Nawapa Siri wazazi kuhusu kuwasaidia watoto wenu

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
17,964
45,451
Habari zenu

Watu wengi wanalalamika kuhusu watoto wao kuwa wanafanya Sana Uzinzi, uchafu, ushoga, wizi, tabia zote chafu chafu wanafanya wao tu.

Jambo la kuwa nalo makini hata Kama wewe husali au huamini uwepo wa Mungu hiyo Ni wewe tu.

Watoto ukitaka wawe mfano Bora katika jamii na wapate kuheshimika hakikisha unawapa vitu viwili tu

Malezi ya kiroho
Malezi sahihi ya wazazi.

Hizo tabia zako mbovu mbovu, kuongea maneno machafu, hakikisha haufanyi hivyo mbele ya watoto wako

Watoto wasio na Malezi sahihi ya kiroho ndo wanao fanya Mambo yote machafu , Uzinzi , nk.

Kama haumani hili Jambo nenda pale katika shule ya Kata hapa dsm then anagalia watoto ambao hawajalelewa katika malezi ya kiroho then hapo hapo nenda katika shule ya shekh kishiki ujionee watoto wa kike na kiume walivyo smart.

Viboko, jela Wala mahakama haviwezi mbadilisha Mwanao ili awe kijana Bora Ni kumpatia Spiritual care
 
Inasaidia kupunguza ila sio Kwa 100% labda asilimia 60 Hadi 80 na Mifano ipo Tena mingi TU mfano mdogo wachunguze mateja na wapiga debe wengi utakuta wamesoma saana dini hasa ya kiislam.

Panya rodi wengi wana majina ya kiislam na wamelelewa katika misingi yote kwa a dini na hata maeneo wanayotoka kama tandika, temeke, mbagala dini ya kiislam ndio imetawala kuliko dini zingine na ukiwachunguza wazazi wao wana misingi mizuri TU yadini ma waliwapeleka watoto wao kujifunza misingi ya dini kama ni uislam au ukristo.

Nini kifanyike, kweli kabisa wafundishwe misingi yote ya dini Kisha na wazazi wachukue majukumu Yao ya kuwalea Hawa watoto kama kuwajali kuwahudumia na wakipata changamoto yoyote wawe wa kwanza kuwasaidia.

Wazazi wengi akishawaandikisha shule kuwalipia ada, kuwapa chakula na malazi na kuwapeleka madrasa na mafundisho wanaona wamemaliza, Tena wazazi wa siku hizi wanawapeleka kabisa watoto shule za boarding kuanzia msingi Hadi sekondari, ila kumbe Kuna mengi zaidi ya hayo kama kutenga muda na watoto wako, kufurahi nao kuwapa majukumu wajihisi wanathaminiwa na kuwafanya wawe bize wasiwe na mda mwingi wa free.
 
Back
Top Bottom