Nawapongeza wale wote waliotoa filamu zao ingawaje zingine zilikuwa series

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Nawapongeza wale wote waliotoa filamu zao ungawaje zingine zilikuwa series.

Kwa muda wa wiki moja kumetolewa fulamu zaidi ya tatu zenye madhumuni hasa ya kuua series moja iliyokuwa ikiendelea "Albert"

Clouds waliianzisha filamu ya kwanza. Sababu haiwezekani kama Kweli kile kitendo kiliwauma na lilikuwa kosa Kweli kukaa Siku zaidi ya mbili bila kuripoti polisi. Clouds walitoa hewani baada ya baadhi ya taarifa kutoka hadharani na kwa kuficha aibu ndiyo wao wakaanza kuitangaza. Ikiwa kamanda Sira alitangaza hana taarifa hizo je, taarifa iliyokuja kuwa ruge yuko polisi alienda kupiga soga? Kama hiyo haitoshi iweje alipoulizwa kisa hasa ni nini, nani aliyemleta huyo mama liwe jibu gumu kiasi hicho? Je kama angekuwa ni Mnyika au mtu mwingine wangesubiria aje kuomba msamaha kama ilivyokuwa kwa RC?je, kama angetangaza machafuko pia wangekaa kimya?

Wakati tukiwa tunaanza kuangalia filamu hii na kwa mbaali kumsahau Albert tukaletewa ya kaka Nape. Hahahaaaa hapa watu wengi wakaingia wakazidi kumsahau albert. Wakaona haitoshi sasa tuwapoteze kabisa ikaletwa ya kutishwa bastola hadharani. Hapo watu wakachanganyikiwa zaidi. Sasa ikabaki kuwapa kizunguzungu ikaja kauli" nikisema kilichoko humu mtalia" du! Watanzania walie mara ngapi? Watanzania kama ni kupigwa cha juu tumepigwa sana hata sasa tunapigwa sana na kulia naimani tumeshalia sana.

Wakati bado tunafikiria tuende na movie upi tunarudishwa nyuma kidogo huwezi kutoa hukumu kwa mahojiano ya upande mmoja. Hivyo wakati tume inafanya kazi si alitafutwa na hakuonyesha ushirikiano? Sawa hii movie itaendelea kuwa walienda kutafuta ngada na itakuwa mwisho wa muvi. Hapo hapo ikaja episode 2 ya mtoa bastola kuwa hajajulikana! Hivi wale polisi walioenda kuzuia mkutano kama hakuwa mwenzao kwa nini hawakumkamata? Jibu la hii episode litakuja kwenye episode 3.

Baada ya hapo ikatokea taarifa kubwa la maadui sasa hivi anatembea na gari 3 mbili zikiwa za walinzi tinted kubwa. Akipaki eneo anahamia gari lengine. Dah!

Ikawekwa trela nyingine ya msomali kuwa atatoa neno. Macho, masikio ya kahama punde likaja tangazo filamu bado inaandaliwa maana staring amepata mushkeli. " hivi mgonjwa anatumwa hospital au anaenda mwenyewe" ? Muandaaji ya hii muvi amebugi mahali.

Leo hii series iliyokuwa hewana ya Albert haisikiki na haitaendelea kama mwanzo sababu watazamaji na wasilizaji hawajui waende na njia gani.

Tukubali tukatae watanganyika wengi tunachezewa mchezo wa mazingaubwe. Wiki inayokuja tutaletewa komedi nyingine bungeni na hakuna atakayekumbuka

1. Albert - konda
2. Clouds kuvamiwa -konda
3. Nape kutishiwa bastola
4. Mtuhumiwa wa utishiaji ni nani
5. RC amehojiwa
6. Mgonjwa katumwa hospitali
7....

Baada ya sarakasi zote,ishu ya kufoji majina imezikwa kabisa

Kutetea ujinga yakubidi uwe mjinga zaidi ili usione ujinga wa mwenzako
 
Back
Top Bottom