Kwa Kukusanya Takataka Ukapa Msosi Unalalamika Maskini.
Af Unailalamikia Ccm Kwa Uvivu Wako Wa Kufikirisha Ubongo Na Kukamata Fursa.Unadhani Ukawa Itakuja Hapo Kukupa Pesa
Acha Ujinga.

Ukikusanya huo uchafu nani atakulipa ? au ukisha ukusanya tu unageuka kuwa pesa.
 
Sielewi, mtoto wa mbowe au lowasa wanasoma shule za kata? Mbowe (chadema) kwa mabilioni wanayoamisha washawahi kujenga shule hata moja au kufanya chochote kama kuwasaidia wa Tanzania; kwa mfano kutoa scholarship kwa watoto masikini, kujenga kituo cha watoto yatima, kuwapa mikopo wa kina mama n.k vitu vidogo tu kama CSR kusaidia jamii inayowazunguka. Kama laah hawa watu wanautofauti gani na hawa CCM. Wewe hichi chama cha familia ya Mtei kimeku brainwash wenzio wanataka dola walipe madeni kutoka kwa wafadhili unadhani misaada wanapewa tu bure (hawa wanafanaya long term investment) . CCM, chadema wote wale wale na mwisho wa siku wa Tanzania 'wengi' wakifika kwenye chumba cha kupiga kura wanafikiriaga haya mambo, ndio maana wanampigia shetani wanaemfahamu au simba aliyeshiba.

unajuwa kodi anayolipa mbowe lowasa zimejenga shule ngapi au rais wako kalipa nauli ya kwenda tibiwa usa kwa kodi ya mbowe ..
Elimika elimu tuelimike hata mimi kama nina uwezi siwezi peleka mtoti shule za kata hakuna waalimu vitabu vyoo umeme hata uji shuleni hakuna
umewahi ona sec kuna waalimu 4?
 
Ila hawa masikini mwaka huu wameshituka ndiyo huo moto unao waka huko mitaani!
 
Namimi nakushangaa zaidi wewe mtu unayeamini eti Mbowe na Lowasa watakukomboa
 
Nina mama mmoja ndugu yangu ni maskini lakini ccm damu, juzi kaja anaomba hela kwangu nikamwambia kaombe ofisi ya ccm, duh mke wangu aliniwakia kwa kauli hiyo ikabidi yeye ndie ampe mimi nilishaondoka hapo. Ndio mwendo huo maskini nendeni ofisi za ccm ndio mkaombe hela.

Na kwa mtindo huu hata mkeo atahamia CCM kama alikuwa CHADEMA, vinginevyo hutawapata wafuasi hata siku moja...!
 
Hivi Watanzania tumelogwa na Nani, Tunahitaji nini kufunguliwa macho kuona Udhalimu wa CCM. Ni familia gani ya Kigogo wa ccm inaishi maisha ya kawaida isipokua ya Mwalimu Nyerere?

CCM ni wakala wa Umaskini,ujinga na maradhi,tuikatae CCM inayotumia umaskini wetu kama ngazi ya kukwea katika mafanikio!!
 
Kuna wale wafagia barabara nao wanaishabikia ccm, nashangaa sana
 
Hivi Watanzania tumelogwa na Nani, Tunahitaji nini kufunguliwa macho kuona Udhalimu wa CCM. Ni familia gani ya Kigogo wa ccm inaishi maisha ya kawaida isipokua ya Mwalimu Nyerere?

Kwani ni familia gani ya kigogo wa UKAWA anaishi maisha ya kawaida kama nyie Mazombie
 
Back
Top Bottom